Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Jumatatu, 24 Juni 2013

Brazil yazidi kusonga mbele Kombe la Mabara


Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli (kushoto) akizuiwa na beki wa Brazil, David Luiz wakati wa mechi ya Mabara kwenye Uwanja wa Fonte Nova mjini Salvador. Picha AFP.  

Brazil. Timu ya taifa ya Brazil juzi imeichapa Italia 4-2 katika mashindano ya Kombe la Mabara na hivyo Brazil kumaliza hatua ya makundi ikiongoza kundi A.
Mshambuliaji Neymar wa Brazil katika mechi hiyo alifunga bao na hivyo kufikisha mabao matatu katika mashindano hayo.
Brazil ilipata bao la kwanza mwishoni mwa kipindi cha kwanza ambalo lilifungwa na Dante, lakini Italia ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 51 mfungaji akiwa Emanuele Giaccherini.
Katika dakika ya 55, Neymar aliifungia Brazil bao la pili baada ya kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja nyavuni na kumuacha kipa mahiri wa Italia, Gianluigi Buffon asijue la kufanya.
kama hiyo haitoshi Brazil ilipata bao la tatu katika dakika ya 66 ambalo lilifungwa na Fred, lakini Italia nao hawakubaki nyuma kwani katika dakika 71 walifunga bao la pili ambalo lilifungwa na Giorgio Chiellini.
Katika dakika ya 80 bado kidogo Italia wangesawazisha hata hivyo mpira wa kichwa uliopigwa na Christian Maggio ulipita juu kidogo ya goli. Pia dakika chache baadaye Mario Balotelli naye alipiga shuti kali, lakini lilitoka nje.
Ilipofika dakika ya 89, Brazil ilijihakikishia ushindi wa mechi hiyo kwani Fred alitumia vizuri mpira uliopanguliwa na kipa wa Italia na hivyo kuiandikia Brazil bao la nne.
Brazil imemamaliza hatua hii ya makundi ikiwa na pointi tisa ikiwa na pointi tatu juu ya Italia inayomfuatia huku timu za Mexico na Japan zikitolewa mashindanoni.
“Brazil ipo tayari kwa ajili ya mechi ya nusu fainali, tumefanikiwa kusonga mbele kwa sababu ya ufundi mzuri na mbinu bora, pia kikosi kinajiamini,”alisema kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari.

Jumapili, 23 Juni 2013

Vigogo wahaha - wahojiwa mabilioni ya Uswis

Dar es Salaam. Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Jaji Werema alipoulizwa na Mwananchi Jumpili maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.
“Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.
“Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.”
Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa.
Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.
Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini.
Werema anaripotiwa akiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta.
Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.
Werema alisema wanaendelea na uchunguzi kuwabaini zaidi ya Watanzania 200, waliotajwa kuficha mabilioni ya fedha nje ya nchi.
Mbali na Werema, tume hiyo inaundwa na viongozi kadhaa wa taasisi nyeti kama vile Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
Tume hiyo inawahusisha pia Mkuu wa Sheria wa BoT, Mustapha Ismail na maofisa kutoka idara ya upelelezi na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa jarida hilo la kimataifa, miongoni mwa watuhumiwa hao ni wanasiasa na majenerali wastaafu wanaotuhumiwa kutorosha zaidi ya Dola 133 milioni mwaka 2005, kupitia Mfuko wa Ulipaji Madeni ya Nje (EPA)
Baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika wamehojiwa kutokana na taaluma zao, familia zao, akaunti zao za benki zilizoko nchini na nje ya nchi pamoja na nchi walizotembelea mara kwa mara kwa miaka mitatu iliyopita.
Lengo la kuwahoji inaelezwa ni kutaka kujua iwapo walifuata njia zinazotakiwa katika kufungua akaunti hizo nje ya nchi na iwapo fedha zilizohifadhiwa huko zilipatikana kihalali.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa Bungeni kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe mwishoni mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Bunge liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo bungeni.

Jumanne, 18 Juni 2013

Tizama matukio mbali mbali ya chama cha CHADEMA wakiwafariji wafiwa na majeruhi baada ya Mlipuko wa Bomu


Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.




Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani yatanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tanki hilo lilishambuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii ya matangazo lina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.



Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bwana Benny akiwa hospitali


James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani.

