Twende
taratibu, hii ni taarifa ya kisayansi na sio ‘kiimani’ na imetolewa na
daktari bingwa wa moyo wa Marekani. Sasa naomba uniruhusu nikuelezee
nilichokutana nacho kuhusiana na habari hii.
Dr
Sam Parnia wa Marekani amedai kwamba kwa kupitia mbinu za kisasa za
kitaalamu (kisayansi) kuna uwezekano wa kumrudishia uhai mgonjwa
aliyekata roho ndani ya saa 24!! (hata mimi nimeguna)
Dr
huyo wa moyo ambaye amepata mafunzo yake nchini Uingereza, ameendelea
kusema hivi karibuni wanategemea kuanza kuokoa maisha ya wagonjwa
wanaokuwa tayari wamekata roho katika masaa ya mwanzo baada ya
kuthibitisha wamefariki. “We may soon be rescuing people from death’s
clutches hours, or even longer, after they have actually died.” Alisema
Dr Sam
Parnia
ameendelea kutetea kauli hiyo kwa kusema kuwa muigizaji wa Marekani
James Gandolfini aliyefariki mwezi uliopita angeweza kupona endapo
angekuwa ameugulia tatizo lake la moyo New York.
“I
believe if he died here, he could still be alive. We’d cool him down,
pump oxygen to the tissues, which prevents them from dying, Clinically
dead, he could then be cared for by the cardiologist. He would make an
angiogram, find the clot, take it out, put in a stent and we would
restart the heart,” Dr Parnia alilieleza jarida la Der Spiegel la Ujerumani.
Dr
Parnia ambaye ni mkuu wa kitengo cha ‘Intensive care’ katika hospitali
ya the Stony Brook University iliyoko New York, Marekani aliendelea
kusema ni kweli hawawezi kuokoa maisha ya kila mtu sababu wagonjwa wengi
wa moyo huwa na matatizo mengine ya ziada na makubwa zaidi.
Aliendelea
kusema kama teknolojia ya kisasa ya tiba na mafunzo vingekuwa
vinafanyiwa kazi inavyotakiwa, (kitu ambacho anadai bado hakijafanyika)
basi watu ambao wangetakiwa kufa ni wale tu wenye matatizo ambayo
hayatibiki kabisa lakini sio ugonjwa wa moyo unaotibika.
’‘A
heart attack is treatable. Blood loss as well. A terminal cancer isn’t,
neither are many infections with multiresistant pathogens. In these
cases, even if we’d restart the heart, it would stop again and again”.
Akielezea
jinsi ambavyo mgonjwa wa moyo aliyefariki anavyoweza kurudishiwa uhai,
alisema kwanza ni kuugandisha mwili mara tu baada ya kuthibitishwa
amefariki , “freezing the body immediately after death – but cooling
it down to best preserve brain cells while keeping up the level of
oxygen in the blood. This buys time to fix the underlying problem and
restart the heart”. Alisema
Dr
huyo alisema kuna uwezekano katika miaka 20 ijayo madaktari watakuwa na
uwezo wa kurudisha uhai wa wagonjwa masaa 12 hadi 24 toka wathibitishwe
kufa na kuiita hiyo kuwa ni sayansi ya ufufuaji, “You could call that resurrection, if you will. But I still call it resuscitation science”.
Dr Parnia ameandika kitabu kipya kiitwacho ‘Erasing Death’.
SOURCE: DAILY MAIL
Posted in:
1 maoni:
it will be a very very great suceessfull under the sun and helpful. may God enable this science to happen
Chapisha Maoni