Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Jumanne, 30 Aprili 2013

Borussia Dortmund yapeta - Real Madrid 2-0 Borussia Dortmund


Borussia Dortmund imejikatia tiketi ya kuingia fainali ya Klabu bingwa Ulaya 2012-13 baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-3 dhidi ya Real Madrid. Real Madrid imeshinda 2-0  katika mechi ya nusu fainali  ya pili katika Bernabeu Jumanne. Lakini imeshindwa kusonga mbele kutokana na kipigo ilichopata cha magoli 4-1 Kutoka kwa Borussia Dortmund walipokuwa nyumbani wiki iliyopita.
Upande wa timu hiyo ya Bundesliga ulinusurika kutolewa katika kinyang’anyiro hicho. Na kama Rael Madrid wangefanikiwa kuongeza goli moja wangekuwa pazuri zaidi kwakuwa na goli moja la ugenini. Lakini bahati haikuwa upande wao na hivyo kupoteza nafasi hiyo na kutolewa
Hata hivyo, magoli kutoka Karim Benzema na Sergio Ramos katika dakika 10 za mwisho  ghafla ilianzisha nguvu mpya, lakini Dortmund ikiwa juu kimagoli wameingia fainali ya kwanza tangu mwaka 1997, wakati ilipofungwa Juventus 3-1.
Vijana wa Mourinho walijua ukubwa wa kazi waliyokuwa nayo, na walianza mchezo kwa umakini wakiwa na kiu ya kufanya mapinduzi. Gonzalo Higuain angeweza kufungua mchezo kwa bao mnamo dakika nne, lakini shuti alilounganisha toka kwa Mesut Ozil liliishis mikononi mwa Weidenfeller Roman.
Lewandowski alikosa kutoka yadi nane, kabla ya Madrid hatimaye alionyesha dalili ya uhai katika nusu ya pili.
Benzema akitokea benchi wakati zikiwa zimesalia dakika saba, alionyesha uhai na kuipa timu yake nguvu ya kuusaka ushindi baada ya kuipatia goli timu hiyo ya hispania.
Madrid ilipata jumla ya magoli 2 katika mechi hiyo ingawa magoli hayo hayakutosha kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele kwenye hatua ya fainali
Sasa swali kuu ni je Wembley zitacheza timu zote za kijerumani ama Barcelona inaweza kufanya mabadiliko hapo kesho?

Jumatatu, 29 Aprili 2013

Majaji wamnusuru Jerry Muro na wenzake


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemnusuru aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili katika hatari ya kesi yao kusikilizwa umpya, badala yake itaendelea kusikilizwa kama rufaa.
Awali kesi hiyo ilikuwa kwenye hatari ya kusikilizwa upya baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, kudaiwa kufanya makosa katika utoaji wa hukumu ya Muro na wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius  Mugassa.
Hata hivyo leo Majaji wa Makahama ya rufaa wametupilia hoja za mawakili wa Serikali waliotoa hoja za kutaka kesi hiyo isikilizwe upya.
Hoja za Jamhuri wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Oktoba 18, mwaka huu, Mawakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya na Awamu Mbangwa, waliiomba mahakama hiyo iamuru kesi hiyo isikilizwe upya chini ya kifungu cha 388 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Wakili Mbangwa alidai kuwa Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo (Gabriel Mirumbe) alikosea kisheria katika kuweka kumbukumbu za
mwenendo wa kesi.
Alidai kuwa kutokana na dosari hizo, hata hakimu aliyeandika hukumu ya kesi hiyo (Frank Moshi) aliegemea katika mwenendo huo ambao haukurekodiwa vizuri na matokeo yake alitoa hukumu isiyo sahihi.
Wakili Mbangwa alifafanua kuwa katika mwenendo wa kesi hiyo kuna sehemu za ushahidi wa baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka, umerekodiwa kwa namna ambayo hauakisi uhalisia wa kile mashahidi hao walichokiziunguza. Aliongeza kuwa kuna baadhi ya sehemu za ushahidi hazikurekodiwa kabisa ikiwemo uamuzi wa mahakama kukataa kupokea kitabu cha wageni waliokuwa wakifika katika hoteli ya Sea Clif ambako Muro na wenzake walidaiwa kukutana na Wage.
Jerry Muro akiwa chini ya Ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,mwaka 2010Alidai kuwa kutokuwepo kwa uamuzi wa suala hilo katika kumbukumbu kuliinyima nafasi jamhuri kujua sababu za kukataliwa kwa kielelezo hico. Pia alitoa mfano wa maelezo ya onyo ya mjibu rufaa wa kwanza, Muro, kutokuoneshwa kwenye kumbukumbu kuwa yaliopokewa mahakamani hapo. Majibu ya utetezi Wakijibu hoja hizo, mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza na Majura Magafu walidai kuwa malalamiko ya Jamhuri katika hukumu hiyo hayako wazi na kwamba hata kama yapo lakini hawajaonesha jinsi yalivyoathiri hukumu hiyo.
Wakili Magafu alidai kuwa mazingira ya kesi walizozitumia Jamhuri ni tofauti na mazingira ya rufaa hiyo na kwamba kitendo cha Jamhuri kuomba kesi hiyo isikilizwe upya ni sawa na biashara ya kuchagua mahakimu kwamba wakishindwa kwa hakimu mmoja wanakwenda kubahatisha kwa hakimu mwingine. Hata hivyo Wakili wa Serikari Tibabyekomya alidai kuwa hukumu hutokana na ushahidi wa pande zote na kwamba kutokurekodiwa vizuri kwa mwenendo huo na kasoro hizo zilisababisha haki isitendeke kwa pande zote.
Jaji Twaib Jaji Dk Twaib alihoji Jamhuri kama kama mwenendo huo uliochapwa ndivyo ulivyo kwenye mwenendo halisi. Ili kujiridhisha, aliamua kusoma mwenendo halisi uliondikwa kwa mkono, lakini yeye binafsi na hata wakili wa utetezi, Magufu, waalishindwa kuelewa baadhi ya maneno yaliyoandikwa. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Jaji Dk Twaib aliahirisha rufaa hiyo hadi leo kwa ajili ya uamuzi. Muro na wenzake walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 5, mwaka 2010, na kusomewa mashtaka kula njama na kuomba rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage.

GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha. Kwa sasa mamia ya wafuasi wa Chadema wanaandamana na mbunge huyo kuelekea makao makuu ya chama hicho.

Iraq yaifungia Al-Jazeera, vituo vingine tisa

Seriakli ya Iraq imekifungia kituo cha televisheni cha kimataifa cha Aljazeera na vituo vingine tisa vya nchini humo siku ya Jumapili, baada ya kivituhumu kwa kuchochea vurugu za kidini.
Hatua hii imemulika wasiwasi unaozidi wa serikali inayoongozwa na washia, juu ya hali ya usalama inayozidi kudorora, wakati wa machafuko ya waumini wa kisunni na makabiliano yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 180 katika muda wa chini ya wiki moja. Kusimamishwa kwa vituo hivyo ambako utekelezaji wake ulianza mara moja kunaonekana kuvilenga hasa vituo vya kisunii vinavyojulikana kwa kuikosoa serikali ya waziri mkuu Nouri al-Malik.
  Wanamgambo wenye silaha wanaoipinga serikali kutoka maeneo ya wasunni wakiandamana mjini Ramadi, mashariki mwa Baghdad.
 