Jumatano, 12 Juni 2013

TFDA: Kiwanda cha TPI kilisambaza ARV feki kwa Watanzania


MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA), imethibitisha dawa bandia za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARV), zilitengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industry (TPI). Taarifa hiyo, ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hiiti Sillo, wakati wa semina kwa wabunge iliyoandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD).

Sillo, alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), aliyetaka kujua kama dawa hizo bandia za ARV kweli zilitengenezwa na kiwanda cha TPI.

“Ninyi TFDA, mlikuwa wapi hadi kiwanda hicho kinazalisha dawa bandia za ARV?” alihoji Machali.

Alisema ni kweli dawa hizo bandia, ziligundulika zikiwa tarari zipo sokoni katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Tarime mkoani Mara.

“TDFA ilifanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini dawa hizo ni bandia na baada ya uchunguzi pia na kwa mujibu wa nyaraka, ilibainika dawa hizo zilitengenezwa na Kiwanda cha TPI ambayo ndiyo iliyoisambazia dawa hizo MSD,” alisema Sillo.

Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), aliitaka Serikali kupeleka muswada bungeni kutunga sheria kali kwa watakaobainika kuuza dawa za Serikali katika maduka binafsi.

“Sheria hii kali ikitungwa, dawa za Serikali hazitakutwa kwenye maduka binafsi na zikikutwa zitaifishwe,” alisema.

Awali akifungua semina hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alisema lengo la semina hiyo ni kushirikishana uzoefu na wabunge juu ya mfumo wa usambazaji dawa nchini.

Alisema semina hiyo, ilikuwa na mada nne, ikiwemo hiyo ya mfumo wa usambazaji wa dawa na vifaa tiba wa Bohari ya Dawa, ikiwemo kuzungumzia mikakati mbalimbali ya kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani, alisema mbali na jitihada mbalimbali zinazofanywa na bohari hiyo, aliwaomba wateja wake kuboresha mfumo wa utunzaji kumbukumbuku katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika ngazi zote.

“Kuongeza usimamizi wa dawa na vifaa tiba ngazi ya wilaya, kupitia Kamati za Afya za Wilaya ili kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vituoni,” alisema.

Messi na babake wadaiwa kulaghai serikali


Mshambulizi matata wa Barcelona Lionel Messi na babake wanachunguzwa nchini Uhispania kwa kuilaghai serikali ya nchi hiyo zaidi ya pauni milioni tatu nukta nne.
Mchezaji huyo kutoka Argentina na babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa kujaza fomu zizizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na 2009.
Hata hivyo mechezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na mitano hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
Messi hulipwa Euro milioni kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi duniani.
Lakini mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za mahakama nyumbani kwake kwa mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini Barcelona.
Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.
Messi na babake wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ngambo, mjini Belize na Uruguay kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Uhispania, ambako anaishi na kucheza soka ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa pauni milioni tatu na nusu.

CHANZO: bbc.co.uk/swahili

Alhamisi, 6 Juni 2013

MTOTO WA MICHAEL JACKSON ATAKA KUJIUA





Imeripotiwa kuwa mtoto wa marehemu Michael jackson,Paris Jackson  amekimbizwa hospitalin
baada ya kufanya jaribio la kujiuwa. Jackson Paris  mwenye umri wa miaka 15 sasa,alikimbizwa hospitali mapema Jumatano asubuhi na vyanzo kutuambia ilikuwa jaribio kujiua.Ripoti inasema kuwa alijiovadozi kwa dawa ambazo bado hazijafahamika Ndugu wa karibu na Paris jackson  wameuambia mtandao wa TMZ toka America kuwa hiyo yawezakuwa si jaribio la kwanza  kwani ana alama za  kujichanja kwa kifaa chenye ncha kali kwenye mkono wake.Siku moja kabla ya tukio hilo,Paris jackson alitweet maneno yafuatayo yenye mafumbo: “I wonder why tears are salty?” … na “yesterday, all my troubles seemed so far away now  it looks as though they’re here to stay.”





BREAKING NEWS: MUME WA KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA



                              Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe Jaffari Ally enzi za uhai wake


Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Jumanne, 4 Juni 2013

KIBANDA AREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI, KWA KISHINDO


                                  Kibanda akiongea na waandishi wa habari alipowasili air port

                                       Hapa akilia kwa uchungu baada ya kuwasili airport


BAADA ya kuwa Afrika Kusini  majuma kadhaa kwa ajili ya matibabu, Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya New Habari 2006 na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, hatimaye  amerejea nyumbani leo mchana na  kulakiwa na mamia ya waandishi wa habari.

