Lushoto. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Lushoto, mkoani Tanga, kimepata pigo baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwekitui, Miraji Kassim kujiuzulu, kufuatia kile alichokielezea kuwa ni kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzie ngazi ya kijiji ambao wote ni wa CCM.
Mwenyekiti huyo ambaye alichaguliwa Aprili 27
mwaka huu katika uchaguzi mdogo, aliwashangaza wafuasi wake baada ya
Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho Athumani Kibiriti, kusoma baraua ya
kujiuzulu kwake katika mkutano wa hadhara.
Mkutano huo uliitishwa na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teklonojia, January Makamba.
Akithibitisha hatua hiyo katika mkutano huo
uliohudhiriwa na umati mkubwa wa watu, Mtendaji Kibiriti alisema
mwenyekiti huyo amejiuzulu kwa ridhaa yake mwenyewe baada ya kukosa
ushirikiano.
Alisema alipokea barua ya kujiuzulu kwa kiongozi
huyo siku moja kabla ya mkutano huo na kwamba hakuwa amejua mwenyekiti
wake ameandika ujumbe gani.
Alipotakiwa kueleza mahali alipo mwenyekiti huyo
ili aweze kufungua mkutano huo, uliokuwa ukijadili maendeleo ya kijiji
na wananchi kutoa kero zao, mtendaji alitoa barua ya mwenyekiti huyo
kujiuzulu. Kitendo hicho kiliwafanya wafuasi wa Chadema kutoka ndani ya
ukumbi wa mkutano wakiwa wanapiga kelele na kusema hawakubali kujiuzulu
kwa mwenyekiti wao.
0 maoni:
Chapisha Maoni