BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA
(BAVICHA) IRINGA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la
Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Iringa limesikitishwa na kitendo cha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujivika jukumu la
kupachika raia vyeo ambavyo haviko kwenye utaratibu wa CHADEMA
wala BAVICHA ilili kutimiza lengo la kujaribu kukipaka matope CHADEMA
na BAVICHA.
Tunapenda
kuufahamisha umma kuwa taarifa zilizotolewa na Bwana Kamuhanda, RPC wa Iringa
na na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Bwana
Athanas Mongo (mtuhumiwa wa ujambazi) ni Kamanda wa Vijana wa CHADEMA
Mkoa wa Iringa ni uongo na uzushi wenye hila za makusudi za kujaribu
kuharibu taswira ya BAVICHA na CHADEMA kwa umma.
Bwana
Mongo anayetuhumiwa kwa ujambazi si Kamanda wa BAVICHA Mkoa wa Iringa na
wala Muongozo wa Mabaraza ya chama unaosimamia mabaraza yote
likiwemo BAVICHA kwa upande mmoja na Katiba ya CHADEMA kwa upande
mwingine haina na wala haitambui cheo ambacho RPC Kamuhanda kamvisha bwana
Mongo.
Tunavyojua
sisi hicho ni cheo kinachotumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sasa labda RPC
Kamuhanda ni mzoefu wa kukariri vyeo vya CCM. Yeye anajua hilo.
Mongo ni
mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo
chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA. Ni Mtanzaniamwenye haki ya kuwa
mwanachama wa chama chochote cha siasa. Kutuhumiwa kwake kwa
masuala ya uhalifu hakupaswi wala hakuwezi kuhusiswa na CHADEMA wala
BAVICHA.
BAVICHA
tunamuonya RPC Kamuhanda kuacha mara moja tabia ya kukurupuka na
kutokuwa makini katika utendaji kazi kiasi cha kuingilia na kujaribu
kubaka Katiba ya CHADEMA na Kanuni za BAVICHA ili tu kukidhi haja yake ya
kuipaka matope CHADEMA baada ya kushindwa hila hizo kwenye tukio la mauaji ya
Mwandishi wa habari, marehemu Daudi Mwangosi kule Nyololo.
Bila
shaka ni ukurupukaji na kukosa umakini kama huu, ndiyo uliosabisha RPC
Kamuhanda akakiuka misingi ya utawala bora kama ilivyoelezwa na Ripoti ya
Uchunguzi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala juu ya mauaji ya
Mwangosi.
Uchunguzi huo wa THUB ambacho
ni chombo cha serikali chenye majukumu ya kikatiba na kisheria kuhusu masuala
ya haki za binadamu ulibaini kuwa RPC Kamuhanda mnamo tarehe
02/09/2012 alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha
11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa
Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa “Officer
In-charge” wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo amri aliyoitoa haikuwa
halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri
hiyo. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya
utawala bora.
Kimsingi baada ya taarifa hiyo
ya uchunguzi uliofanywa na chombo cha serikali, unaoonesha kuwa utendaji mbovu
wa Kamuhanda, RPC huyo pamoja na polisi wenzake walioshiriki katika tukio
la Nyololo kumuua mwandishi wa habari, kisha wakaanza kufanya propaganda za
kuipaka matope CHADEMA ili kuwanusuru wao, alipaswa kuwa amejizulu au
amefukuzwa kazi na kushtakiwa mahakamani kutokana na tukio hilo la mauaji ya
Mwangosi, kama ambavyo CHADEMA imeshauri mara kadhaa, ikiwemo kuandika barua
kwa Rais Jakaya Kikwete.
Imetolewa
na leo tarehe 10/04/2013 Mkoani Iringa na:
Joseph Nzala Lyata
Mwenyekiti BAVICHA
Mkoa wa Iringa
0757925514
0 maoni:
Chapisha Maoni