Alhamisi, 2 Mei 2013

AIBU YA KARNE CAMP NOU, BARCELONA YAPIGWA JUMLA 7-0, BAYERN YATINGA FAINALI

Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani jana iliidhalilisha tena Barcelona ya Uhispania kwa kuichapa mabao matatu kwa nunge tena katika uwanja wa nyumbani wa Camp Nou.
Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kugombea Klabu Bingwa barani Ulaya iliyochezwa wiki moja iliyopita, Bayern Munich ilikuwa imeitandika Barcelona mabao manne kwa sifuri.
Matokeo hayo yana maana kwamba fainali ya michezo hiyo itazikutanisha timu mbili za Ujerumani, Bayern Munich na Borussia Dortmund katika uwanja wa Wembley mjini London hapo tarehe 25 mwezi huu wa Mei.
Dortmund imefanikiwa kuingia fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya licha ya kuchapwa mabao mawili kwa sifu na Real Madrid katika mechi iliyochezwa Jumanne iliyopita. Katika mzunguko wa kwanza wa mechi za nusu fainali Borussia Dortmund iliichapa Real Madrid mabao wanne kwa moja.

Kila mmoja alikuwa na lake la kusema, wengine walithubutu kutamka kuwa bora Real Madrid wamekufa kiume ingawa kipigo ni kipigo.

Barcelona wameaga michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu kwa aibu ambayo itabaki katika historia yao kwa kipindi kirefu baada ya kufungwa jumla ya mabao 7-0.
 
Mabao 4-0 mjini Munich na 3-0 ndani ya Camp Nou, ni aibu ya aina yake, mbaya zaidi wageni Bayern walionekana kuutawala zaidi mchezo.
Mabao ya Bayern yalifungwa na Robben, Pique akajifunga na Muller akamalizia la tatu.
 
Lionel Messi ambaye ni sawa na mkombozi alikuwa kwenye benchi akiishuhudia Barcelona ikiumizwa nyumbani na Wajerumani hao.

Mara kadhaa, Aarjen Roben na Frank Ribery wa Bayern ndiyo walionekana kuwa matatizo makubwa kwa beki ya Barcelona iliyoongozwa na Gerard Pique.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More