Mtu mmoja ameuawa katika makabiliano makali nje ya
kanisa la kikopti kufuatia mazishi ya wakristo wanne wa kanisa hilo
waliouawa katika ghasia za kidini siku ya Alhamisi.
Waombolezaji waliokuwa wanatoka katika kanisa hilo walikabiliana na wenyeji wa eneo hilo nje ya kanisa.
Polisi walifyatua gesi ya kutoa
machozi kujaribi kuwatawanya waandamanaji. Zaidi ya watu 80 walijeruhiwa
kwa mujibu wa shirika la kitaifa la habari.
Wizara ya afya ilisema kuwa mtu mmoja aliuawa katika ghasia hizo. Waombolezaji awali walikuwa wakiimba nyimbo za kupinga serikali ya rais Mohammed Morsi.
Walioshuhudia vurugu hizo waliambia wanahabri
kuwa ghasia zilianza baada ya umati wa watu kuvamia kikundi cha
waombolezaji walipokuwa wanaondoka kanisani kwa kuwarushia mawe na
mabomu ya petroli. Wakati huo pilisi walikuwa wachache sana katika eneo
hilo.
Wakristo nao walijibu mashambulizi dhidi yao kwa
kuwarushia mawe watu hao hadi polisi walipowasili katika eneo hilo na
kujaribu kusitisha vurugu kwa kuwarushia watu gesi ya kutoa machozi
Duru zilisema kuwa barabara zilizoko karibu na eneo hilo zilikuwa na ghasia kati ya wakristo na watu wasiojulikana
Aidha moto uilianzishwa katika jengo lililokuwa karibu na kanisa hilo lakini moto huo ukazimwa kwa wakati.
Pia inaarifiwa kuwa Rais Morsi alilaani ghasia
hizo kupitia kwa njia ya simu kwa papa Tawadros wa pili ambaye ndiye
kiongozi kwa kanisa la kikopti.
''Shambulizi lolote dhidi ya kanisa hilo ni kama
shambulizi dhidi yangu,'' alisema Papa Towadros ambaye pia aliwataka
watu kuwa watulivu.
0 maoni:
Chapisha Maoni