Ijumaa, 10 Mei 2013

Jenerali wa Uganda amshutumu Museveni kutaka kumwachia madaraka mwanae.

 
Jenerali mmoja wa jeshi anamshutumu rais Yoweri Museveni  wa Uganda kwa kujaribu kuhakikisha mwanae anarithi madaraka kama kiongozi wa nchi hiyo, akiwa ni kiongozi wa kwanza wa juu kuelezea  wasi wasi wake juu ya mpango wa mrithi wa madaraka wa rais Museveni baada kuwepo madarakani kwa  karibu miongo mitatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP , David Sejusa mmoja wa majenerali 6 wa Uganda alisema katika barua yake ya hivi karibuni kwa mkuu wa usalama wa taifa kwamba anataka uchunguzi ufanyike  juu ya shutuma kwamba wale watakaompinga mtoto wa museveni kuwa kiongozi ajaye wanaweza kulengwa kuuwawa.

Jenerali Nyaronda  Nyaikirima kamanda wa juu wa jeshi alisema Jumanne kwamba jeshi limedahalilishwa na barua ya Sejusa.

Shutuma hizo na afisa wa juu wa jeshi zimewashtua wengi huko Uganda.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More