Pamoja na kituo cha Aljazeera, uamuzi huo uliviathiri vituo nane vya kisunni na kimoja cha kishia. hatua hii ya serikali imekuja huku utawala mjini Baghdad ukijaribu kukabiliana na ongezeko la machafuko nchini humo, yaliyoripuka siku chache zilizopita, baada ya vikosi vya usalama kuanzisha operesheni ya ukandamizaji dhidi ya kambi ya waandamanaji wa kisunni katika mji wa kati wa Hawija, na kuua watu 23, wakiwemo wanajeshi watatu.
Tangu wakati huo, zaidi ya watu 180 wameuawa katika mapigano na vikosi vya usalama na mashambulizi mengine. Wimbi la hivi karibuni la vurugu linafuatia miezi minne ya maandamano ya amani ya waislamu wa madhehebu ya sunni, dhidi ya serikali ya waziri mkuu Nouri al-Maliki. Watazamaji nchini Iraq watanedelea kutizama vituo hiyvo, lakini tangazo la kusitishwa kwake lililotolewa na tume ya mawasiliano na vyombo vya habari linasema kama vituo hivyo kumi vitajaribu kuendesha shughuli zake katika ardhi ya Iraq, vitakabiliwa na hatua za kisheria kutoka kwa vyombo vya usalama. Kimsingi amri hiyo inawazuia wanahabari kutoka vituo hivyo kufanya kazi zao nchini Iraq.
Aljazeera yashtushwa na kufungiwa
Mbunge wa Kisunni Dahfir al-Ani aliielezea hatua hiyo kama sehemu ya majaribio ya serikali kuficha umuagaji damu uliyofanyika mjini Hawija na kile kinachoendelea katika maeneo mengine nchini humo. Al-jazeera ilisema katika taarifa kuwa imeshangazwa na hatua hiyo ya serikali ya Iraq, na kuongeza kuwa imekuwa ikiripoti pande zote za habari nchini Iraq kwa miaka mingi. Aljazeera iliripoti kwa undani kuhusu mapinduzi katika mataifa ya kiarabu, na imekuwa ikiripoti kwa kiasi kikubwa kuhusu mgogoro unaondelea nchini Syria.
Magazeti na vyombo vingine vya habari vilianzishwa nchini Iraq baada ya kuanguka kwa utawala wa Saddam Hussein mwaka 2003, lakini nchi hiyo imeendelea kuwa mmoja yenye hatari zaidi kwa waandishi wa habari, ambapo zaidi ya 150 wameuawa tangu mwaka 1992, kwa mujibu wa kamati ya kulinda waandishi wa habari.
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki.  
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki.
 
Iraq na serikali nyingine za mashariki ya kati ziliwahi kufunga ofisi za Al-Jazeera kwa muda huko nyuma, kwa sababu hazikupendezwa na jinsi inavyoripoti matukio. Vituo vingine tisa ambavyo leseni zake zimefungiwa na tume ya mawasiliano ya Iraq ni pamoja Al-Sharqiya na Al-Sharqiya News, ambacho kinaikosoa serikali mara kwa mara, na vituo vingine vidogo saba vikiwemo Salahuddin, Fallujah, Taghyeer, Baghdad, Babiliya, Anwar 2 na al-Gharbiya.
Televisheni ya Baghdad yasema ni uamuzi wa kisiasa
Televisheni ya Baghdad iliyopo mjini Baghdad, ilisema uamuzi huo ulikuwa ni wa kisisiasa. "Serikali ya Iraq haina uvumilivu kwa maoni yanayokinzana na wanajaribu kunyamanzisha sauti zinazokwenda kinyume na msismamo rasmi," alisema Omar Subhi, mkurugenzi wa kitengo cha habari. Alisema Televisheni hiyo ilikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa wafanyakazi wake, ikihofia kuwa vikosi vya usalama vinaweza kuwafukuza.
Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao wake, tume ya habari ya serikali ilivilaumu vituo vilivyofungiwa kwa kuongezeka kwa wasiwasi wa kidini, ambao unachochea vurugu zilizofuatia mapigano ya maafa mjini Hawija. Tume hiyo ilivishtumu vituo kwa kutoa ripoti za upotoshaji na zilizotiwa chumvi, kutangaza wito wa dhahiri wa uvunjivu wa amani, na kuanzisha mashambulizi ya kihalifu ya kulipiza kisasi dhidi ya vyombo vya usalama. Pia ilivilaumu vyombo hivyo kuyatangaza makundi ya kigaidi yaliyopigwa marufuku, yaliyotenda uhalifu dhidi ya watu wa Iraq.
Osama Abdul-Rahman, mfanyakazi wa serikali wa madhehebu ya kisunni kutoka kaskazini mwa Baghdad, alisema serikali inatumia sera ya ndumila kuwili kuhusiana na vyombo vya habari, kwa kuvifumbia macho vituo kadhaa vya kishia ambavyo anadai vinachochea vurugu. "Vituo vilivyo karibu na vyama vikuu vya kishia na hata televisheni ya taifa pia vinarusha vipindi vya ubaguzi wa kidini vinavyochochea vurugu muda wote, lakini hakuna mtu anaevisimamisha," aliongeza.
  Wananchi wakibeba jeneza la mwanajeshi alieuwawa katika vurugu za hivi karibuni.
 
HRW yasema madai ya serikali yana mashaka
Erin Evers, mtafiti wa masuala ya mashariki ya kati kutoka shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch, aliyaita madai ya serikali kwamba imevivhukuliwa hatua vituo vya televisheni kwa kuchochea ubaguzi wa kidini kuwa ya mashaka, kwa kuzingatia "historia yake endelevu ya ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari - hasa vyombo vya habari vinavyoegemea upinzani -hasa katika nyakati nyeti kisiasa."
"Kufungiwa kwa vituo hivyo ni ushahidi mwingine kuwa serikali inataka kuzuia kuripotiwa kwa habari wasizozipenda," alisema Evers. Aliituhumu tume ya habari ya Iraq kwa kuchanganya ripoti ya hotuba iliyo na vidokezo vya ubaguzi wa kidini na kuchochea kwa wazi kwa vurugu za kidini. "Haya ni mambo mawili tofauti kabisaa na lwa kwanza linalindwa chini ya sheria za kimataifa na za Iraq pia," alisema.
Uamuzi wa kufungia vituo hivyo ulikuwa wakati ambapo al-Maliki akihudhuria isivyo kawaida katika maziko rasmi ya wanajeshi watano waliouawa siku ya Jumamosi, na watu wenye silaha katika mkoa wa wasunni wa Anbar. Polisi katika mkoa huo ilisema wanajeshi hao waliuawa katika mapigano baada ya gari lao kusimamishwa karibu na kambi ya maandamano ya wasunni.
  Matukio ya mashambulizi kama hili yameongezeka nchini Iraq.
 
Serikali ilitoa muda wa masaa 24 kwa waandaji wa maandamano hayo kukabidhi watu waliohusika na mauaji hayo, au wakabiliwe na hatua kali. Lakini hakuna mtu aliekabidhiwa na muda uliyotolewa umepita. Siku ya Jumamosi, watu wenye silaha wakitumia bunduki zilizofungiwa vifaa vya kuzuia sauti, walipiga risasi na kuwauwa viongozi wawili wa kikabila wasunni katika matukio mawili tofauti ya kusini mwa Baghdad.
Miripuko yazidi kutikisa
Wakati huo huo, miripuko mitatu ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari imesababisha vifo vya watu wasiopungua 20 kusini mwa Iraq siku ya Jumatatu, katika maeneo yanayokaliwa na washia wengi. Mripuko moja ulitokea karibu na soko, wakati mwingine ulitokea karibu na mkusanyiko wa wafanyakazi katika mji wa Amara, uliyopo kilomita 400 kusini-mashariki mwa Baghdad. Mripuko huo uliua watu 16 na kujeruhi 25.
Kkatika mji wa Diwaniya, uliyoko kilomita 150 kusini-magharibi mwa Baghdad, bomu la kwenye gari liliripuka karibu na mgahawa, na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 11. Kuongezeka kwa vurugu hizi kunaongeza hofu ya kurudisha vurugu za kidini zilizoipeleka nchi hiyo karibu na kuripuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 2006 na 2007.

