Ombi hilo la Waziri Mkuu limekuja wakati kukiwa na vilio
vya ukosefu wa huduma bora za jamii huku maisha ya Watanzania
yakidorora.
Akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za
Serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na
Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2013/2014, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliomba
Bunge kuidhinisha jumla ya Sh123 bilioni (123, 401,059,000) kwa ajili ya
Mfuko wa Bunge na Sh4 trilioni nne, (4,226,123,954,802) kwa ajili ya
Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi ikiwa ni
matumizi ya kawaida na fedha za maendeleo za ndani na nje, ambapo kati
yake ameomba kiasi cha Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi.
Ombi hilo la Waziri Mkuu limekuja wakati kukiwa na
vilio vya ukosefu wa huduma bora za jamii kama afya, chakula, maji na
hali za maisha ya Watanzania zikiendelea kudorora.
Wakichangia mjadala wa bajeti hiyo baadhi ya
wabunge na wanasiasa wameguswa na kuhoji vigezo vilivyotumika kutenga
kiasi kikubwa hicho cha pesa kwa ajili ya mazishi ya watu walio hai
badala ya kutumia kiasi hicho cha pesa kurekebisha huduma bora za
wananchi ili kuwaondoa katika hatari za kupoteza maisha.
Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Lucy Owenya
ndiye aliyeibua hoja hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio na
matumizi ya ofisi hiyo iliyowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu Mizengo
Pinda aliposema inashangaza kutenga mabilioni kwa watu watakaokufa
badala ya kuwekeza fedha hizo kwa maendeleo ya walio hai.
Anasema Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni
ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma, Serikali inawajali
viongozi watakaokufa na kupuuza kufutatua matatizo ya akina mama
wajawazito wanaolala chini au wanne kitanda kimoja katika hospitali
nyingi nchini.
Owenya akaitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kupunguza
fedha hizo na kuzitumia kujenga chumba cha upasuaji cha hospitali ya
Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi pamoja na kuisaidia Hospitali Teule ya St
Joseph kununua vitanda vya wodi ya wazazi.
“Ni aibu na fedheha kubwa kutenga kiasi kikubwa
cha fedha kwa ajili ya maandalizi ya kuzika viongozi, huku mambo muhimu
na ambayo ni kipaumbele yakiachwa, hivi mmetenga kiasi hicho kwani
mnajua nani atakufa na lini atakufa ndiyo mnajiandaa kumzika, ni aibu
kutenga kiasi kikubwa hiki cha pesa kwa ajili ya watu watakaokufa na
ambao kwa sasa wapo hai…Kwa nini pesa hii isitumike kwa maendeleo ya
watu waliohai,” anahoji Owenya.
Mbunge huyo akaongeza kusema Serikali imeshindwa
kufikiri hasa namna ya kuwaondolea umaskini na taabu wanazopata wananchi
wake lakini inathibutu kutenga kiasi kukubwa cha fedha kwa ajili ya
kuwazika viongozi ambao bado wapo hai.
Mbunge mwingine aliyeonyesha kukerwa na bajeti
hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu ni Kangi Lugola wa Jimbo la Mwibara (CCM)
anayesema licha ya kuwa mbunge wa CCM haungi mkono bajeti ya makadirio
ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kile aliochosema
kitendo cha kutengea Sh1 bilioni kwa ajili ya mazishi ya viongozi
watakaokufa ni ubadhirifu.
Lugola ameongeza kuwa hataunga mkono bajeti hiyo kwa sababu hajui atakufa lini.
“Mazishi gani ya viongozi kwa shilingi bilioni moja? Huu ni wizi mtupu ndani ya Serikali, kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo? Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” anasema.
“Mazishi gani ya viongozi kwa shilingi bilioni moja? Huu ni wizi mtupu ndani ya Serikali, kama wasipokufa tutapata ripoti ya matumizi mengine ya fedha hizo? Siungi mkono hoja mpaka nione bajeti inaeleza mikakati na dhamira ya dhati ya kumaliza rushwa na dawa za kulevya nchini,” anasema.
Mbali na wabunge hao, wanasiasa wengine
wamezungumzia bajeti hiyo ya Waziri Mkuu na kusema Serikali inapaswa
kuwa makini na matumizi ya pesa za wananchi na kuzitumia kwa manufaa ya
maendeleo yao na siyo ya kundi dogo la viongozi.
0 maoni:
Chapisha Maoni