California. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imechelewesha jaribio la kombora la masafa marefu lililotarajiwa kufanywa wiki hii katika jimbo la California, wakati kukiwa na ongezeko la mvutano wa nyuklia na Korea Kaskazini.
Ofisa mmoja wa Wizara alisema Waziri wa Ulinzi
Chuck Hagel alipanga upya siku ya kufanywa jaribio la kombora hilo kwa
jina Minuteman 3 litakalofanywa katika kambi ya jeshi la angani ya
Vandenberg mwezi ujao.
Alisema kutokana na wasiwasi kuwa uzinduzi huo
huenda ukachukuliwa na wengine kumaanisha kuwa Marekani inalenga
kuuchochea hata zaidi mzozo unaoendelea kwa sasa na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini, iliyoghadhabishwa na vikwazo vya
Umoja wa Mataifa na majaribio ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini,
ilitoa msururu wa vitisho vya kuanzisha vita vya nyuklia katika wiki
chache zilizopita.
Tangazo hilo la Pentagon limefuatia ripoti kuwa
Korea Kaskazini imeificha mizinga miwili ya masafa marefu ndani ya
handaki karibu na viwanda vyake vya pwani ya Mashariki.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imehamisha makombora baadhi kwenye mwambao wake wa Mashariki tayari kwa mashambulizi dhidi ya Marekani, huku nchi hiyo inayotishiwa kushambuliwa ikisema inachukua tahadhari kutokana na vitisho hivyo.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imehamisha makombora baadhi kwenye mwambao wake wa Mashariki tayari kwa mashambulizi dhidi ya Marekani, huku nchi hiyo inayotishiwa kushambuliwa ikisema inachukua tahadhari kutokana na vitisho hivyo.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Yonhap cha
Korea Kaskazini kilimnukuu ofisa mmoja wa Serikali nchini humo,
makombora mawili tayari yameshasafirishwa kwa treni na kuwekwa katika
magari tayari kwa kushambulia.
Kwa upande wake Wizara ya Ulinzi ambayo
ilithibitisha kupelekwa kwa kombora la kwanza ilikataa kutoa maoni yake
juu ya habari za hivi karibuni kwamba makombora mengine yamesafirishwa
Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni