Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba bomu limelipuka katika kanisa katoliki, parokia mpya ya Olasiti iliyokuwa inazinduliwa leo jijini arusha.
Bomu hilo
limelipuka wakati waumini wa kanisa hilo
wa wakijiandaa na misa ya uzinduzi wa
parokia hiyo.
Mpaka
sasa haijajulikana idadi kamili ya watu
waliojeruhiwa ama kupoteza maisha lakini taarifa za awali zinasema
kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa hospitali
Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama....
Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo..
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni
balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo baada ya
kunusurika katika mlipuko huo
Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )
Kanisa lililolipuliwa na bomu Parokia ya Olasiti kama linavyoonekana
Baadhi ya majeruhi waliokumbwa na zahma hilo la mlipuko wa Bomu walipokuwa katika ibada ya jumapili
Askari wa kutuliza ghasi wakiwa eneo la tukio la kanisa
0 maoni:
Chapisha Maoni