Arusha: Kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.
Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia
Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha
Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa
kwake kungehatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha
kwa askari hao usiku huo wa kuamkia juzi, Lema alithibitisha kuwapo kwa
polisi nje ya nyumba yake:
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga
mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi wangu na
mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui alisema mahojiano ya
mteja wake na polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa 7:50
mchana hadi saa 11:15 jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja
tatu walizodai kwamba zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati
alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA).
Maneno hayo yanayotafsiriwa na polisi kuwa ni
uchochezi ni pamoja na “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni
woga” na “Nimepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa atafika,
asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya
msingi ya kupatiwa ulinzi.”
Kauli nyingine ni “Hawa ndio viongozi wetu
(akimaanisha mkuu wa mkoa), tunaowategemea wanakuja kwenye matatizo
wakijivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off.”
Lema anadaiwa kutamka maneno hayo baada ya Mulongo
kugoma kuzungumza na wanafunzi kisha kurejea ndani ya gari akitaka
viwepo vipaza sauti, kitendo kilichowafanya wanafunzi kuanza kumzomea
kabla polisi kuanza kulipua mabomu ya machozi na kumwondoa eneo la tukio
mkuu huyo wa mkoa.
Lema na Mulongo wote walikwenda IAA kutokana na
tukio la kuuawa kwa kuchomwa kisu kwa aliyekuwa mwanafunzi wa taasisi
hiyo, Henry Kago.
Baada ya vurugu hizo Mulungo alimtuhumu Lema kuandaa mazingira ya yeye kuzomewa .
Wakati hayo yakiendelea, askari katika kituo
anakoshikiliwa Lema jana asubuhi walivutana vikali na ndugu wa mbunge
huyo pamoja na uongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha baada ya kumpa dakika
moja kunywa chai aliyoletewa na kukataa asipewe dawa ya meno kutoka kwa
mkewe, Neema.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinasema
kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chadema ulilazimika kumtuma wakili wa
Lema, Method Kimomogoro kwenda Kituo cha Kati cha Polisi Arusha kujua
sababu za polisi kufanya hivyo.
Mmoja wa ndugu wa Lema alisema polisi walimpa mbunge huyo dakika
moja tu kunywa chai na kwamba muda huo ulipokwisha walimwongezea dakika
nyingine tatu na kwamba zilipomalizika walimwamuru arejee mahabusu.
Wakati polisi wakifanya hivyo, tayari walikuwa
wamekataa asipewe dawa ya meno aliyopelekewa na mkewe, Neema na kwamba
matukio hayo yalizua mvutano mkali baina yake (Lema) na polisi waliokuwa
kituoni hapo.
Mdee, Nassari kukutana na Mulongo
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Nassari aliliambia gazeti hili jana kwamba wameamua kutoka Dodoma hadi Arusha kwa ajili ya “kushughulikia suala hilo.”
“Jumatatu tunatarajia kuonana na mkuu wa mkoa na
tayari nimempa taarifa. Tunataka kuzungumza naye kilichotokea na hali ya
kisiasa kwa sasa Arusha,”alisema Nassari.
Alisema wao kama wabunge, hawawezi kukaa kimya
wakati kunaonekana kuna mgogoro baina ya mkuu huyo wa mkoa na mbunge
mwenzao, Godbless Lema ambao unakiuka haki za kibinadamu.
“Tutazungumza naye na tutatoa ushauri wetu …na
mimi kama mbunge wa Mkoa wa Arusha, nadhani nina nafasi ya kushauriana
na mkuu wa mkoa kuhusiana na hali ya mambo ilivyo sasa Arusha,”alisema
Nassari na kuongeza:
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
Hata hivyo, juhudi za kumpata jana mkuu wa Mkoa wa
Arusha, kuelezea kama amepokea ujumbe kutoka kwa wabunge hao,
zilishindikana kutokana na kuwa katika mapokezi ya marais watano wa nchi
za Afrika ya Mashariki.
Chadema kumzomea RC
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani
Golugwa alisema wafuasi wa chama hicho wataendelea kumzomea Mulongo kila
watakapomwona hadi pale atakapobadilika kifikra, kimwenendo, maneno na
vitendo kuhusiana na uhalali wa Chadema na viongozi wake katika uongozi
wa umma waliokabidhiwa kisheria.
“Kama kupigiwa makofi na kushangiliwa anapofanya vyema kazi yake,
vivyohivyo mkuu wa mkoa ategemee kukumbana na
zomeazomea kubwa kuliko aliyopata Uhasibu iwapo hatabadilika kiutendaji
kwa kufanya kazi za kisiasa badala ya kuhudumia umma wote bila kujali
tofauti za kiitikadi kisiasa,” alisema Golugwa.
Katika mkakati wake, Chadema kimetishia kumburuta mahakamani
Mulongo kwa tuhuma za kuzusha uongo na kumtishia Lema kwa maneno makali.
“Mawakili wetu wanaendelea na utaratibu wa
kufungua kesi ya kumshtaki mkuu wa mkoa kwa kosa la kumtishia kwa maneno
makali Lema na pia kutoa maneno ya uzushi, upotoshaji na uongo,”alisema
Golugwa.
Chadema pia walisema askari polisi waliomkamata
Lema hawakuwa na kibali cha ofisi ya Spika wala hati ya kukamata kutoka
kwa ofisa wa jeshi hilo kama sheria inavyoelekeza.
CCM Arusha
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
0 maoni:
Chapisha Maoni