ALIYEZIKWA AKIWA HAI AFUKULIWA NA KUKUTWA AMEKUFA CHUNYA MBEYA

JENEZA LA ALIYEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUKULIWA
MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUTOLEWA KABURINI
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
  
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu  majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.
Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika  marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
  
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.
  
Baada ya Mzee huyo  kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye kaburi moja.
  
Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.
  
Hata hivyo baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Credo Kayanza ambaye pia alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata hiyo Chesco Ngairo ambao kwa pamoja walitoa taarifa Jeshi la Polisi ambao baada ya taarifa hiyo walifika eneo la tukio huku wakidhani lililotokea ni kuchomwa kwa nyumba pekee.
  
Jeshi la Polisi baada ya kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.
  
Baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita ukizikwa upya palepale.
  
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na kuwaasa  wananchi na jamii kuacha tabia  ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.
Aidha ameongeza kuwa wakumbuke kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia  amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Rais wa Algeria alazwa hospitalini Ufaransa

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amepelekwa mjini Paris Ufaransa kwa matibabu baada ya kupatwa na kiharusi.
Bwana Bouteflika, mwenye miaka 76, alipata tatizo la mshipa wake wa damu kuziba kwa muda, hali ambayo inasemekana kuwa kiharusi.
Jumapili, Madaktari walisema kuwa rais huyo anapata nafuu na kuwa athari aliyopata kutokana na kuziba kwa mshipa wa damu inaweza kutibika.
Bwana Bouteflika anapokea matibabu katika hospitali ya kijeshi ya Val de Grace ambayo huwapokea wagonjwa mashuhuri kutoka ndani na nje ya Ufaransa.
Aidha daktari wake Rachid Bougherbal, alisema kuwa hali aliyokuwa nayo mgonjwa wake haikudumu kwa muda mrefu na inaweza kutibika. Aliongeza kuwa hali yake sio mbaya na anaendelea kupata nafuu.

Ripoti kuhusu Saratani

Waziri mkuu Abdelmalek Sellal alirejelea wito wake kwa wananchi kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu rais huyo.
Bwana Bouteflika, ambaye kawaida huwa haonekani hadharani sana alifanyiwa upasuaji mjini Paris Miaka michache iliyopita.
Kulingana na taarifa ya madaktari ni kuwa alikuwa na vidonda vya tumbo , lakini taarifa iliyofichuliwa baadaye ilisemekana kuwa alikuwa na saratani ya tumbo.
Licha ya umri wake na hali yake duni ya kiafya, kunao wanaoamini kuwa bwana ,Bouteflika huenda akawania muhula wake wa nne wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka ujao.
Yeye ni mmoja wa viongozi wakongwe ambao wamekuwa wakiongoza Algeria, tangu nchi hiyo kujipatia uhuru miaka hamsini iliyopita.

CHANZO: bbc.uk/swahili

Nyumba nyingi kuporomoka nchini

Dar es Salaam. Imebainika kuwa nyumba nyingi zilizopo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, zipo hatarini kubomoka kutokana na kujengwa kwa matofali yasiyokuwa na ubora.
Pia, hatua hiyo inatokana na kutokuwapo kwa ukaguzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi yakiwamo matofali ya saruji yanayotumika katika ujenzi wa nyumba hizo.
Uchunguzi uliyofanywa na Mwananchi hivi karibuni jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneo nchini, umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la biashara holela ya matofali yanayotengezwa kwa ubora hafifu.
Uchunguzi pia unaonyesha kutokuwapo kwa usimamizi wa kutosha katika sekta ya ujenzi nchini ni moja ya vyanzo vya watu kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kiholela.
Biashara hizo ni pamoja na uuzaji wa matofali yasiyokuwa na viwango kutokana na kukosa udhibiti maalumu.
Moja ya mambo yanayosababisha matofali yanayotumika katika ujenzi jijini Dar es Salaam kuonekana kuwa hayana ubora ni utengenezaji wa matofali hayo.
Imegundulika kuwa saruji inayotumika katika utengenezaji huo ni ndogo na mchanga unakuwa mwingi kwa lengo la kutengeneza matofali mengi ili kupata faida.
Wakati uchunguzi huo ukionyesha hivyo Mwananchi, ilimtafuta Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Mhandisi Boniface Muhegi, ambaye alishauri kufanyika kwa uchunguzi wa bidhaa zinazotumika katika ujenzi.
Muhegi anasema “Ili kuepusha madhara hasa kuanguka kwa majengo ni vyema Shirika la Viwango Tanzania (TBS), likachukua hatua ya kufanya ukaguzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi ili kuongeza usalama katika masuala ya ujenzi.|
Anasema ili kuhakikisha kuwa majengo yanakuwa salama, ni vyema watu wakatumia wakandarasi waliosajiliwa ili kuwabana wakati kunapotokea madhara.
“Sisi tunashauri kwamba kama mtu anataka kujenga nyumba amayo ni salama, ni vyema akatumia wakandarasi waliosajiliwa ili iwe rahisi kuwabana wakati tatizo lolote linapojitokeza,”anasema.
Mhandisi Muhegi anasema “Ni vyema wananchi nao wakatambua kwamba matumizi ya vifaa visivyokuwa na viwango sio salama kwa maisha yao”.
Anasema kila mmoja aone haja ya kutumia vifaa vyenye ubora ili kujihakikishia usalama wa makazi yake na kuepusha kutokea kwa majanga mbalimbali.
“Kama tutakuwa makini katika matumizi ya vifaa bora vya ujenzi tutakuwa na makazi salama na tutaepusha majanga mbalimbali.
NUKUU
Machi 29 mwaka huu jengo la ghorofa 16 liliporomoka jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30.
Febuari 17 mwaka huu, jengo lingine la ghorofa tatu liliporomoka huko Sinza Mori Dar es Salaam na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili waliokolewa na vikosi vya uokoaji.
Mwaka 2006 Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliunda tume ya kufuatilia ujenzi wa maghorofa na kubaini kuwa zaidi ya majengo 100 jijini Dar es Salaam yamejengwa bila kuzingatia vigezo.
Msomaji wetu kama una maswali yoyote kuhusiana na ujenzi na ubora wa majengo unaweza kumuuliza Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), kwa kutuma kupitia baruapepe: mwananchijumamosi@yahoo.com au ujumbe wa simu kupitia namba: 0658 376410

