Maofisa wa
Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine
za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la
makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako
walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.
Operesheni
ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha
(OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa
na silaha hizo.
Walifika
nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini walilazimika kusubiri hadi saa
9:10 walipomkamata Mbunge huyo baada ya yeye mwenyewe kujisalimisha.
Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni,
alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba “anaweza kuhatarisha amani”.
Mashuhuda
waliokuwa karibu na anakoishi Lema, eneo la Njiro Mwisho wa Lami,
walisema polisi hao walifika wakiwa kwenye magari manne na kwamba ili
kuchunguza ndani ya uzio wa nyumba yake, walipanda juu ya mabega ya
wenzao huku wakielekeza mitutu ya bunduki tayari kukabiliana na lolote
ambalo lingejitokeza.
Baada ya
kuchungulia baadhi yao walitumbukia ndani ya uzio na kwenda kusimama
mbele ya milango na madirisha ya nyumba ya Lema na huku nyuma wengine
walipanda tena kwenye mabega ya wenzao kuendelea kuweka ulinzi kwa
walioingia ndani.
Askari
hao wanadaiwa kwamba waliwataka walinzi wa nyumba hiyo iliyopo karibu
na Chuo cha Ufundi Veta, kuwafungulia mlango, lakini walinzi hao
walikataa hivyo kuzua mabishano makali.
Kutokana na
mabishano hayo, Lema aliyekuwa ndani amelala alishtuka na kuanza
kufuatilia na kubaini kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake hiyo. Mke wa
Lema, Neema alimpigia simu Katibu wa Wilaya wa Chadema, Aman Golugwa
kumwarifu kuhusu uwepo wa watu walioruka ukuta.
Golugwa jana
alithibitisha kupokea simu ya mke wa Lema na kwamba alipopata taarifa
hizo alimwarifu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa
Arusha, Camillius Wambura ambaye baadaye alimuahidi kwamba angefuatilia
suala hilo.
“Baadaye
alithibitisha kuwapo kwa polisi waliotumwa kwa ajili ya kumkamata Lema
lakini akasema amewapa maelekezo ya kufuata taratibu za kawaida,”alisema
Golugwa na kuongeza:“Baada ya hapo, wale askari waliokuwa wameruka
ukuta walitoka nje ya uzio”.
Habari
zinasema wakati baadhi ya askari wanaruka ukuta, wengine walibaki nje
wakizingira uzio wa nyumba ya Lema huku wakiwazuia viongozi wa Chadema
waliokuwa eneo hilo kusogea.
Kukamatwa
kwa Lema katika mtindo wa aina yake kumefanywa saa chache tangu alipotoa
kauli ya kukataa kujisalimisha polisi, kutokana na agizo la Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo. Mulongo aliagiza Lema akamatwe kwa
tuhuma kwamba alichochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Katika
vurugu hizo, wanafunzi hao walimzomea Mulongo na kurushia mawe msafara
wake wakati alipokwenda kusikiliza malalamiko yao yaliyotokana na kuuawa
kwa mwanafunzi mwenzao, Henry Kago (22) ambaye alichomwa kisu na watu
wasiofahamika wakati anatoka kujisomea saa 4:00 usiku.
“Kuna
taratibu za kumwita mbunge polisi, wanaweza kunipigia simu au
kuwasiliana na Spika, lakini siyo kutumia utaratibu huu wa kutangaza
kwenye vyombo vya habari kuwa mimi natakiwa kukamatwa wakati najua sina
kosa,”alisema Lema.
Kauli ya Lema
Akizungumza na Mwananchi kabla ya kujisalimisha kwa askari hao juzi usiku, Lema alisema alishangaa polisi kuvamia nyumba yake usiku wakati walikuwa na uwezo wa kumpigia simu na kumwita.
Akizungumza na Mwananchi kabla ya kujisalimisha kwa askari hao juzi usiku, Lema alisema alishangaa polisi kuvamia nyumba yake usiku wakati walikuwa na uwezo wa kumpigia simu na kumwita.
“Wapo nje ya
nyumba yangu, wanatishia kupiga mabomu kama nisipotoka nje, lakini
wanajadiliana na walinzi wangu na mimi nimewataka wanipe hati ya
kunikamata,” alisema Lema. Hata hivyo, baada ya muda idadi kubwa ya
wafuasi wa Chadema, walijitokeza na kuzingira nyumba ya Lema, hali
ambayo ilianza kutishia uvunjifu wa amani.
Golugwa
ndiye aliyefanya majadiliano na OCD Muroto kuhusu namna ya kufanikisha
mbunge huyo kujisamilisha baada ya kuwa amewasiliana na Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa na ilipotimu saa 9:10 usiku Lema
alijisamilisha baada ya kuhakikishiwa usalama wake.
Mmoja wa
viongozi wa Chadema, Calist Lazaro alisema walikubali Lema aende polisi,
baada ya majadiliano na viongozi wa juu ya chama hicho.
“Tulitaka
Polisi watuhakikishie usalama wake na pia tulitaka suala hili lifanyike
kwa uwazi kwani siyo jambo la kawaida mbunge kuvamiwa na polisi usiku
kama jambazi,”alisema Lazaro.
Polisi wanena
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas jana, alikiri maofisa wa jeshi hilo kumkamata mbunge huyo juzi usiku na hadi jana mchana alikuwa bado yupo rumande.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas jana, alikiri maofisa wa jeshi hilo kumkamata mbunge huyo juzi usiku na hadi jana mchana alikuwa bado yupo rumande.
“Ni kweli
tupo naye hapa polisi, anasubiri kuhojiwa kutokana na tuhuma za
uchochezi katika Chuo cha Uhasibu Arusha,”alisema Kamanda Sabas. Alisema
uamuzi wa kuendelea kumshikilia au kumwachia, utatolewa baada ya
kukamilika mahojiano.
Mapema
wakili wa Lema, Hamphrey Mtui akizungumza na Mwananchi nje ya kituo
kikuu cha polisi, alisema bado alikuwa hajaruhusiwa kuonana na mteja
wake .
“Bado
tunasubiri polisi wamtoe na wakati wa kuchukua maelezo yake ndiyo
wameniambia wataniita,” alisema Mtui. Baadaye Lema alihojiwa lakini
alikataliwa kupewa dhamana.
Taarifa za
kukamatwa kwa Lema zilianza kusambaa juzi saa sita kasorobo usiku na
ilipofika jana asubuhi tayari tukio hilo lilikuwa limeishateka mijadala
ya mitandao ya kijamii.
Mijadala hiyo iliambatana na mkanda wa Video wa Lema wakati akizungumza na wananfunzi wa IAA.
0 maoni:
Chapisha Maoni