TUMEUANZA mwaka mpya kwa mambo yale yale kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Akili za wengi zipo kwenye harakati za maendeleo, karo za watoto wao na ugumu wa maisha unaowakabili wengi.
Kingine ni kodi ya pango, mdudu ambaye hunyanyasa wengi hasa wa kipato ha chini.
Lakini, kila anayemiliki nyumba katika
maeneo ya mijini hasa hasa katika majiji kama Mwanza, Dar es Salaam,
Arusha na Mbeya, hakika anaitwa mbarikiwa.
Anaitwa mbarikiwa kwa sababu nyingi.
Kwanza, ardhi ni kitu cha thamani, pili ujenzi ni gharama na
anayefanikiwa…hakika huyo amejikwamua kiuchumi na kijamii.
Wamiliki wengi wa nyumba wapo katika makundi
kadhaa, kuna wanaoishi katika nyumba zao bila kupangisha na wengine
wanaozikodisha na kujipatia fedha.
Dhamira nzima ya wino huu inadondokea kwa wale wanaopangisha nyumba zao yaani…wenye nyumba.
Ama kwa hakika wenye nyumba wengi wamekuwa kama
miungu watu. Baadhi yao wamejivika kilemba cha utukufu na kutumia
rasilimali zao kwa unyanyasaji wa hali ya juu.
Mara kadhaa unapokwenda kutafuta nyumba si ajabu
ukapewa masharti ya ajabu. Kwa mfano, wapo wanaoambiwa wasipike aina
fulani ya mboga, wasiwe na watoto au wakanyimwa kuleta wageni.
Lakini, pia wapo wenye nyumba ambao
wanataka wamtawale mpangaji kama mtoto wao kwa kumwekea masharti hata ya
kutoka na kurudi saa ngapi.
Haya yote yanasababishwa na sheria butu
za nyumba nchini ambazo husababisha wenye nyumba kujigeuza miungu kwa
sababu tu wanamiliki nyumba.
0 maoni:
Chapisha Maoni