Yanga ijipange kwa mashindano ya Afrika

Timu ya soka ya Yanga ndiyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2012/2013.
Yanga imetwaa ubingwa huo ikiwa bado imebakiza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Coastal Union na Simba.
Huu ni ubingwa wa 24 kwa Yanga tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara rekodi ambayo hakuna timu yoyote ya Tanzania inayoifikia kwani Simba wanaowafuatia wametwaa ubingwa huo mara 18 tu.
Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011 na 2012-2013.
Kwa ubingwa wa Ligi Kuu iliyotwaa Yanga imepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya klabu bingwa Afrika mwakani.
Historia ya soka la Tanzania inaonyesha kuwa kabla mashindano hayo ya Afrika hayajaitwa Ligi ya Mabingwa kutoka klabu bingwa Afrika, timu ya Simba ndiyo iliwahi kufika hatua ya nusu fainali.
Tangu mashindano hayo yabadilishwe jina mwaka 1997 na kuitwa Ligi ya Mabingwa barani Afrika timu za Simba na Yanga zote zimewahi kuishia hatua ya makundi tu.
Tunaamini Yanga ambayo itatuwakilisha mwakani katika mashindano ya klabu bingwa ya Afrika ina jukumu kubwa la kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Yanga itaweza kufanya vizuri katika mashindano hayo kama viongozi wao watakuwa na malengo ya kutaka kutwaa ubingwa wa Afrika na kucheza mashindano ya FIFA ya klabu bingwa ya dunia.
Tunasema hivyo kwa sababu ili kutwaa ubingwa wa Afrika, lazima kuwe na mipango madhubuti ya kufanikisha hilo ambayo ni usajili mzuri, maandalizi mazuri na kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika.
Viongozi wa Yanga wanatakiwa kufanyia kazi ripoti watakayopewa na kocha wao mwisho wa msimu huu ili wajue kikosi chao kina mapungufu gani na wafanye vipi usajili utakaowawezesha kuwa na kikosi chenye wachezaji mahiri wanaoweza kupambana katika mashindano hayo makubwa ya Afrika.
Tunasema hivyo kwa sababu tumeshuhudia mechi nyingi za mashindano hayo ya Afrika na kuona jinsi klabu za wenzetu zilivyo na wachezaji wenye akili ya mchezo, miili ambayo imefanyishwa mazoezi kwa ajili ya kupambana uwanjani ili kupata ushindi na stamina.
Tumeona pia katika mashindano hayo ya Afrika jinsi wachezaji wa timu mbalimbali wanavyotoa pasi na kupokea mpira, kufunga mabao, kuzuia, kushirikiana, kukokota mpira, kupiga mashuti, kuusoma mchezo kwa haraka, kujiamini na wachezaji kufanya uamuzi wa haraka.
Vilevile Yanga inaweza kufanya vizuri katika mashindano hayo ya Afrika kama wachezaji watakuwa na umoja, bidii na kuwa na lengo moja la kutafuta ushindi, pia wachezaji wachezaji wanatakiwa kujiandaa wenyewe kwa kufanya mazoezi binafsi.
Tunatarajia kuona Yanga ikitumia kipindi hiki vizuri kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya klabu bingwa Afrika ili kufuta aibu ya kuishia hatua ya pili kila wakati.

Mbowe amtwisha mzigo mzito Zitto

Tabora. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki), Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo hayo yanachukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa mtaa, nyumba kwa
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine alisema anazindua kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ambapo Zito Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia  kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono chama hicho ili kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea mishahara yao kuliko ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu ikilinganishwa na ugumu wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama sisi, sasa ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili tuwakomboe wanyonge,” alisema Mbowe.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alisema Kanda ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora kuwa kitovu cha mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha mapambano ya mageuzi.


CHANZO: Mwananchi

Lema kizimbani Arusha leo

Dar/mikoani. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema anafikishwa mahakamani leo kwa madai ya kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha, huku ikielezwa kwamba jiji hilo litakuwa katika ulinzi mkali.
Ulinzi umeimarishwa maradufu katika mitaa yote jijini Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi anakoshikiliwa mbunge huyo tangu usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.
Lema anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo akidaiwa kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya wanafunzi kuchachamaa kutokana na mauaji ya mwenzao, Henry Kago aliyeuawa kwa kisu karibu na chuo hicho, Jumanne iliyopita.
Ingawa Jeshi la Polisi linadai ulinzi huo ni jukumu lao la kawaida la kila siku, lakini wingi wa askari mitaani umechagizwa na tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani leo kwa Lema suala linalotokana na rekodi ya wafuasi wa Chadema hasa kukiwa na jambo linalomhusisha mbunge wao na polisi.
Tangu baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2010, wafuasi, wapenzi na viongozi wa Chadema Arusha na kitaifa wamekabiliana mara kadhaa na Polisi mkoani hapa na moja ya matukio yanayokumbukwa ni lile la maandamano ya Januari 5, 2011 lililoishia kwa mauaji ya watu wawili huku viongozi kadhaa wa chama hicho wakifunguliwa kesi ya kusanyiko lisilo halali.
Viongozi wa Chadema wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa, Lema, wabunge kadhaa na viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa. Polisi kutoka wilaya jirani na Arusha za Arumeru, Monduli, Karatu na Longido wanahusika katika ulinzi huo ulioimarishwa tangu juzi.
Wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani wamekuwa na desturi ya kujaa mahakamani pale viongozi wao wanaposhtakiwa kwa kosa lolote na hutoka kwa maandamano yasiyo rasmi kila kesi inapoahirishwa, jambo ambalo limekuwa likizua mvutano kati yao na polisi na aghalabu kuishia kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na baadhi kutiwa mbaroni.
Ulinzi mkali ‘selo’ ya Lema
Polisi wameimarisha ulinzi katika eneo lote la Kituo Kikuu anakoshikiliwa mbunge huyo tangu Ijumaa iliyopita na tangu siku hiyo, watu ambao wamekuwa wakifika hapo kwa sababu mbalimbali wamelazimika kujieleza kwanza kwa askari wa doria kabla ya kuruhusiwa kukaribia lango la kituo hicho.
Katika mitaa mbalimbali nako kuna askari wenye silaha wanaotembea kwa miguu wakiwa wawiliwawili hadi watatu pamoja wale wa pikipiki na wa kikosi cha mbwa na farasi.
Kesi nyingine kubwa za leo
Mbali na kesi hiyo, huenda leo Mahakama Kuu ikatoa uamuzi wa maombi ya Jamhuri katika rufani ya kesi ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Jerry Murro na wenzake wawili.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajiwa kutoa uamuzi wa kama Muro na wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius Mugassa wapandishwe kizimbani tena na kuanza kusikiliza upya kesi ya rushwa iliyokuwa ikiwakabili au la.
Kesi nyingine ni ya anayedaiwa kumuua Padre Evaristus Mushi ambaye atapandishwa kizimbani kwa mara ya tatu.
Mtuhumiwa huyo, Omar Yusufu Makame, mkazi wa Mwanakwerekwe, Unguja alikamatwa Machi 29, mwaka huu baada ya uchunguzi uliofanywa na wapelelezi wa Tanzania walioshirikiana na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI). Pia leo kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba na wenzake na inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mara ya mwisho kesi hiyo iliahirishwa, kwa sababu Hakimu Mkuu Mfawidhi, IIvin Mugeta anayeisikiliza alikuwa na shughuli nyingine za kiofisi. Mbali na Simba, washtakiwa wengine ni Meneja wake, Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Shirika, Salim Mwaking’ida.
Katika Mahakama ya Kinondoni, dereva aliyemgonga Askari wa Usalama Barabarani, WP 2492 CPL-Elikiza na kusababisha kifo chake, Jackson Fimbo atafikishwa mahakamani leo.
Dereva huyo alimgonga askari huyo wakati msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukipita katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Kesi nyingine itakuwa huko Liwale ambako watu 31 akiwamo Diwani wa Kata ya Liwale B, Mohamedi Mtesa (CUF), wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Liwale leo wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kuharibu mali na kuchoma nyumba za mbunge, viongozi wa  vyama vya ushirika vya msingi na Mwenyekiti wa halmashauri.
Idadi hiyo ya watuhumiwa itafanya watu 68 kupandishwa kizimbani baada awali, watu 37 kufikishwa mahakamani Alhamisi iliyopita.
Mjini Sumbawanga, Rukwa, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Samweli Kisabwiti na Diwani wa Kata ya Katandala (CCM), leo anafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Sumbawanga kwa tuhuma za kutishia kujeruhi kwa panga.
Imeandikwa na James Magai (Dar), Juddy Ngonyani (Sumbawanga), Christopher Lilai (Lindi), Mussa Juma na Peter Saramba (Arusha) na Masoud Sanani (Zanzibar).

CHANZO: Mwananchi

Jumapili, 28 Aprili 2013

DIAMOND PLATNUMZ AWATUPIA UJUMBE WAREMBO WA UINGEREZA


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.

Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. 

Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”

Arsenal yaibana Man United


Ligi kuu soka nchini Uingereza imeendelea kwa michezo mitatu iliyopigwa kwenye viwanja vitatu tofauti jijini London jumapili hii.

