Ijumaa, 17 Mei 2013

Wapiganaji Boko Haram wauawa Nigeria

 

Takriban wapiganaji 30, wa waasi nchini Nigeria, wameuawa kwenye mashambulio ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali, Kaskazini Mashariki mwa nchini hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, amesema, ndege za kivita na helicopta zilitumika kushambulia kambi kadhaa wa waasi hao.
Aidha ameiambia BBC kuwa ndege moja ilishambuliwa kwa kombora na waasi hao lakini ilifanikiwa kurejea salama hadi kambi yao.
Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki, yanayoshuhudia mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Kwa sasa jeshi la Nigeria, linajaribu kutwaa uthibiti wa majimbo ya Adamawa, Yobe na Borno kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Wakati huo huo, milipuko na milio ya risasi imesikika usiku kucka katika jimbo la Katsina.
Raia wameiambia BBC kuwa mabenki, vituo vya polisi na magerza yaliharibiwa kufuatia mapigano makali mjini Daura karibu na mpaka wa nchi hiyo na Niger.
Wanasema wameona miili ya wanajeshi watano na mitatu ya wapiganaji wa waasi lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa.
Mawasiliano ya simu ya mkononi yamekatizwa katika maeneo mengi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Lakini afisa mmoja wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mitandao ya simu ilifungwa wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More