Dodoma.Tanzania imetajwa kama nchi ya mwisho
Afrika Mashariki kwa ukusanyaji wa kodi kutoka kampuni za simu kutokana
na kutokuwa na utaratibu mzuri wa kusimamia makusanyo hayo.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Muhambwe, Felix
Mkosamali alipokuwa akiuliza swali bungeni akitaka kujua kampuni hizo za
simu zimepata faida kiasi gani kwa kipindi cha miaka mitano na Serikali
imafaidika na nini.
“Nataka kujua kwa sasabu kwa mwaka 2010 Kenya
imekusanya dola 79 milioni, Uganda dola 36 milioni, Rwanda dola 14
milioni na Tanzania dola 1 milioni, kitu ambacho ni aibu,”alisema
Mkosamali na kuongeza:
“Tunashindwa na Rwanda ambayo idadi ya watu wake ni sawa na wateja wa Vodacom waliopo hapa nchini.”
Akitoa ufafanuzi juu ya hilo Naibu Waziri wa Ofisi
ya Makamu wa Rais (Mazingira), Charles Kitwanga alisema ni muhimu kujua
kodi gani inayozungumziwa kwa kuwa zipo za aina nyingi.
Kitwanga ambaye alikuwa akitoa maelezo hayo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, hata hivyo alisema kuwa mtambo wa kufuatilia kampuni za simu umeshawasili nchini ili kuhakikisha zinalipa kodi inayostahili.
Kitwanga ambaye alikuwa akitoa maelezo hayo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, hata hivyo alisema kuwa mtambo wa kufuatilia kampuni za simu umeshawasili nchini ili kuhakikisha zinalipa kodi inayostahili.
Alisema kinachosubiriwa hivi sasa ni kurekebishwa
kwa kanuni zinazosimamia kampuni hizo ili mtambo huo uweze kuanza
kufanya kazi mapema mwaka huu.“Mpango huu wa kuwekwa mtambo wa
kufuatilia simu zote utaanza kufanya kazi mwaka huu hivyo
tusubiri,”alisema Kitwanga.
0 maoni:
Chapisha Maoni