Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Ijumaa, 30 Agosti 2013

MWANAJESHI WA UN AUAWA NCHINI DRC

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mwanajeshi wake mmoja wa kutunza amani ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mapigano makali kati ya na wapiganaji wa waasi Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Farhan Haq, hata hivyo hajatangaza uraia wa wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa.
Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa walitumia ndege za helicopta kuwasukuma nyuma wapiganaji wa M23 karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi katika eneo hilo la Mashariki.
Watu themanini waliuawa kwenye mapigano hayo wiki iliyopita.
Mwaka wa 2012, waasi wa M23 waliuteka mji huo kwa muda kabla ya kuondoka kufuatia shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Umoja wa Mataifa Umetuma kikosi maalum katika eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa madini kukabiliana na waasi hao.
Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, wanapambana na wapiganaji hao wa waasi kwa ushirikiano na wanajeshi wa serikali.

Silaha kali

Jeshi hilo la Monusco limelazimika kufanya mashambulio ya anga na ardhini ili kuzuia waasi hao wa M23 kukaribia Goma na ripoti zinasema mapigano makali yanaendelea katika maeneo ya milima ya Kibati, takriban kilomita kumi na tano Kaskazini mwa Goma.
Watu wapatano laki mbili wanasemekana kuishi katika eneo hilo la Kibati.
Wapiganaji wa M23 wamesema kuwa wanajeshi wa Congo na wenzao wa Umoja wa Mataifa walifanya mashambulio ya anga na ardhini katika maeneo wanayoyadhibiti, Kaskazini mwa Goma.
Daktarri mmoja mjini Goma, Isaac Warwanamiza, ameliambia shirika la habari la AP kuwa aliona miili ya watu themanini na wawili, ishirini na tatu zikiwa za wanajeshi wa serikali.
Umoja wa Mataifa una zaidi wanajeshi elfu kumi na nane nchini Congo

UINGEREZA INAWEZA KUISHAMBULIA SYRIA BILA IDHINA YA UN

Uingereza huenda ikaanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria, bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Hayo ni kwa mujibu wa ushauri wa wataalamu wake wa masuala ya kisheria.
Ushauri huo unasema, mashambulio hayo yatahitajika ikiwa yatatekelezwa ili kuzuia raia kuuawa, hata ikiwa wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Urussi na Uchina zikitumia kura zao za turufu kupinga mikakati za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria.
Maafisa wa ujasusi nchini Uingereza wamemueleza Waziri Mkuu, David Cameron kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulio la kemikali wiki iliyopita mjini Damascus.
Wabunge wa Uingereza wanatarajiwa kujadili suala hilo katika kikao chao cha leo jioni.
Serikali ya Syria imekana madai ya kutumia silaha za kemikali katika shambulio mjini Damascus tarehe 21 mwezi huu, ambapo mamia ya watu waliuawa.
Lakini Bwana Cameron anaamini kuwa kuna ushahidi wa kutosha kutoka wa maafisa wake wa ujasusi na pia kutoka kwa wanainchi kuhusu ukatili unaofanywa na utawala wa sasa wa Syria.
Ofisi ya Waziri mkuu wa Uingereza, imechapisha ripoti hiyo, kuambatana na ushauri wa mkuu wake wa sheria Dominic Grieve, inayotoa idhini ya mashambulio ya kijeshi ili kuzuia utumiaji wa silaha za kemikali siku zijazo, kuambatana na sheria za kimataifa.

Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema atapokea ripoti kutoka kwa wachunguzi wake wa silaha, wanaochunguza ikiwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria.
Mamia ya watu wanaripotiwa kuuawa kwenye shambulio hilo, lililofanyika karibu na mji mkuu wa Damascus wiki iliyopita.
Rais wa Marekani Barack Obama, am
Mataifa mengine pia yanajadili hatua watakayo chukua na Uingereza imekuwa ikishinikiza baraza la Usalama la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha azimio litakalihakisha raia wamelindwa nchini Syria.
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema taifa lake litajilinda kutokana na shambulio lolote kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Syria kujilinda asema Assad

Awali Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Labour, nchini Uingereza, Ed Miliband, amesema bunge la nchi hiyo halipaswi kuamua ikiwa itaidhinisha mzozo wa Syria kutatuliwa Kijeshi.
Milliband ameyasema hayo muda mfupi kabla ya bunge la Uingereza kupiga kura ikiwa Uingereza itaishambulia Syria, kufuatia madai ya kutumia silaha za kemikali mjini Damascus.
Waandishi wa habari wanasems serikali ya Uingereza inahofia huenda ikapoteza kura hiyo na hivyo kukosa idhini ya kuingilia mzozo huo wa Syria.
Milliband amesema wamejifunza mengi kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa miaka ya zamani kama ule wa kuivamia Iraq.
Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuipa jopo maalum na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nafasi ya kufanya kazi yao.
Serikali ya Uingereza imesema ina habari za kujasusi kuhusu Syria na itachapisha ripoti hiyo na ushauri wa kisheria kabla ya mjadala huo kuanza bungeni.
esema ha
jaamua kuhusu mpango wa kuishambulia Syria kijeshi


