Borussia Dortmund imejikatia tiketi ya kuingia fainali ya
Klabu bingwa Ulaya 2012-13 baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-3 dhidi
ya Real Madrid. Real Madrid imeshinda 2-0 katika mechi ya nusu fainali ya pili katika Bernabeu Jumanne. Lakini
imeshindwa kusonga mbele kutokana na kipigo ilichopata cha magoli 4-1 Kutoka
kwa Borussia Dortmund walipokuwa nyumbani wiki iliyopita.
Upande wa timu hiyo ya Bundesliga ulinusurika kutolewa
katika kinyang’anyiro hicho. Na kama Rael Madrid wangefanikiwa kuongeza goli
moja wangekuwa pazuri zaidi kwakuwa na goli moja la ugenini. Lakini bahati
haikuwa upande wao na hivyo kupoteza nafasi hiyo na kutolewa
Hata hivyo, magoli kutoka Karim Benzema na Sergio Ramos
katika dakika 10 za mwisho ghafla ilianzisha
nguvu mpya, lakini Dortmund ikiwa juu kimagoli wameingia fainali ya kwanza tangu
mwaka 1997, wakati ilipofungwa Juventus 3-1.
Vijana wa Mourinho walijua ukubwa wa kazi waliyokuwa nayo,
na walianza mchezo kwa umakini wakiwa na kiu ya kufanya mapinduzi. Gonzalo
Higuain angeweza kufungua mchezo kwa bao mnamo dakika nne, lakini shuti
alilounganisha toka kwa Mesut Ozil liliishis mikononi mwa Weidenfeller Roman.
Lewandowski alikosa kutoka yadi nane, kabla ya Madrid
hatimaye alionyesha dalili ya uhai katika nusu ya pili.
Benzema akitokea benchi wakati zikiwa zimesalia dakika saba,
alionyesha uhai na kuipa timu yake nguvu ya kuusaka ushindi baada ya kuipatia
goli timu hiyo ya hispania.
Madrid ilipata jumla ya magoli 2 katika mechi hiyo ingawa
magoli hayo hayakutosha kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele kwenye hatua ya
fainali
Sasa swali kuu ni je Wembley zitacheza timu zote za
kijerumani ama Barcelona inaweza kufanya mabadiliko hapo kesho?
0 maoni:
Chapisha Maoni