Jumamosi, 20 Aprili 2013

WATAALAMU WA AFYA NA LISHE WAENDESHA SEMINAR YA KUONGEZA VIRUTUBISHO KWENYE CHAKULA JIJINI DAR ES SALAAM



Semina ya kuongeza virutubisho kwenye chakula ili kukifanya chakula kiwe bora kwa afya na kukuza kinga ya mwili. Semina iliendeshwa tar 18 - 19/04/2013 na ilimalizika kwa ushindi mkubwa sana katika ukumbi wa Land mark Hotel. LENGO LA SEMINA HII LILIKUWA NI;
Ushawishi
(Persuasion stage
1.Uelimishaji – viongozi mbalimbali wa kisiasa na kidini, waandishi wa habari, wafanyabiashara wakubwa
na wadogo, asasi zisizo za kiserikali, waatalamu wa vyakula na lishe,wahudumu wa afya. nk
2.Shughuli za ushawishi – mashuleni, kliniki, maigizo na ngoma zenye ujumbe ,
sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa jamii husika.
Uhamasishaji
•Kutambulisha Nembo (logo) kwenye jamii.
•Kuhamasisha ulaji wa vyakula vilivyo ongezewa virutubishi/ kuulizia vyakula hivyo
 Ushawishi
 •Kuelimisha jamii yetu juu ya faida za ulaji wa vyakula vilivyo ongezewa virutubishi.
• Kuendelea kuulizia vyakula hivyo
Hatua ya Pili.
Lengo kuu katika hatua hii ni kuelimisha jamii yetu juu ya faida na umuhimu wa kula vyakula vilivyo ongezewa virutubishi,wakati huo huo kuelimisha jamii jinsi ya kutambua Nembo (logo) kwenye vyakula vilivyo ongezewa virutubishi.
 Takwimu za tatizo la upungufu wa nishati na utomwili (protini)
Asilimia 16 ya watoto chini ya miaka mitano wana uzito pungufu kulinganisha na umri (Underweight Wt/Age)
Asilimia 42 ya watoto wana urefu pungufu kulinganisha na umri (Stunted Ht/Age)
Asilimia 5 ya watoto ni wakondevu (Wasted Ht/Wt)
Asilimia 23.2 Ya Wanawake walio katika umri wa kuzaa wana uzito mdogo na asilimia 10.7 Wana uzito uliozidi

 Upungufu wa virutubishi
      Upungufu wa virutubishi  (vitamini na madini) au njaa iliyofichika ni mojawapo ya tatizo kuu la kilishe nchini; upungufu huo ni wa virutubishi   kama vile :
Upungufu wa madini chuma
Upungufu wa vitamini  A
Upungufu wa madini joto
 

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More