 

Alhamisi, 22 Agosti 2013

Star wa "Prison Break" Wentworth Miller (MichaelScolfield) amejiweka wazi kuwa yeye ni Shoga

 
Star wa "Prison Break",  Wentworth Miller  a.k.a Michael Scofield, amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga), katika barua ya wazi aliyoiandika kwenda kwa Directoe wa St. Petersburg International Film Festival (tamasha la filamu la kimataifa la St. Petersburg)

Muigizaji huyo (41) ameandika barua hiyo kukataa mualiko uliokuwa ukimtaka kuhudhuria tamasha hilo linalofanyika nchini kwao Russia na kwa mara ya kwanza kupitia barua hiyo amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga).
"Asante kwa ukarimu wa mualiko wako, nikiwa kama mtu ambaye amefurahia kutembelea Russia kwa miaka ya nyuma na naweza pia kudai shahada ya asili ya kirusi, ningefurahi kusema ndio, hata hivyo nikiwa kama shoga lazima nikatae". amesema Miller

Miller akaendelea kusema ... nasumbuliwa sana na tabia ya sasa dhidi ya na jinsi wanavyochukuliwa mashoga na wanawake  na serikali ya Urusi.

"hali hii haikubaliki kabisa, na mimi siwezi kwa dhamira nzuri kushiriki katika tukio la kusherehekea linaloandaliwa (wenyeji) na nchi ambayo watu kama mimi kwa mfumo uliopo wananyimwa haki zao za msingi za kuishi na kupenda kwa uwazi"

akamalizia kwa kusema.. kama hali hii itarekebishwa, nitakuwa huru kufanya uchaguzi tofauti.

Alhamisi, 8 Agosti 2013

Bilionea Wama dini Mererani auawa kwa risasi 20 Moshi







Moshi. Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana.
Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,
aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
“Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.
Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.
Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.
RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara,” alisema.
Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.
Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.
Kijana pekee wa kabila la kimasai anayedaiwa kushuhudia mauaji hayo, aliwaeleza polisi kuwa mara baada ya Erasto kufika eneo hilo la mtaa wa Wasomali, alisimamisha gari na kuwapigia wauaji.
Habari hizo zimedai kuwa vijana wale wawili walipokea simu hiyo na kumtaka ashuke kwenye gari lake la kifahari aina ya Range Rover New Model, ili wafanye biashara ambayo haijui.
Inadaiwa kuwa Erasto alipojaribu kupeleka mkono ili achomoe bastola, mmoja wa wale vijana alianza kumshambulia kwa risasi nyingi ambazo zilimfanya afariki dunia papo hapo.
Kijana huyo wa kimasai anayedaiwa kuwa msaada mkubwa kwa polisi, alidai kuwa baada ya Erasto kudondoka chini, vijana hao walichukua begi alilokuwa nalo na kutokomea.
Pikipiki iliyotumika yapatikana
Taarifa zilizopatikana baadaye jana jioni zilisema pikipiki iliyotumika katika tukio hilo imepatikana katika kijiji cha Olkolili, huko Sanyajuu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.
Kamanda Boaz alithibitisha kupatikana kwa pikipiki hiyo yenye nambari za usajili T316 CLV ikiwa imetelekezwa baada ya gurudumu moja kupata pancha baada ya kufika katika eneo hilo.
“Kwa vile tulikuwa tumesambaza taarifa kila mahali kwamba kuna raia wema walituarifu kuwa kuna watu wametelekeza pikipiki, baada ya kupata pancha na walikuwa wakitembea kwa miguu,” alisema.
Alisema Polisi walikwenda katika eneo hilo na mashuhuda walioshuhudia tukio hilo la mauaji wameitambua pikipiki hiyo kuwa ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na wauaji wa mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema pia kuwa polisi watachunguza kwa kina mawasiliano ya simu ya mfanyabiashara huyo, kwa lengo la kutafuta watu wa mwisho kuwasiliana na marehemu.

