Dodoma. Baadhi ya wabunge na wadau wa elimu wametaka Serikali
kutoishia kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, bali iwajibishe
Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) kwa kufelisha wanafunzi.
Akizungumza kuhusu kauli ya Serikali kufuta
matokeo hayo jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza alisema
taarifa ya tume ingekuwa tofauti na ilivyotolewa ilikuwa isababishe
vurugu nchini.
“Kauli hii ya Serikali ndiyo iliyotegemewa na
wadau wa elimu, tume wangefanya vinginevyo tunge-riot (fanya vurugu),
kwa sababu matokeo yaliyotolewa na Necta siyo halisi. Tume imefanya kazi
nzuri na kilio cha wanafunzi kimesikika,” alisema Rweikiza na kuongeza:
“Sasa na hili nalisema bila kificho, Necta lazima
wawajibishwe kwa sababu wanafunzi wanne wamejiua kwa matokeo hayo yasiyo
halali, kule kwangu (Bukoba Vijijini) wanafunzi wamekata tamaa na
wanaolewa. Hiyo yote ni hasara ambayo haina wa kuilipa.”
Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo
Marekani, mtihani wa mwisho hauchukuliwi kama kigezo kwa sababu
inategemea mwanafunzi jinsi alivyoamka siku ya mtihani na kwamba,
wanatumia mitihani iliyopita kufanya tathmini yao.
“Necta ni aibu tangu uhuru hawajawahi kufanya
mambo ya ajabu kama hivi. Lazima wawajibishwe kwani wanafunzi wamepoteza
maisha kwa sababu yao,” alisema.
Mbunge wa Ngara, Deogratias Ntukamazina alisema
suala la mfumo wa kuweka viwango haliwezi kuchukuliwa peke yake kwa
kusababisha matokeo mabaya.
Ntukamazina ambaye kitaaluma ni mwalimu, alisema
suala la kufeli kwa wanafunzi analigawa sehemu mbili; taaluma na maslahi
kwa walimu.
Ombi la ziada lazima liangaliwe tofauti na hivi
sasa. Serikali inapojaribu kutumia kigezo kimoja cha upangaji matokeo
kuwa ndicho kilichosababisha kufeli kwa wanafunzi hao.
“Suala la vitabu, vitendeakazi, mazingira ya kazi, walimu kukata tamaa hatutakiwi kupuuza haya mambo,” alisema Machali.
Alisema suala la maslahi ya walimu lazima Serikali
ikae nao hata kama siyo kiwango wanachotaka, lakini iwaongezee kidogo
na kwamba, kufutwa kwa matokeo hayo ni jambo zuri lakini siyo mwisho wa
tatizo, huku akiongeza kuwa hata alama zikipunguzwa aliyeandika zombi
kavaa viatu hatapata kitu.
“Unabadili mfumo wa kupanga matokeo na madaraka,
mathalan mwaka jana daraja D ilikuwa alama 35, zamani ilikuwa 21. Hivi
hawa wanafunzi umewaandaa kwa sababu walikuwa wameshajipanga kwa 21,
huyu wa Zombi hata ungempa mtihani kutwa nzima asingeweza kupata hizo
alama,” alisema.
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
0 maoni:
Chapisha Maoni