Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.
Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini
wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu,
kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana
kijana.
Dawa hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye
vyakula vya kila siku, zina uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa
mwanafunzi au mfanyakazi.
Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ’.
Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka.
“Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda
katika mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya
juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula
tunavyotumia na siyo kemikali.”
Haule ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea
anasema kwamba mtindo wa maisha na vyakula vinavyoliwa na watu mara kwa
mara kwa sasa huufanya mwili kuhifadhi sumu nyingi mwilini.
Anasema kuwa dawa hizo pia zina uwezo kuondoa sumu
mwilini na kuufanya mwili wa binadamu kurejesha rangi yake halisi na
kumeng’enya vizuri chakula anachokula.
Haule anayefanya kazi pamoja na Shirika la Nativa
linalotengeneza dawa hizo la nchini Afrika Kusini, anaeleza kuwa tangu
kuingiza dawa hizo nchini watu wengi wamejitokeza kuzihitaji.
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA), Gaudensia Simwanza anasema kuwa mamlaka hiyo inazitambua dawa
hizo kama virutubisho vya chakula, zimesajiliwa na ni salama kwa
binadamu.
“Tuna taarifa kuwa bidhaa za ‘Go Woman’ na ‘Go Man’ zimesajiliwa na ni salama,” anasema.
Dawa nyingine zinazotengenezwa na kampuni hiyo
zimetajwa kuwa na uwezo wa kuunda mifupa kwa watu wazima na majeraha ya
wagonjwa wa kisukari.
Source: gazeti la Mwananchi
Source: gazeti la Mwananchi
0 maoni:
Chapisha Maoni