KIONGOZI Mkuu wa jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Songea , Mhashamu Askofu
Norbeth Mtega amejizulu. Taarifa za kujiuzulu kwa kiongozi huyo
zilipatikana jana saa saba mchana zikieleza kuwa Askofu Mtega alikuwa
ametembelea Abasia ya Wabeneditini iliyopo Hanga wilayani Namtumbo
mkoani Ruvuma.
Mhashamu Askofu Mtega alipokuwa katika abasia hiyo ya Hanga
aliwatangazia waumini na watawa wa Shirika la Wabeneditini kuwa kuanzia
sasa yeye siyo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea.
Alisema badala
yake jimbo hilo litashikiliwa na Askofu wa jimbo la Iringa, Taricisius
Ngalalekumtwa ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la maskofu Tanzania
mpaka atakapopatikana kiongozi mwingine wa kushika wadhifa huo.
Kwa
mjibu wa kiongozi mmoja wa Parokia ya Kanisa hilo ambaye hakutaka jina
lake litajwe gazetini, hizo ni taarifa za kweli kuwa Mhashamu Askofu
Mtega ametangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Alisema hata wao hawajui kilimkuta nini maana hata hajawahi kudokeza kuhusiana na jambo hilo.
“Watumishi
wote hatukujua kinachoendelea tumeshangazwa kuwa Askofu Mtega anatamka
kwa kinywa chake kuwa yeye kuanzia sasa siyo Askofu Mkuu wa Jimbo hili
la Songea jambo ambalo wote tulibaki midomo wazi na hatujui kuna
nini,”alisema mtumishi huyo.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki
Jimbo Kuu la Songea katika maeneo mbalimbali mjini Songea nao
walionyesha kushitushwa na taarifa hizo.
Askofu huyo alilipokea jimbo hilo na kuliongoza baada ya aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo marehemu Jacobo Komba kufariki dunia.
0 maoni:
Chapisha Maoni