Tizama picha zinazoonyesha kuwasili kwa mwili wa Albert Mangwea


Wasanii,waandaji,mashabiki na wadau wa muziki wa kizazi kipya Tanzania wameungana kupokea mwili wa marehemu Albert Mangwear pale Air Port Mchana wa leo.Albrt Mangweha "Ngwair" alifariki Jumanne iliyopita 28/5/2013 huko Afrika Kusini
 

Mwili wa marehemu Albert Mangweha a.k.a Ngawair ukiwa unapakiwa kupelekwa Airport kwa ajili ya kuletwa Tanzania.…

Jumatatu, 3 Juni 2013

Maandamano yakutaka kumngoa JK yanaandaliwa


MAANDAMANO makubwa ya kutaka Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio cha wakazi wa Mtwara na Lindi wanaopinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam yanaandaliwa.
Baadhi ya wakazi wa Lindi na Mtwara kwa kushirikiana na Chama cha Wananchi (CUF), Juni 29 mwaka huu wanatarajia kufanya maandamano hayo kutoka makao makuu ya CUF Buguruni hadi Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Maandamano hayo pia yatakuwa na lengo la kumtaka Rais Kikwete awang’oe madarakani mawaziri watatu ambao ni Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Emanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani).
Wakizungumza katika mkutano wa kongamano la gesi lililowakutanisha wakazi wa Lindi na Mtwara, lililofanyika jana jijini Dar es salaam katika Ofisi za Makao Makuu ya CUF, baadhi ya wakazi hao walisema wamechoshwa na ahadi za serikali.
Walisema wanaamua kufanya maandamano kwenda Ikulu ili kilio chao kimfikie Rais Kikwete ambaye kama hatakisikiliza asitarajie wananchi watarudi nyuma kutetea rasilimali zilizoko mikoani mwao.
Walibainisha kuwa vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara ni ishara ya kuchoshwa na mgawanyo wa rasilimali unaofanywa na serikali ambayo hivi sasa badala ya kuufikiria mkoa wa Mtwara unahangaika kujenga bomba la gesi kutoka mkoani humo.
Lipumba aanza
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni mkoani Mtwara zimesababishwa na serikali ya CCM iliyopuuza kilio cha umaskini cha wakazi cha mkoa huo.
Alisema serikali imeanza kushtuka na kwenda kuweka msingi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji baada ya machafuko na upinzani kutoka kwa wananchi.
Alibainisha kuwa nguvu na kuwaziba midomo wanasiasa, wananchi na wanaharakati kamwe hazitoisaidia serikali kutatua mzozo huo unaoonekana kuutikisa utawala wa Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa watu wa Mtwara na Lindi wamekosa mahali na fursa za kuonana na viongozi wao kuzungumzia suala la gesi na matokeo yake imesababisha vurugu, manyanyaso kutoka kwa polisi waliokwenda kutuliza ghasia.
Profesa Lipumba alisema serikali inaeneza propaganda za uongo kwamba wananchi wa Mtwara hawataki Watanzania wengine wafaidi rasilimali zinazotoka katika mkoa huo.
Alisema wananchi wanataka maendeleo yaanzie katika mkoa huo kutokana na rasilimali zilizopo ndani yake ikiwemo kujengwa kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kufua umeme wa MW 300 kama ahadi ya serikali ya mwaka 2011 inavyoeleza.
Aliongeza kuwa serikali katika ahadi zake miaka miwili iliyopita iliwaeleza wananchi wa Mtwara kwamba ingejenga kiwanda cha mbolea na kujenga kiwanda cha kufua gesi ambayo ingezalisha umeme wa MW 300 kisha uunganishwe kwenye gridi ya taifa lakini mipango hiyo haikufanyika.
Alisisitiza kwamba endapo mipango ya serikali iliyoainishwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ingetekelezwa hakuna vurugu wala matatizo ambayo yangejitokeza.
Alisema wananchi wanaoishi mikoa ya kusini wanadharaulika na kuonekana hawastahili kupata haki kama watu wa mikoa mingine na kwamba hali hiyo imewafanya wachoke na kufanya matendo ambayo yataaonyesha kuchoshwa na kuhitaji mabadiliko.
Wakazi wafunguka
Baada ya Lipumba kuzungumza, wakazi waliokuwapo ukumbini hapo walipata fursa ya kutoa dukuduku ambapo wengi wao walitaka mawaziri watatu wang’olewe madarakani.
Waziri Nchimbi anatakiwa kung’olewa kwa sababu ya kutowachukulia hatua polisi waliokwenda kutuliza ghasia mkoani humo kuendesha vitendo vya kihalifu, kubaka na kuwanyanyasa wananchi.
Mmoja wa wakazi hao alisema Nchimbi alisema damu ya polisi iliyomwagika haitapotea bure wakati askari hao walikufa kwenye ajali wakiwa njiani kwenda Mtwara.
“Polisi hawakufa kwenye mapambano, walikufa kwa ajali ya gari lao sasa wananchi watalipa vipi vifo hivyo? Waziri Nchimbi alichemka na hatufai,” alisema mkazi huyo.
Pia wananchi hao walimtaka Waziri Shamsi Vuai Nahodha aondolewe madarakani kwa kushindwa kuulinda mkoa huo pamoja na kutowawajibisha wanajeshi waliokiuka maadili ya kazi zao wakati wakilinda usalama mara baada ya kutokea kwa vurugu.
Mwananchi mwingine alitaka Waziri Muhongo aondolewe kwa kuwa ameshindwa kusimamia suala hilo la gesi lililo chini ya wizara yake na hivyo kusababisa vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Jumapili, 2 Juni 2013