Manchester United ambao ni mabingwa wa ligi hiyo msimu huu, Hii leo walikuwa wageni wa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates Kaskazini mwa london,
Theo Walcot alianza kuifungia Arsenal bao la mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo huo ambao BBC ulimwengu wa soka ilikuwa ikuutangaza moja kwa moja.
United walio chini ya Sir Alex Ferguson walionekana kutokuwa kwenye kiwango chao kama mabingwa baada ya kuanza mchezo huo kwa kufanya makosa mengi, na kujikuta wakipewa kadi nne za njano ndani ya dakika 30 za mchezo huo.
Lakini makosa ya safu ya ulinzi wa Arsenal, hasa lile la beki Bakar Sagna la kurudisha mpira kwa kipa wake yaani back pass yaliifanya United isawazishe bao lao kwa njia ya penati baada ya Sagna kutaka kufuta makosa kwa kumchezea vibaya Robin Van Persie ambaye aliifunga timu yake ya zamani bila ya kushangilia.
Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kugawana pointi na Arsenal kufikisha pointi 64 pointi mbili zaidi ya wapinzani wao Tottenham ambao walitoka sare pia hapo jana na Wigan.
Kwingineko Mashariki mwa jiji la London kulikuwa na michezo miwili kwenye viwanja tofauti,
Chelsea wakiwa wenyeji wa Swansea kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Mchezo uliomalizika kwa vijana wa Roman Abromavich kuibuka na ushindi wa 2-0, Mabao yao yakifungwa na Mbrazil Oscar Dos Santos Junior huku Frank Lampard akifunga kwa mkwaju wa penati.
Na Mchezo wa awali kabisa ulichezwa kwenye uwanja wa Roftus Road kwa QPR kupambana na Wigan, Mchezo ambao ulimalizika kwa sare bila kufungana.
Matokeo hayo ya sare kwa QPR na Wigan yalizifanya timu zote mbili kushuka daraja la ligi kuu.
Mechi nyingine itapigwa hapo kesho kati ya Aston Villa na Sunderland, Mechi ambayo itakuwa ni ya kukata na shoka kwani timu zote mbili zinajitutumua kutoshuka daraja.
CHANZO: bbc.uk

Mambo matatu aliyohojiwa Lema Polisi


Arusha: Kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.
Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa kwake kungehatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha kwa askari hao usiku huo wa kuamkia juzi, Lema alithibitisha kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake:
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi wangu na mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui alisema mahojiano ya mteja wake na polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa 7:50 mchana hadi saa 11:15 jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja tatu walizodai kwamba zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA).
Maneno hayo yanayotafsiriwa na polisi kuwa ni uchochezi ni pamoja na “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga” na “Nimepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa atafika, asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya msingi ya kupatiwa ulinzi.”
Kauli nyingine ni “Hawa ndio viongozi wetu (akimaanisha mkuu wa mkoa), tunaowategemea wanakuja kwenye matatizo wakijivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off.”
Lema anadaiwa kutamka maneno hayo baada ya Mulongo kugoma kuzungumza na wanafunzi kisha kurejea ndani ya gari akitaka viwepo vipaza sauti, kitendo kilichowafanya wanafunzi kuanza kumzomea kabla polisi kuanza kulipua mabomu ya machozi na kumwondoa eneo la tukio mkuu huyo wa mkoa.
Lema na Mulongo wote walikwenda IAA kutokana na tukio la kuuawa kwa kuchomwa kisu kwa aliyekuwa mwanafunzi wa taasisi hiyo, Henry Kago.
Baada ya vurugu hizo Mulungo alimtuhumu Lema kuandaa mazingira ya yeye kuzomewa .
Wakati hayo yakiendelea, askari katika kituo anakoshikiliwa Lema jana asubuhi walivutana vikali na ndugu wa mbunge huyo pamoja na uongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha baada ya kumpa dakika moja kunywa chai aliyoletewa na kukataa asipewe dawa ya meno kutoka kwa mkewe, Neema.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinasema kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chadema ulilazimika kumtuma wakili wa Lema, Method Kimomogoro kwenda Kituo cha Kati cha Polisi Arusha kujua sababu za polisi kufanya hivyo.

Mmoja wa ndugu wa Lema alisema polisi walimpa mbunge huyo dakika moja tu kunywa chai na kwamba muda huo ulipokwisha walimwongezea dakika nyingine tatu na kwamba zilipomalizika walimwamuru arejee mahabusu.
Wakati polisi wakifanya hivyo, tayari walikuwa wamekataa asipewe dawa ya meno aliyopelekewa na mkewe, Neema na kwamba matukio hayo yalizua mvutano mkali baina yake (Lema) na polisi waliokuwa kituoni hapo.
Mdee, Nassari kukutana na Mulongo
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Nassari aliliambia gazeti hili jana kwamba wameamua kutoka Dodoma hadi Arusha kwa ajili ya “kushughulikia suala hilo.”
“Jumatatu tunatarajia kuonana na mkuu wa mkoa na tayari nimempa taarifa. Tunataka kuzungumza naye kilichotokea na hali ya kisiasa kwa sasa Arusha,”alisema Nassari.
Alisema wao kama wabunge, hawawezi kukaa kimya wakati kunaonekana kuna mgogoro baina ya mkuu huyo wa mkoa na mbunge mwenzao, Godbless Lema ambao unakiuka haki za kibinadamu.
“Tutazungumza naye na tutatoa ushauri wetu …na mimi kama mbunge wa Mkoa wa Arusha, nadhani nina nafasi ya kushauriana na mkuu wa mkoa kuhusiana na hali ya mambo ilivyo sasa Arusha,”alisema Nassari na kuongeza:
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
Hata hivyo, juhudi za kumpata jana mkuu wa Mkoa wa Arusha, kuelezea kama amepokea ujumbe kutoka kwa wabunge hao, zilishindikana kutokana na kuwa katika mapokezi ya marais watano wa nchi za Afrika ya Mashariki.
Chadema kumzomea RC
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema wafuasi wa chama hicho wataendelea kumzomea Mulongo kila watakapomwona hadi pale atakapobadilika kifikra, kimwenendo, maneno na vitendo kuhusiana na uhalali wa Chadema na viongozi wake katika uongozi wa umma waliokabidhiwa kisheria.
“Kama kupigiwa makofi na kushangiliwa anapofanya vyema kazi yake,
vivyohivyo mkuu wa mkoa ategemee kukumbana na zomeazomea kubwa kuliko aliyopata Uhasibu iwapo hatabadilika kiutendaji kwa kufanya kazi za kisiasa badala ya kuhudumia umma wote bila kujali tofauti za kiitikadi kisiasa,” alisema Golugwa.
Katika mkakati wake, Chadema kimetishia kumburuta mahakamani Mulongo kwa tuhuma za kuzusha uongo na kumtishia Lema kwa maneno makali.
“Mawakili wetu wanaendelea na utaratibu wa kufungua kesi ya kumshtaki mkuu wa mkoa kwa kosa la kumtishia kwa maneno makali Lema na pia kutoa maneno ya uzushi, upotoshaji na uongo,”alisema Golugwa.
Chadema pia walisema askari polisi waliomkamata Lema hawakuwa na kibali cha ofisi ya Spika wala hati ya kukamata kutoka kwa ofisa wa jeshi hilo kama sheria inavyoelekeza.
CCM Arusha
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.

