Ni wale tu wanaopenda demokrasia ndio wako hapa, Rais wa bunge la
Ufaransa alisikika akisema kwa satui ya ukali wakati wa kupiga kura,
ambapo vurugu zilianza kutimka kutokana na kugawanyika wka mawazo ya
wabunge hao, huku kinara wao akiwa amevalia nguo za rangi ya pink, rangi
ambayo imeasiliwa na wanaopinga vitendo vya ushoga nchini humo.
Kura 331 za kukubali kati ya zile 225 za kupinga kupitisha kwa sheria
hiyo ndizo zilizopelekea taifa la Ufaransa kuwa taifa la 14 duniani
kuidhinisha vitendo hivyo, licha ya upinzani mkubwa ambao hutokea mara
kwa mara nchini humo, ikiwemo leo bungeni.
Waziri wa haki
nchini Ufaransa, Bi. Christiane Taubira akihutubia wabunge wakati wa
maswali kwa serikali, kwenye baraza kuu jijini Paris.
Kutokana na kuchukizwa kwa baadhi ya wananchi kufuatia mpango wa
serikali wa kuidhinisha muswada huo, hali ya usalama kwa baadhi ya watu
wanaojihusisha na tabia hizo wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa
wanaharakati na wananchi wanaopinga, huku kinara mmojawapo wa kuunga
mkono vitendo hivyo akipokea barua jumatatu iliyo na unga wa silaha (gun
powder), ikiwa ni ishara ya kumtahadharisha aachane na mambo yake
vinginevyo atadhuriwa.
Katika hatua nyingine, mshabiki mkubwa wa ndoa za jinsia moja nchini
humo amekuwa waziri wa haki, Bi Taubira, ambaye amesema kuwa anaamini
ndoa za kwanza kwanza zitakuwa mnamo mwezi juni, hali ambayo italeta
hamasa na kubadilisha upeo wa baadhi ya watu wanaipinga vitendo hivyo.
"Naamini wale wanaopinga watajawa na furaha pale ambapo ndoa hizo
zinafungwa, ndugu, jamaa na familia wakishuhudia." Bi Taubira anasema.
Wakati rais François Hollande alipoahidi kushughulikia kuruhusu ndoa za
jinsia moja, haikuwa na utata kwa sana, lakini jambo hilo limekuwa
likimgusa karibu kila mtu, na kupelekea umaarufu wa rais Hollande
kushuka sana.
wabunge wa chama cha msimao mkali cha UMP, kupitia mbunge wake, Laurent
Wauquire, ameiambia serikali kuwa licha ya wao kuforce kupitisha jambo
hilo kuwa sheria, lakini hiyo haitowazuia watu kuingia mtaani na
kuandamana kulipinga jambo hilo, wakitaka lirudishwe kwenye hatua ya
muswada ili baadae liondolewe kabisa.
Hali yamtaani karibu na bunge ilikuwa tofauti, watu kadhaa wakishuhudiwa
kuwa na chupa za wine na champagne, wakijipongeza kwa kunywa, akili zao
zikichangamka kwa kujua kwamba sasa wanaweza kuoana jinsia moja na pia
kuasili mtoto kama ambavyo haki hiyo ipo kwa wanandoa wowote wale.
Kwa upande mwingine, wapinzani wa ndoa za jinsia moja nao pia
walionekana mtaani wakipinga hatua hiyo huku wakionesha alama ya vidole
viwili kwenye maeneo mengi akama ambavyo GK imeshuhudia kwenye vyombo
kadhaa vya habari.
Mwezi Aprili unashuhudia nchi ya pili ikipitisha muswada huu, huku New
Zealand likiwa taifa la kwanza Asia Pacific kuruhusu ndoa za jinsia
moja, ikiungana na mataifa mengine ya Ulaya kama vile Uholanzi,
Ubeljiji, Spain, Norway, Denmark, Ureno, Iceland na Sweden, ambayo kwa
muda sasa imekuwa kimbilio la Waafrika wanaounga mkono ndoa za namna
hiyo, huku wakitimkia hukokufunga ndoa zao. Na iwapo Rais wa Ufaransa
atatia saini kwenye muswada huo, basi Wafaransa watakuwa wamepewashiwa
taa ya kijani kwa ajili ya vitendo hiyvo
0 maoni:
Chapisha Maoni