Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania, imeagiza kuwa filamu ya marehemu Steven Kanumba 'Love&Power' inayotarajiwa kuingia sokoni rasmi leo, inatakiwa kuangalia na watu wenye umri wa kuanzia miaka 16 na kuendelea.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joyce
Fisoo aliagiza umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16
na kuendelea.
"Baada ya kuikagua filamu hii tumependekeza umri
stahiki wa kutazama filamu hii ambao ni kuanzia umri wa miaka 16,"
alisema Fisoo.
Akizungumza Msemaji wa filamu hiyo Myovela Mfwaisa
alisema Love&Power ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na
familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu
na michezo ya kuigiza Tanzania.
"Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’. "
“Filamu ya Love & Power imetengenezwa na
kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na Steps Entertainment
Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power
imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania kama
Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace
Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na
marehemu na kuongozwa na Steven Kanumba."
Alisema watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd na pia imetengenezwa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti tofauti.
Myovela aliwaomba wasanii kuwa walinzi wa kazi hiyo ya marehemu kwa kupambana na maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu.
"Tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala
halali yenye nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi
kwa wasanii wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo
nunua filamu ya Love & Power halali." alisema Myovela.
CHANZO: mwananchi
CHANZO: mwananchi
0 maoni:
Chapisha Maoni