Wafu wanavyofukuliwa, kisha kuzikwa wapya

 Siku zote tunaamini kuwa mtu anapofariki hupumzika kwa amani, lakini siku hizi wafu hao hawapumziki tena kwa amani, bali huamshwa, kisha, wafu wengine kushika nafasi zao.
Ni kama vile muda wa marehemu hao kukaa kaburini umekwisha hivyo, nafasi zao zinatakiwa kutumiwa na wengine kutokana na uhaba wa maeneo ya kuzikia.
Maeneo mengi ya kuzikia katika Jiji la Dar es Salaam, hasa yale maarufu kama Kinondoni, Sinza, Temeke na Kisutu yanapendwa zaidi na watu na sasa yamefurika.
Kujaa kwa maeneo haya ya kuzikia kumesababisha makaburi ya watu wengine, kufukuliwa kisha kutumika kuzikia miili mingine.
Hata hivyo, makaburi ambayo hufukuliwa ni yale ambayo hayajajengewa, yametelekezwa, hayana kitu chochote cha kuonyesha kuwa kuna kaburi pale au mengine hayana alama kama misalaba au imeondolewa.
Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Kaiohela anasema kuwa anafahamu kwamba makaburi hayo yamejaa, lakini hakutaka kuzungumza zaidi akitoa ahadi kuwa siku ya Jumatatu atalifikisha suala hilo kwa wahusika wakuu.
Katika makaburi ya Temeke Chang’ombe, Mwananchi Jumapili lilishuhudia makaburi yakiwa yamesongamana kiasi ambacho ni vigumu mtu kupata nafasi ya kuweka mguu.
Mlinzi wa makaburi hayo, Athuman Mtembwe anasema kutokana na ufinyu wa nafasi katika makaburi hayo, makaburi ambayo hayana alama yoyote ni rahisi kufukuliwa na kuzikiwa kwa mara nyingine.
“Mimi kama mlinzi wa eneo hili ninaweza kukutafutia sehemu ambayo unaweza kuchimba kaburi, lakini kama hufahamu utafukua tu maiti nyingine,” anasema
Anasema kuwa mara kwa mara watu wanaokuja kuchimba makaburi ili kuzika ndugu zao, wamekuwa wakifukua miili ya watu wengine ambayo makaburi yao hayakuwa na alama yoyote.
“Ni kawaida, mchimba kaburi anafukua, anakuta mifupa, anaiweka pembeni au anaizika katika shimo dogo…kisha anaendelea na taratibu za kuzika mwili mwingine,” anaeleza.
Lakini Mtembwe anasisitiza kuwa iwapo atachimba yeye, hawezi kufukua kaburi lililokwishatumika kwani anafahamu maeneo machache ambayo hayajatumika, ingawa ni finyu mno.
“Hapo uliposimama ni kaburi hapo ingawa wewe hujui,” anasema akimwambia mwandishi wa makala haya huku akimwonyesha kwa kidole kuwa aliposimama ingawa hakuna dalili ya kuwepo kwa kaburi, lakini lipo.
Mzee Mtembwe ambaye amekuwa mlinzi wa makaburi hayo kwa zaidi ya miaka 30, anaeleza kuwa siyo kwamba ardhi ya kuzikia hakuna kabisa, bali hali hiyo inatokana na tabia ya watu kupenda kuzika karibu au mahali ambapo ndugu wengine wamezikwa.
“Maeneo mengine ya kuzikia yametengwa, huko Yombo Buza na Tabata Segerea, lakini wanaoyatumia ni wale wanaoishi huko au ambao hawaoni umuhimu wa kuzikia hapa Temeke,” anasema.
Anasema imejengeka dhana kwa jamii kupenda kuzikia maeneo ya Sinza, Kinondoni au Temeke.
Anaisihi jamii kuwa inapomzika ndugu au rafiki, isikawie kujengea au kuweka alama ya kudumu, vinginevyo ni rahisi watu kutumia tena eneo hilo kwa kuzikia.
Hata hivyo, jitihada za gazeti hili za kuwatafuta wakurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Kinondoni na Ilala ili kuzungumzia adha hii hazikufanikiwa.
Lakini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecky Sadiki alisema anafahamu kuwa watu wengi wanapenda kutumia makaburi maarufu kama Kinondoni, Temeke na Sinza, licha ya maeneo hayo kujaa.
“Makaburi hayo yanapendelewa zaidi kwa sababu labda ya ukaribu au kukwepa gharama za usafirishaji. Lakini maeneo mapya ya kuzikia yapo,” anasema Sadiki.
Waliopoteza makaburi
Teddy Mmbaga mkazi wa Temeke anasema, makaburi ya ndugu zake wawili, yamepotea na eneo walipowazika, sasa wamezikwa watu wengine.
“Tunapakumbuka alizikwa hapa (anaonyesha chini ya mti) lakini sasa hivi amezikwa mtu mwingine,” anasema.
Monica Mlaponi, naye anasema amepoteza kaburi la dada yake ambaye alizikwa katika Makaburi ya Temeke mwaka 2005, lakini hivi sasa kaburi lake amezikwa mtu mwingine kabisa.
Mtembwe anasema kuwa makaburi yanayofukuliwa zaidi ni ya watoto wachanga akitaja mfano siku moja, mbili au wiki.

“Kwa vichanga wanavizika juu juu tu kisha wanafukia na wakimaliza hapo hawarudi tena na kaburi hilo huwa limesahaulika. Ndiyo maana yanafukuliwa na kutumika tena,” anasema.
Mwananchi Jumapili likiwa eneo hilo, wanaume watatu wanafika katika makaburi hayo wakiwa na maiti ya mtoto mchanga, wanachimba kaburi lisilozidi urefu wa futi nne, kisha wanakizika kichanga hicho na kuondoka.
Alama wanayoiweka ni tawi kubwa la mti ambalo limekatwa kutoka katika mti ulio karibu.
Makaburi ya Buruda
Si eneo hili tu ambalo makaburi yamekuwa yakizikiwa mara mbili au zaidi bali hata eneo la Mbagala Misheni maarufu kama Makaburi ya Buruda.
Eneo hili ambalo hata hivyo kwa sasa limefungwa kutokana na kujaa, uzikaji wake ulifanyika kwa mtindo huohuo wa kufukua la zamani na kuzikia marehemu wa sasa.
Seleman Mohamed au Keto, ambaye makazi yake yametazamana na eneo hilo anasema kabla ya kufungwa, watu walilazimisha kuzika hivyo hivyo kwa kutumia nafasi finyu waliyoiona, ambayo aghalabu huwa ni kaburi la zamani.
“Mara nyingi tu watu wamefukua mifupa hapa, lakini inakuwa siyo kazi rahisi kulifukia tena hilo kaburi bali wanaizika mifupa ile sehemu nyingine kisha wanamzika marehemu ‘mpya’,” anasema Keto.
Anasema kama taratibu za kisheria zisingefuatwa basi watu wangeendelea kuzika hapo hapo licha ya kujaa.
Mazindiko, vibaka makaburini
Mtembwe anasema katika miaka zaidi ya 30 aliyokuwa mlinzi wa Makaburi ya Temeke ameshuhudia mambo mengi ya ajabu makaburini hapo.
Anasema wapo watu ambao hufika kufanya mambo ya ajabu juu ya makaburi kutokana na imani za kishirikina.
“Wengine wanakuja kuzika vichwa vya kondoo, mbuzi au kuku. Wanafanya hivyo usiku wakati mimi sipo lakini ninajua,” anasema.
Anasema kuwa wakati mwingine anapofika eneo lake hilo la kazi, hukuta damu juu ya kaburi, nazi zilizovunjwa au mayai.
Mtembwe anaeleza kuwa baadhi yao huja mchana na humwomba kufanya matambiko katika makaburi.
“Mtu anakuja anaomba atumie kaburi la Kiislamu au la Kikristo, kuna mambo ya ajabu hapa,” anasimulia.
Si hivyo tu, bali vibaka nao wameyafanya maeneo hayo kuwa sehemu ya kujificha ili kunasa mitego yao.
Gazeti hili lilishuhudia maboksi na matambara mabovu yaliyotandikwa juu ya baadhi ya makaburi ikidhaniwa kutumiwa kwa kulaliwa na baadhi ya vibaka.
“Ni kweli wanalala juu ya makaburi, sasa kweli mtu mwenye akili timamu atalala juu ya makaburi?” anasema akihoji.
Mtembwe anasema, wanaolala juu ya makaburi usiku baadhi yao ni vibaka ambao huwavizia wapita njia usiku.
Anasisitiza kuwa wale wasiojengea makaburi watapoteza kumbukumbu ya ndugu zao na hata wakati Serikali itakapohamisha makaburi watakosa malipo.

