Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa
jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba
0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa
mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka
mimi.”
Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”
Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe
huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza.
Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo
kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu
ningemkamata.”
Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo
kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka
kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13
waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”
kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

Alisema Mbunge huyo, anajua kazi ambayo, ilifanya
chuo cha uhasibu na ndiyo sababu anajificha... “Alifanya kazi yake
nikazomewa, kama ningetaka kutumia madaraka yangu asingekuwa salama …
nadhani Lema anahitaji kusaidiwa ili abadilike.”
Kuhusu madai ya kujificha, Lema alisema
haitajisalimisha polisi licha ya Mulongo kuagiza akamatwe kwa kuwa kuna
taratibu za kufuatwa polisi inapomhitaji mbunge ambaye amechaguliwa na
watu.
Alisema kama polisi wanamuhitaji, wanapaswa kumuita na pia kuwasiliana na Ofisi ya Spika wa Bunge.
Alisema kama polisi wanamuhitaji, wanapaswa kumuita na pia kuwasiliana na Ofisi ya Spika wa Bunge.
“Naomba ieleweke kuwa mimi sijawakimbia polisi,
siogopi kesi na wala siogopi jela nitaendelea na shughuli zangu waje
kunikamata barabarani,” alisema Lema.
Akizungumzia tukio la juzi, Lema alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu kwa kukosa weledi wa kuzungumza na wanafunzi wenye majonzi.
Akizungumzia tukio la juzi, Lema alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu kwa kukosa weledi wa kuzungumza na wanafunzi wenye majonzi.
Alisema alikwenda chuoni hapo baada ya kuitwa na
wanafunzi na kabla ya kuzungumza, alikutana na uongozi wa chuo, akiwamo
Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha.
“OCD Arusha aulizwe kazi ambayo nilifanya kutuliza
hasira za wanafunzi na tutasambaza DVD zaidi ya 3,000 kwa wakazi wa
Arusha kujionea tukio hili ambalo sasa limebadilishwa na kuwa la
kisiasa,” alisema Lema.
Mwanafunzi, Henry Kago(22) aliyeuawa kwa kuchomwa
kisu na watu wasiojulikana na kusababisha wanafunzi kucharuka chuoni
hapo anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Iringa kwa mazishi.
0 maoni:
Chapisha Maoni