Sanamu la rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Machel huko Chimoio
Mapigano kati ya wafuasi wa RENAMO na polisi yameangamiza maisha ya watu wanne na 13 kujeruhiwa katika mkoa wa kati wa Sofala.
Nchini Msumbiji watu wanahofia hivi sasa baada ya miaka 20 ya amani,vita
vya wenyewe kwa wenyewe visije vikaripuka upya kati ya waasi wa zamani
wa RENAMO na serikali.
Hali imevurugika kufumba na kufumbua .Inatia wasi wasi na kuzusha hofu
baada ya wanamgambo waliokuwa na silaha kutoka chama cha ukombozi wa
taifa ,chama kikubwa cha upinzani nchini Msumbiji-RENAMO kuwashambulia
wanajeshi wa kikosi cha kuingilia kati haraka-FIR katika mtaa wa
Muxungué.
Kwa kufanya mashambulio hayo ,wafuasi wa RENAMO walitaka kulipiza kisasi
dhidi ya polisi na pia kuwafungua wenzao waliowekwa korokoroni.Siku
moja kabla ya hapo wanajeshi wa kikosi cha kuingilia kati haraka
waliutawanya mkutano wa wafuasi wa RENAMO huko MUXUNGUÉ na kuwakamata
wanachama 15 wa RENAMO.Kwa mujibu wa polisi wanachama hao walikuwa
wakifanya mazoezi ya kijeshi.
Eti RENAMO wanaweza kweli kuanzisha vita?
Katika miji mengine pia mfano wa Gondola katika mkoa wa kati wa
Manica,machafuko yamekuwa yakiripotiwa wiki na miezi iliyopita kati ya
polisi na wafuasi wa RENAMO.Hali inatisha zaidi katika mkoa wa
Sofala-ngome ya zamani ya RENAMO.Katika enzi za vita vya wenyewe kwa
wenyewe,huko ndiko RENAMO walikokuwa na makao makuu yao katika mbuga ya
wanyama ya Gorongosa,wenyewe wanayaita "Casa Banana."
October mwaka jana kiongozi wa RENAMO Afonso Dhlakama na wanachama
kadhaa wengine wa chama hicho,walirejea katika kituo hicho cha zamani
cha uongozi wa wanamgambo.Kwa kufanya hivyo alitaka kulalamika dhidi ya
kutengwa RENAMO na serikali inayoongozwa na chama cha FRELIMO.Kila mara
amekuwa akitishia kurejea upya msituni na kuanzisha tena vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini Msumbiji.Sultan Musa ,mwakilishi wa wakfu wa
Konrad Adenauer nchini Msumbiji anahisi kitisho cha kuripuka vita vya
wenyewe kwa wenyewe kipo.Anahisi serikali haizingatii kwa makini
mazungumzo pamoja na RENAMO.Na kuambatana na katiba na makubaliano ya
amani ya Roma,serikali hailazimiki kufanya hivyo kwasababu mazungumzo
yanabidi yafanyike bungeni..Ukweli lakini ni kwamba RENAMO haina nguvu
bungeni kuweza kushawishi maamuzi na ndio maana wanashikilia kuzungumza
na serikali."
Frelimo wamefaidika na makubaliano ya amani
RENAMO wanaonyesha kukata tamaa.Wanamgambo hao wa zamani waliokuwa wakiangaliwa kama wenye kuelemea upande wa kambi ya magharibi,wameondoka patupu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika nchini humo.Walioibuka na ushindi ni FRELIMO waliokuwa wakielemea upande wa kambi ya mashariki.Wanafaidika pia na neema ya mali ghafi iliyogunduliwa nchini humo.
0 maoni:
Chapisha Maoni