Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

Ijumaa, 30 Agosti 2013

MWANAJESHI WA UN AUAWA NCHINI DRC

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mwanajeshi wake mmoja wa kutunza amani ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mapigano makali kati ya na wapiganaji wa waasi Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Farhan Haq, hata hivyo hajatangaza uraia wa wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa. Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa walitumia ndege za helicopta kuwasukuma nyuma wapiganaji wa M23 karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji...

UINGEREZA INAWEZA KUISHAMBULIA SYRIA BILA IDHINA YA UN

Uingereza huenda ikaanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria, bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Hayo ni kwa mujibu wa ushauri wa wataalamu wake wa masuala ya kisheria. Ushauri huo unasema, mashambulio hayo yatahitajika ikiwa yatatekelezwa ili kuzuia raia kuuawa, hata ikiwa wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Urussi na Uchina zikitumia kura zao za turufu kupinga mikakati za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria. Maafisa...

Alhamisi, 22 Agosti 2013

Star wa "Prison Break" Wentworth Miller (MichaelScolfield) amejiweka wazi kuwa yeye ni Shoga

  Star wa "Prison Break",  Wentworth Miller  a.k.a Michael Scofield, amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga), katika barua ya wazi aliyoiandika kwenda kwa Directoe wa St. Petersburg International Film Festival (tamasha la filamu la kimataifa la St. Petersburg) Muigizaji huyo (41) ameandika barua hiyo kukataa mualiko uliokuwa ukimtaka kuhudhuria tamasha hilo linalofanyika nchini kwao Russia na kwa mara ya kwanza kupitia barua hiyo amejitangaza kuwa yeye ni "Gay"...

Alhamisi, 8 Agosti 2013

Bilionea Wama dini Mererani auawa kwa risasi 20 Moshi

Moshi. Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana. Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri, aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. “Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli...

Ijumaa, 2 Agosti 2013

SAYANSI YA UFUFUAJI: MIAKA 20 IJAYO MADAKTARI WATAKUWA NA UWEZO WA KUWARUDISHIA UHAI WAGONJWA WALIOKATA ROHO!

Twende taratibu, hii ni taarifa ya kisayansi na sio ‘kiimani’ na imetolewa na daktari bingwa wa moyo wa Marekani. Sasa naomba uniruhusu nikuelezee nilichokutana nacho kuhusiana na habari hii. Dr Sam Parnia wa Marekani amedai kwamba kwa kupitia mbinu za kisasa za kitaalamu (kisayansi) kuna uwezekano wa kumrudishia uhai mgonjwa aliyekata roho ndani ya saa 24!! (hata mimi nimeguna) Dr ...

Jumatatu, 15 Julai 2013

CCM Chali, Chadema yaibuka kidedea Arusha

Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana. Katika uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na ambao ulichukuliwa kama kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na mvutano mkubwa, Chadema kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi. Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama...

Jumatatu, 1 Julai 2013

Rais Barack Obama awasili Tanzania

Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani Afrika. Ziara ya Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.  Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam. Obama amewasili Tanzania baada...

Page 1 of 5812345Next

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More