Utajiri wake marehemu Msuya Katika kipindi cha uhai wake, marehemu alikuwa akijihusisha na uchimbaji na biashara ya madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani na jiji la Arusha. Kutokana na biashara zake hizo, alimudu kumiliki mali kadhaa zikiwemo nyumba za kawaida za kuishi pamoja na hoteli maarufu Arusha ya SG Resort iliyoko eneo la Sakina. Pamoja na hoteli na nyumba kadhaa zilizoko mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, marehemu pia alikuwa akimiliki magari kadhaa ya kifahari. Nyongeza na Peter Saramba, Arusha

Ijumaa, 2 Agosti 2013

SAYANSI YA UFUFUAJI: MIAKA 20 IJAYO MADAKTARI WATAKUWA NA UWEZO WA KUWARUDISHIA UHAI WAGONJWA WALIOKATA ROHO!


dr
Twende taratibu, hii ni taarifa ya kisayansi na sio ‘kiimani’ na imetolewa na daktari bingwa wa moyo wa Marekani. Sasa naomba uniruhusu nikuelezee nilichokutana nacho kuhusiana na habari hii.
Dr Sam Parnia wa Marekani amedai kwamba kwa kupitia mbinu za kisasa za kitaalamu (kisayansi) kuna uwezekano wa kumrudishia uhai mgonjwa aliyekata roho ndani ya saa 24!! (hata mimi nimeguna)
Dr huyo wa moyo ambaye amepata mafunzo yake nchini Uingereza, ameendelea kusema hivi karibuni wanategemea kuanza kuokoa maisha ya wagonjwa wanaokuwa tayari wamekata roho katika masaa ya mwanzo baada ya kuthibitisha wamefariki. “We may soon be rescuing people from death’s clutches hours, or even longer, after they have actually died.” Alisema Dr Sam
Parnia ameendelea kutetea kauli hiyo kwa kusema kuwa muigizaji wa Marekani James Gandolfini aliyefariki mwezi uliopita angeweza kupona endapo angekuwa ameugulia tatizo lake la moyo New York.
“I believe if he died here, he could still be alive. We’d cool him down, pump oxygen to the tissues, which prevents them from dying, Clinically dead, he could then be cared for by the cardiologist. He would make an angiogram, find the clot, take it out, put in a stent and we would restart the heart,” Dr Parnia alilieleza jarida la Der Spiegel la Ujerumani.



dr-3
Dr Parnia ambaye ni mkuu wa kitengo cha ‘Intensive care’ katika hospitali ya the Stony Brook University iliyoko New York, Marekani aliendelea kusema ni kweli hawawezi kuokoa maisha ya kila mtu sababu wagonjwa wengi wa moyo huwa na matatizo mengine ya ziada na makubwa zaidi.
Aliendelea kusema kama teknolojia ya kisasa ya tiba na mafunzo vingekuwa vinafanyiwa kazi inavyotakiwa, (kitu ambacho anadai bado hakijafanyika) basi watu ambao wangetakiwa kufa ni wale tu wenye matatizo ambayo hayatibiki kabisa lakini sio ugonjwa wa moyo unaotibika.
’‘A heart attack is treatable. Blood loss as well. A terminal cancer isn’t, neither are many infections with multiresistant pathogens. In these cases, even if we’d restart the heart, it would stop again and again”.
Akielezea jinsi ambavyo mgonjwa wa moyo aliyefariki anavyoweza kurudishiwa uhai, alisema kwanza ni kuugandisha mwili mara tu baada ya kuthibitishwa amefariki , “freezing the body immediately after death – but cooling it down to best preserve brain cells while keeping up the level of oxygen in the blood. This buys time to fix the underlying problem and restart the heart”. Alisema
Dr huyo alisema kuna uwezekano katika miaka 20 ijayo madaktari watakuwa na uwezo wa kurudisha uhai wa wagonjwa masaa 12 hadi 24 toka wathibitishwe kufa na kuiita hiyo kuwa ni sayansi ya ufufuaji, “You could call that resurrection, if you will. But I still call it resuscitation science”.
Dr Parnia ameandika kitabu kipya kiitwacho ‘Erasing Death’.

