Waumini wa dini ya Kihindu wakienda kuoga ili kujitakasa na dhambi walizotenda
Mamilioni ya Wahindu wakiwa wamejipaka majivu tayari kuingia mtoni kuoga
Mamilioni ya wahumini wa madhehebu ya kihindu wakiwa katika foleni ya kuingia kuoga ili kujitakasa na dhambi zao
kina mama nao huchanganyika na wanaume wakati huo wa kutakasa dhambi zao kwa maji
Kutokana na wingi wa watu, treni kama unavyoona zinakuwa zimepakia hadi
dereva hapati pa kuangalizia. Kila penye upenyo panakaa mtu isipokuwa tu
kwenye magurudumu
Hii ndio hali halisi ya usafili wakati wa sherehe za kwenda katika mto ganges ili kusafishwa hdambi
ALLAHABAD, India, Mamilioni ya watu
wa dini ya Hindu hufanya ibada yakusafishwa dhambi zao kwa kuoga katika makutano ya
mito mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati inapokutana. Kwa mujibu wa Imani ya
Kihindu, binadamu anakuwa ametenda dhambi nyingi katika mzunguko wa mwaka na
hivyo anahitaji kutakaswa na dhambi zake. Waumini wanaume wanajipaka majivu
kuanzia utosini hadi unyayo na mara nyingi wanakuwa uchi wa mnyama ingawa
sikuhizi wengine wanapendelea kuvaa pajama, wanaingia kwenye mto huo na kuoga
nakuamini kuwa wameondolewa dhambi zao zote na nuksi nyingine zote.
Hii ni sherehe kubwa na inayodumu
muda mrefu kuliko zote duniani kwani inadumu kwa kipindi cha siku 55.
Mratibu mkuu wa sherehe hizo Mani
Prasad Mishra amesema karibu watu milioni 3 huwa wanauzulia katika ibada ya sherehe hizo za kuoshwa dhambi.
Zaidi ya watu milioni 110 hutarajiwa kuoga kwenye eneo hilo liitwalo SANGAM. Hili ni eneo ambapo
makutano ya mito ya GANGES, YAMUNA NASARASWATI . Sikukuu hii inategemea
mwonekano wa nyota zinazolandana angani. Baada ya nyota hizo kukaa katika mkao
fulani basi wahindu wanaenda kuoga ili kujitakasa na madhambi yao na kuepuka
kufa na kuzaliwa upya katika hali ya adhabu.
0 maoni:
Chapisha Maoni