Anna Kilango na Sophia Simba nusura Wachapane Hadharani


UHASAMA wa kisiasa kati ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, umevuka mipaka na sasa ni uadui wa wazi wazi. Hali hiyo ilidhihirika wiki iliyopita mjini Dodoma, wakati wawili hao walipokutana katika Benki ya CRDB iliyopo bungeni na badala ya kusalimiana, waliishia kutofautiana.
Shuhuda wa tukio hilo, aliiambia MTANZANIA, kuwa tukio hilo lilitokea saa 6 mchana, baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha Bunge kutokana na vurugu zilizosababishwa na wabunge wa upinzani, wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Shuhuda huyo alisema kuwa, kabla ya tukio hilo, Anne Kilango pamoja na wabunge wengine wa CCM, walikuwa ndani ya benki hiyo wakibadilishana mawazo.

Wakati wakiendelea kuzungumza, Sophia Simba aliingia ndani na kuanza kuwasalimia kila mmoja kama ilivyo kawaida.

“Sisi tulikuwa hapa ndani ya benki pamoja na Diana Chilolo (Mbunge wa Viti Maalum CCM), Turky, Mbunge wa Mpendae (Salim Abdallah Turky) pamoja na wahudumu wa benki.

“Sofia Simba alipofika, alitusalimia lakini Anne Kilango hakuitikia salamu yake na hapo Sofia akasema, mheshimiwa Anne Kilango nakusalimia.

“Aliposema hivyo tu, Anne Kilango akahamaki na kusema usinisalimie, mimi sitaki salamu yako. Kauli hiyo ilionekana kutushangaza na wakati tunashangaa, Sofia Simba akasema, mheshimiwa Anne Kilango mimi ni shoga yako na tumetoka mbali, kwa nini tusisalimiane?

“Aliposema hivyo, Anne Kilango akasema sitaki kusikia salamu yako, ‘shut up’ kisha akaondoka,” alisema shuhuda huyo akinukuu maneno ya Anne Kilango.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Simba alisema kwa kifupi, kwamba, “nina ngozi ngumu, sizungumzi mambo haya kwa sababu mimi ni kiongozi,” alisema na kukata simu.

Naye, Anne Kilango alipoulizwa naye alisema yeye hawezi kuzungumzia masuala hayo, kisha akakata simu.

Mgeja ataka Sitta afukuzwe CCM kwa usaliti


SIKU chache baada ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kutangaza timu inayoundwa na kundi lake kuwania urais 2015, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema chama hicho kinatakiwa kumchukulia hatua za kinidhamu kwa sababu anahatarisha uhai wa chama.

Alisema, kama chama kitamuacha aendelee kutoa kauli zinazohatarisha uhai wa chama, CCM itajiweka katika mazingira mabaya kisiasa pindi wapinzani watakapoanza kuchambua kauli hizo.