SOURCE: DAILY MAIL

Jumatatu, 15 Julai 2013

CCM Chali, Chadema yaibuka kidedea Arusha

Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana.
Katika uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na ambao ulichukuliwa kama kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na mvutano mkubwa, Chadema kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni).
Matokeo
Katika matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa Chadema aliyepata kura 2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika Kata hiyo kulikuwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).
Katika Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa Chadema aliibuka na ushindi baada ya kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe aliyepata kura 326 na Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura 307.
Kata ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi, Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi ya Emmanuel Mliari wa CCM aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata kura 275 na Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura mbili.
Kata ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi, Suleiman Kilingo alimtangaza Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 2,761 na kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163. Kwa matokeo hayo, Chadema sasa kimefikisha madiwani 12 wakati CCM kimebakiwa na kumi na moja na TLP kina wawili.
Ushindi huo wa Chadema una athari kwa nafasi ya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kwani CCM kina wajumbe 14 tu kwenye Baraza la Madiwani, TLP wawili wakati Chadema sasa kimefikisha 15. Wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu pia ni madiwani.
Aidha, Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti kingine cha udiwani kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kinatarajiwa kuitisha uchaguzi mdogo Kata ya Sombetini.
Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alimwambia mwandishi wetu kuwa tume yake inatarajia kuitisha uchaguzi mdogo hivi karibuni baada ya kata hiyo kutangazwa wazi na Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi.
Malaba alisema uchaguzi huo utaitishwa baada ya aliyekuwa Diwani wake, Alphonce Mawazo kujitoa CCM na kujiunga na Chadema hali inayokifanya chama tawala kuwa katika wakati mgumu kukitetea kiti hicho.
Wachache wajitokeza
Uchaguzi ulikuwa na idadi ndogo ya wapigakura kulinganisha na chaguzi zilizopita.
Elerai inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wapigakura 23,885 waliojitokeza ni 3,824 tu ikifuatiwa na Kimandolu yenye wapigakura 17,209 lakini waliopiga kura ni 3,967.
Kata ya Kaloleni ina wapigakura 12,674 hata hivyo, waliopiga kura ni 2,292. Themi yenye wapigakura wachache kuliko zote ikiwa na watu 6,387 lakini waliojitokeza kupiga kura ni 1,319 tu.
Licha ya idadi hiyo ndogo, baadhi ya wapigakura waliojitokeza walishindwa kutimiza dhamira yao baada ya kugundulika dosari kadhaa kwenye vitambulisho vyao na Daftari la Kudumu la Wapigakura.
“NEC wamevuruga uchaguzi huu makusudi kwa kuchezea Daftari la Wapigakura kwa nia ya kukibeba CCM. Haiwezekani waliopiga kura Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 leo hii waambiwe majina yao hayamo kwenye daftari,” alilalamika mgombea udiwani Kata ya Kaloleni, Abbas Mkindi ‘Darweshi’.
Mkindi aliyewania kiti hicho kupitia CUF alitoa mfano wa mtoto wake, Omar Othman mwenye kitambulisho cha mpigakura namba 32479962 alichokitumia mwaka 2010 kuzuiwa kupiga kura baada ya jina lake kukosekana kwenye Daftari hilo. Wapiga kura wengine, Godchan Msella mwenye kadi namba 32479396  na Richard Minja mwenye namba 32479311 alizuiwa kupiga kura baada ya kubainika kuwa namba iliyopo kwenye Daftari ni tofauti na ya kadi yake.
Kutokana na kuwapo kwa mkanganyiko huo, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Hamid Mohamoud Hamid alilazimika kuwaita wataalamu wa mfumo wa kompyuta (IT), katika Kituo cha Kupiga Kura cha Kaloleni kusaidia, kazi ambayo ilifanywa na timu iliyoongozwa na Seif Mtero.
Malaba alikiri uwezekano wa kutokea tofauti za tarakimu kwenye vitambulisho vya wapigakura na Daftari la Kudumu la Wapigakura huku akishauri wasimamizi na mawakala wa vyama kutumia busara kuruhusu wananchi wenye vitambulisho na maelezo sahihi kupiga kura.
“Tofauti ya tarakimu kwenye kadi ya mpigakura na Daftari la Mpiga Kura ni kosa la NEC, hivyo siyo sahihi kuwahukumu wapiga kura kwa kuwanyima haki yao ya kuchagua viongozi wawapendao,” alisema Malaba.
Amani yatawala
Ukiacha dosari na idadi ndogo ya wapiga kura, uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa tofauti na hofu iliyokuwapo awali kwamba huenda vurugu zingeibuka kutokana na mvutano uliopo kati ya vyama vya CCM na Chadema.
CHANZO: www.mwananchi.co.tz

Jumatatu, 1 Julai 2013

Rais Barack Obama awasili Tanzania

Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani Afrika.

Ziara ya Obama inasemekana kulenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika. 

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.

Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.

Baadhi ya wananchi wa Tanzania kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa ziara ya Obama katika nchi yao, wakisema kuwa ziara yake imeathiri shughuli za maisha yao ya kila siku.

Obama alitembelea Senegal kabla ya kupitia Afrika Kusini na kisha Tanzania ambako ziara yake ya Afrika inaishia kabla ya kurejea Marekani.

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More