Jumanne, 28 Mei 2013

Dk. Mwakyembe aundiwa zengwe bandarini


MAKUNDI mawili yenye nguvu kifedha na madaraka katika mamlaka za Serikali yanapanga njama ili kukwamisha jitihada za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Makundi hayo yametajwa kutoka Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kwa pamoja wanadaiwa kuunganisha nguvu ili kupunguza kasi ya kuwafukuza watumishi wa bandari inayolenga kuziba mianya ya rushwa.
Baadhi ya watumishi TPA waliliambia MTANZANIA kuwa mkakati huo ulianza baada ya Dk. Mwakyembe kufanya operesheni ya kuwatimua baadhi ya watumishi wa bandari.

Walisema Dk. Mwakyembe amekuwa akifanya maamuzi mazito, ikiwemo kufukuza watumishi wa bandari na kuwasimamisha wengine.

“Si kazi rahisi kupata kazi bandari ukizingatia hali yenyewe ilivyo ya kupata ajira, kwanza unapata kazi kwa kuhonga hata kama una sifa zinazostahili,” walisema.

Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, alisema Dk. Mwakyembe aliwahi kuagiza kurudishwa haraka scanner ya kupimia mizigo iliyoondolewa Bandari ya Dar es Salaam na kupelekwa Bandari ya Tanga, lakini hadi sasa haijarudishwa.

Alisema scanner hiyo ilipelekwa kwa kificho zaidi ya miaka mitatu iliyopita na haijawahi kufanya kazi yoyote huko mkoani Tanga.

Msemaji wa TPA, Janet Ruzangi alikiri scanner hiyo kupelekwa Tanga chini ya usimamizi wa TRA.

Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya hakupatikana kuzungumzia suala hilo, baada ya wasaidizi wake kutaka aandikiwe maswali.

Hata hivyo, licha ya maswali hayo kuandikwa, ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna majibu yaliyo

Source: Gazeti la Mtanzania

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More