Kauli hiyo ya Mgeja, aliyoitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari, imekuja ikiwa ni siku chache tu tangu Sitta aitaje timu inayoundwa na kundi lake kuwania ukuu wa dola mwaka 2015.

Alisema wanaounda timu hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, ambaye hata hivyo amekana kuwamo kwenye timu hiyo.

Jana akimzungumzia Sitta, Mwenyekiti huyo wa CCM, Mgeja alimshushia tuhuma nyingi akimwita mkorofi, mlalamishi na kwamba anaonekana wazi kukihujumu chama.

Mgeja pamoja na mambo mengine, alimshutumu Sitta kuwa alianzisha CCJ akiwa ndani ya CCM, kisha akataka kuhamia Chadema akiwa ndani ya CCM na yote hayo chama kiliyajua na kumwacha.

Alisema Sitta yeye ni waziri, lakini kuna wakati alikaririwa akisema kwamba, Serikali iwaombe radhi wananchi kwa sababu ya mgawo wa umeme, baadaye akasema maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezekani na sasa amekaririwa hivi karibuni akisema Rais Kikwete alimhujumu kwenye uspika.

“Yaani anajiamini kiasi cha kuanza kumchokonoa hata Rais Kikwete, wakati akijua kwamba mambo anayoyafanya yanakwenda kinyume na mtazamo wa chama.

“Hivi huyu ni mtu gani asiyetosheka, kila wakati analalamika wakati yeye ni waziri na ana nafasi kubwa ya kupeleka malalamiko yake kwenye chama ili yakafanyiwe kazi.”

Alisema kama Sitta anaona yuko kwenye basi lenye abiria asioendana basi aondoke na kuhoji anafanya nini ndani ya CCM wakati anaonekana wazi kwamba haridhishwi na mwenendo wa chama na Serikali.

Mgeja pia alimtaka Sitta kwenda TAKUKURU kama anaona kuna rushwa ndani ya chama, au kama kuna wezi aende polisi na kama anaona kuna wahalifu, basi aende mahakamani.

“Lakini huyu mzee lazima chama kimchukulie hatua, huyu ni mzigo, kama hatadhibitiwa atakiharibu chama kwa sababu anaonekana ana ajenda ya siri,” alisema.

Mgeja aliitaka Kamati ya Maadili ya chama inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula, imjadili ili ijulikane ana ajenda gani.

Alisema kwa upande wake katika kikao cha NEC kijacho, atawasilisha hoja binafsi kutaka Sitta ajadiliwe.

“Yeye anajifanya ni msafi wakati mambo yake mengi tunayo, kwani hata alipopata uspika anaouota hadi sasa, alibebwa, tena kwa kampeni kali kweli kweli. Hivi, kwa nini asiwe kama mzee Msekwa (Pius Msekwa) ambaye baada ya kushindwa uspika alinyamaza kimya?” alifoka Mgeja.

Kwa mujibu wa Mgeja, kitendo kinachofanywa na Sitta ni cha hatari kwa uhai wa chama na kwamba kama isingekuwa huruma ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete, angeshafukuzwa uanachama wa CCM.

“Kuna wakati tulikaa tukataka kumnyang’anya kadi na aliokolewa na Mwenyekiti wetu, lakini pamoja na kusamehewa, bado hatulii, anaendeleza mambo yake ya ajabu ajabu,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Sitta ya wiki hii aliyoitoa akiwataja Magufuli, Membe na Dk. Mwakyembe kwamba ni wasafi, alisema ni ya kibaguzi, kwa kuwa waliotajwa ni Wakristo, wala hakuna Muislamu hata mmoja.

“Aliowataja wote hao akiwa kanisani ni wakristo, wala hakuna Muislamu, wote hao ni wanaume na hakuna mwanamke, pia hao wote ni kutoka Tanzania Bara na inavyoonekana Unguja na Pemba hakuna watu safi.

“Sasa mtu kama anadiriki kusema uongo, tena madhabahuni, ana sifa gani ya kuwa kiongozi, yaani amefika mahali sasa anaanza ubaguzi wa Watanzania Bara na Visiwani, anaanza kubagua jinsia, huyu hafai na lazima achukuliwe hatua.

“Namtaka anyamaze, asiendelee na mambo yake kwa sababu kama ataendelea kupiga porojo, nitasema mengi zaidi yanayomhusu kwa sababu siyo msafi kama anavyotaka kuwadanganya Watanzania,” alisema.

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More