CHADEMA KUMSHITAKI RC MKOA WA ARUSHA



Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Arusha (Chadema) kinafanya utaratibu wa kumfungulia mashitaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, dhidi ya kauli zake za uchochezi kwa chama hicho na vitisho kwa Mbunge Godbless Lema ambaye kwa sasa anashikiliwa na Polisi.

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Katibu wa chama hicho, Amani Golugwa, alisema tayari wameanza kufuata taratibu za kumfikisha kwenye vyombo vya sheria na karibu wanakamilisha kupitia wanasheria wao wa chama.

Golugwa alisema Mulongo amekuwa kikwazo kikubwa kwa kuwa si mara ya kwanza, kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Chadema na kumtuhumu Lema kwa uongo, hali ambayo hadi kwenye mauaji ya chuo cha Uhasibu ilijitokeza.

Alisema kutokana na hali hiyo hawawezi kupuuzia hali hiyo, kwasababu itazidi kuwaumiza na kubambikiwa kesi zisizo za kwao.

“Tunavyoongea mpaka sasa tayari tumeshawasiliana na wenzetu ambao ni wanasheria wa Chadema na tutamfikisha mahakamani huyu mkuu ili iwe fundisho kubwa... kauli zake za uchochezi na za kutupinga sisi zinatuchosha na mimi kama katibu naona amefilisika kisera na hata kimawazo, kwa kuwa kamwe siwezi kumfananisha hata na mtendaji wangu wa chama yoyote,” aliongeza Golugwa.

Akiongelea kesi inayomkabili Mbunge Lema, alisema kuwa mpaka sasa kesi hiyo haina mlalamikaji lakini vitisho alivyotoa mkuu huyo wa mkoa vinasema kuwa Lema kwa sasa hatabanduka na wala hatachomoka.

Alisema kupitia kwa mwanasheria wao wanajipanga kukabiliana na mkuu huyo wa mkoa.
Awali Wakili wa Mbunge Lema, Humprey Mtui, alisema anashangazwa na kitendo cha jeshi la polisi, kumvunjia heshima mbunge Lema.

Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria Lema angepaswa kuitwa na Polisi na kama angekataa angeweza kuchukuliwa sheria kama hiyo. 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Jumamosi, 27 Aprili 2013

CHAMA CHA CUF CHAHUSISHWA NA FUJO ZA LIWALE

 
MBUNGE wa Liwale, Faith Mitambo (CCM), amekishutumu Chama Cha Wananchi (CUF) kwamba ndicho kilichoasisi vurugu zilizotokea jimboni kwake. Mbunge huyo pia alilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti machafuko hayo na badala yake kuwaacha wafuasi wa chama hicho kufanya uharibifu wa mali za watu.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, katika vurugu hizo amepoteza nyumba zake mbili zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 100, huku wengine wakichomewa magari na maduka.

Akizungumza na MTANZANIA juzi kwa njia ya simu, Mitambo alisema vurugu hizo hazitokani na suala la stakabadhi ghalani pekee bali pia kuna siasa chafu ambazo zimeingizwa.

“Tatizo hili si la stakabadhi ghalani peke yake, CUF wamekuwa wakifanya mipango hii siku nyingi na ilikuwa wafanye maandamano April 15, mwaka huu.

“Lakini yalizuiliwa, leo hii yametokea yaliyotokea, lakini ni vyema wakafahamu kuwa ni complete unfair kwani kuchoma na kutuharibia mali zetu ni kutuonea.

“Ukiangalia mali zote zilizoharibiwa ni za viongozi wa CCM, mimi ni mbunge wa CCM, mwenyekiti wa CCM nyumba yake imechomwa na madiwani wa CCM.

“Viongozi mbalimbali wa CCM nyumba zao zimeharibiwa vibaya kwa moto, huu ni uonevu mkubwa ndiyo maana nasema tatizo sio korosho kuna siasa chafu ndani yake,” alisema Mitambo.

“Nilipopata taarifa hizo asubuhi juzi niliwasiliana na vyombo vya dola, RPC na OCD niliwapa taarifa mapema lakini hawakutoa msaada wowote hadi nyumba zetu zikateketezwa.

“Mimi nimesikitika kama vyombo vya dola unaweza kuwasiliana navyo vikashindwa kutoa msaada hadi kusababisha mali kuharibika ni tatizo kubwa,” alisema.

Alisema tatizo la stakabadhi ghalani wamekuwa wakilipigia kelele kila siku na wamekuwa wakikutana kwa lengo la kulipatia suluhu.

“Ni miezi saba sasa, kipindi chote tumepiga kelele kuomba Serikali ilifanyie kazi, wiki mbili zilizopita ndiyo wamenza kuuza korosho na kulipwa,” alisema.

