Afrika Kusini imetangaza kuwa
itatuma wanajeshi Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kujumuika katika kikosi
maalumu cha Umoja wa Mataifa cha kuingilia kati nchini humo ili
kuwanyan'ganya silaha wapiganaji.
Taarifa hiyo imetolewa majuma
machache tu baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa Jamhuri ya
Afrika ya Kati katika hali ya kutatanisha.
Upande wa upinzani umelaani mpango huo, wanasema kuwa haukufikishwa mbele ya bunge.
Waziri kivuli wa Ulinzi wa chama cha Democratic
Alliance, David Maynier, alisema kuna hatari ya wanajeshi zaidi kupoteza
maisha yao.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa
idhini mwisho wa mwezi uliopita kutuma kikosi kitachoweza kupigana na
kuingilia kati katika Congo.
0 maoni:
Chapisha Maoni