Ikungi. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni
ya uzinduzi wa nafasi ya udiwani Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja, Wilaya
ya Ikungi, Tundu Lissu, juzi alishindwa kuuza sera za Chadema, na badala
yake alitumia muda mwingi kuhimiza ‘sera ya kuwakataza’ wananchi
kuchangia maendeleo yao .
Tundu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Singida
Mashariki kupitia chama hicho, alipanda jukwaani huku akiwa amebeba
makabrasha ya michanganuo ya Bajeti ya Serikali ya kuanzia mwaka wa
fedha wa 2010/11 hadi 2013/14.
“Mimi leo sitaki kabisa kuzungumzia habari za
Amosi Mghenyi ambaye ametusaliti kwa kuhama Chadema na kurejea CCM.
Amosi kisiasa ni mfu, kwa hiyo siwezi kupoteza muda wangu kuzungumiza
mambo ya mfu”,alisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi
waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha iseke.
Alisema ufunguzi wake utajikita zaidi katika
kuwaelimisha wananchi wa Kata ya Iseke kwamba Serikali inazo fedha
nyingi na za kutosha kugharamia maendeleo ya wananchi.
Akijenga hoja yake hiyo, alisema kwa mfano katika
mwaka wa fedha wa mwaka 2010/11, Mkoa wa Singida, ulipewa zaidi ya Sh903
milioni za undeshaji wa shule, lakini zilizotumika ni Sh464 milioni na
kubaki Sh438.2.
Alisema fedha hizo zaidi ya Sh438.2 milioni
zilizobaki, hazijaainishwa zilipelekwa wapi. “Kwa vyo vyote zitakuwa
zimeishia kwenye matumbo ya mgambo na watendaji wa Serikali ya CCM”.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma, aliwataka wakazi wa Kata ya Iseke, kumchagua Emmnuel Jackson Jingu awe diwani wao.
ili waondokane na manyanyaso ya michango kama walivyojikomboa wakazi wa Jimbo la Singida Mashariki.
Wagombea wengine wa nafasi ya udiwani Kata ya
Iseke, ni Amosi Munghenyi wa CCM na Abdallah Kinyenje maarufu kwa jina
la Petro wa CUF.
0 maoni:
Chapisha Maoni