Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia bao la kwanza
Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wamejiweka
katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu
bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Barcelona 4-0 katika mchezo wa
kwanzawa nusu fainali nchini Ujerumani.
Mabao mawili ya Thomas Müller, na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliizamisha Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa,akiwemo Messi ambaye alikosa michezo kadhaa kabla ya kuanzishwa hii leo.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kufungwa mabao 4-0 tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kyiv ya Urusi mwaka 1997 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
Habari zaidi zinakujia hivi punde
0 maoni:
Chapisha Maoni