POLISI WARUKA UKUTA KUMKAMATA MBUNGE LEMA


Maofisa wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.
Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo.
Walifika nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini walilazimika kusubiri hadi saa 9:10 walipomkamata Mbunge huyo baada ya yeye mwenyewe kujisalimisha. Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba “anaweza kuhatarisha amani”.
Mashuhuda waliokuwa karibu na anakoishi Lema, eneo la Njiro Mwisho wa Lami, walisema polisi hao walifika wakiwa kwenye magari manne na kwamba ili kuchunguza ndani ya uzio wa nyumba yake, walipanda juu ya mabega ya wenzao huku wakielekeza mitutu ya bunduki tayari kukabiliana na lolote ambalo lingejitokeza.
Baada ya kuchungulia baadhi yao walitumbukia ndani ya uzio na kwenda kusimama mbele ya milango na madirisha ya nyumba ya Lema na huku nyuma wengine walipanda tena kwenye mabega ya wenzao kuendelea kuweka ulinzi kwa walioingia ndani.
Askari hao wanadaiwa kwamba waliwataka walinzi wa nyumba hiyo iliyopo karibu na Chuo cha Ufundi Veta, kuwafungulia mlango, lakini walinzi hao walikataa hivyo kuzua mabishano makali.
Kutokana na mabishano hayo, Lema aliyekuwa ndani amelala alishtuka na kuanza kufuatilia na kubaini kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake hiyo. Mke wa Lema, Neema alimpigia simu Katibu wa Wilaya wa Chadema, Aman Golugwa kumwarifu kuhusu uwepo wa watu walioruka ukuta.
Golugwa jana alithibitisha kupokea simu ya mke wa Lema na kwamba alipopata taarifa hizo alimwarifu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Arusha, Camillius Wambura ambaye baadaye alimuahidi kwamba angefuatilia suala hilo.
“Baadaye alithibitisha kuwapo kwa polisi waliotumwa kwa ajili ya kumkamata Lema lakini akasema amewapa maelekezo ya kufuata taratibu za kawaida,”alisema Golugwa na kuongeza:“Baada ya hapo, wale askari waliokuwa wameruka ukuta walitoka nje ya uzio”.
Habari zinasema wakati baadhi ya askari wanaruka ukuta, wengine walibaki nje wakizingira uzio wa nyumba ya Lema huku wakiwazuia viongozi wa Chadema waliokuwa eneo hilo kusogea.
Kukamatwa kwa Lema katika mtindo wa aina yake kumefanywa saa chache tangu alipotoa kauli ya kukataa kujisalimisha polisi, kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo. Mulongo aliagiza Lema akamatwe kwa tuhuma kwamba alichochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walimzomea Mulongo na kurushia mawe msafara wake wakati alipokwenda kusikiliza malalamiko yao yaliyotokana na kuuawa kwa mwanafunzi mwenzao, Henry Kago (22) ambaye alichomwa kisu na watu wasiofahamika wakati anatoka kujisomea saa 4:00 usiku.
“Kuna taratibu za kumwita mbunge polisi, wanaweza kunipigia simu au kuwasiliana na Spika, lakini siyo kutumia utaratibu huu wa kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mimi natakiwa kukamatwa wakati najua sina kosa,”alisema Lema.
Kauli ya Lema
Akizungumza na Mwananchi kabla ya kujisalimisha kwa askari hao juzi usiku, Lema alisema alishangaa polisi kuvamia nyumba yake usiku wakati walikuwa na uwezo wa kumpigia simu na kumwita.
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi wangu na mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,” alisema Lema. Hata hivyo, baada ya muda idadi kubwa ya wafuasi wa Chadema, walijitokeza na kuzingira nyumba ya Lema, hali ambayo ilianza kutishia uvunjifu wa amani.
Golugwa ndiye aliyefanya majadiliano na OCD Muroto kuhusu namna ya kufanikisha mbunge huyo kujisamilisha baada ya kuwa amewasiliana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na ilipotimu saa 9:10 usiku Lema alijisamilisha baada ya kuhakikishiwa usalama wake.
Mmoja wa viongozi wa Chadema, Calist Lazaro alisema walikubali Lema aende polisi, baada ya majadiliano na viongozi wa juu ya chama hicho.
“Tulitaka Polisi watuhakikishie usalama wake na pia tulitaka suala hili lifanyike kwa uwazi kwani siyo jambo la kawaida mbunge kuvamiwa na polisi usiku kama jambazi,”alisema Lazaro.
Polisi wanena
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas jana, alikiri maofisa wa jeshi hilo kumkamata mbunge huyo juzi usiku na hadi jana mchana alikuwa bado yupo rumande.
“Ni kweli tupo naye hapa polisi, anasubiri kuhojiwa kutokana na tuhuma za uchochezi katika Chuo cha Uhasibu Arusha,”alisema Kamanda Sabas. Alisema uamuzi wa kuendelea kumshikilia au kumwachia, utatolewa baada ya kukamilika mahojiano.
Mapema wakili wa Lema, Hamphrey Mtui akizungumza na Mwananchi nje ya kituo kikuu cha polisi, alisema bado alikuwa hajaruhusiwa kuonana na mteja wake .
“Bado tunasubiri polisi wamtoe na wakati wa kuchukua maelezo yake ndiyo wameniambia wataniita,” alisema Mtui. Baadaye Lema alihojiwa lakini alikataliwa kupewa dhamana.
Taarifa za kukamatwa kwa Lema zilianza kusambaa juzi saa sita kasorobo usiku na ilipofika jana asubuhi tayari tukio hilo lilikuwa limeishateka mijadala ya mitandao ya kijamii.
Mijadala hiyo iliambatana na mkanda wa Video wa Lema wakati akizungumza na wananfunzi wa IAA.

Ijumaa, 26 Aprili 2013

Lema: RC kanitumia ujumbe wa vitisho



Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”
Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”
Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”
Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”
kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”
Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”
Alisema Mbunge huyo, anajua kazi ambayo, ilifanya chuo cha uhasibu na ndiyo sababu anajificha... “Alifanya kazi yake nikazomewa, kama ningetaka kutumia madaraka yangu asingekuwa salama … nadhani Lema anahitaji kusaidiwa ili abadilike.”
Kuhusu madai ya kujificha, Lema alisema haitajisalimisha polisi licha ya Mulongo kuagiza akamatwe kwa kuwa kuna taratibu za kufuatwa polisi inapomhitaji mbunge ambaye amechaguliwa na watu.
Alisema kama polisi wanamuhitaji, wanapaswa kumuita na pia kuwasiliana na Ofisi ya Spika wa Bunge.
“Naomba ieleweke kuwa mimi sijawakimbia polisi, siogopi kesi na wala siogopi jela nitaendelea na shughuli zangu waje kunikamata barabarani,” alisema Lema.
Akizungumzia tukio la juzi, Lema alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu kwa kukosa weledi wa kuzungumza na wanafunzi wenye majonzi.
Alisema alikwenda chuoni hapo baada ya kuitwa na wanafunzi na kabla ya kuzungumza, alikutana na uongozi wa chuo, akiwamo Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha.
“OCD Arusha aulizwe kazi ambayo nilifanya kutuliza hasira za wanafunzi na tutasambaza DVD zaidi ya 3,000 kwa wakazi wa Arusha kujionea tukio hili ambalo sasa limebadilishwa na kuwa la kisiasa,” alisema Lema.
Mwanafunzi, Henry Kago(22) aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana na kusababisha wanafunzi kucharuka chuoni hapo anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Iringa kwa mazishi.

Alhamisi, 25 Aprili 2013

HATUA TANO MUHIMU KUELEKEA MAFANIKIO (High five to success)

 
Maranyingi katika maisha yetu ya kilasiku tumesikia sana maneno kama “nipe tano” “chukua tano” maneno haya yamekuwa maarufu sana na katika mazingira tofauti maneno haya yamekuwa yakiashiria ushindi, au hali ya mafanikio au furaha baada ya hali fulani. Vivyo hivyo katika maisha yetu ya kutafuta kufanikiwa katika yaleyote tunayoyafanya kilasiku viko vitu au ziko hatua ambazo huwa zinatulazimu kuzijua au kuzipitia kama kweli tunamaanisha na tunayadhamiria hayo mafanikio tunayoyatafuta. Ni ukweli kwamba watu wengi hutamani sana mafanikio na kuyazungumzia sana katika maneno yao ya kilasiku lakini kwa bahati mbaya hawajawahi kuyaishi mafanikio hayo kwasababu ya kutokuwa na dhamira madhubuti katika kuyaelekea mafanikio hayo. Kama ambavyo tunaposema “high five” tunagonga mikono yetu na vidole vyetu vitano vikiwa vimefunguka kuashiria ushindi basi vivyohivyo nitajaribu kugusia hatua tano au vitu vitano vitakavyokusaidia kugonga mkono wa “ high five” baada ya kuyafikia mafanikio yako. Kwakifupi vitu hivyo ni, Uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyo navyo ndani yako, uwezo wa kusimama au kuwa na msimamo, uwezo wa kupiga hatua, uwezo wakujitengenezea sura ya maisha yako, na uwezo wa kuyaongoza maisha yako. Fuatana na mimi katika kuzichambua hatua hizi hapa chini.
1.      1. Kuwa na uwezo binafsi wa kuvikagua vile ulivyonavyo ndani yako (Take a stock)
Katika maisha yetu ya kilasiku hatunabudi kujifunza namna ya kujikagua sisi wenyewe, kuvikagua vile tulivyonavyo ndani yetu kwasababu ni ukweli kwamba pasipo kujikagua sisi wenyewe basi hatutaweza kuyatambua mapungufu tuliyonayo na kama hatutoyatambua mapungufu tuliyonayo basi mapungufu hayo hayatoweza kushuhulikiwa na kuondolewa, maana yake ni kwamba tutazidi kuishi na mapungufu yetu na hivyo kuathiri ufanisi wetu na mwisho wake mafanikio yetu kwa ujumla yataathirika. Labda nikupe mfano wa mtu mwenye duka, mara kwa mara mmiliki wa duka huwa na muda wa kuvikagua vitu au mali aliyonayo dukani (stock taking) na hapa huwezakutambua nini kimepungua, nini hakipo kabisa na nini kipo kwa wingi. Katika kujikagua sisi wenyewe sio tu tunapata uhakika wa vile tusivyonavyo (weaknesses) bali pia tunapata kufahamu vile tulivyonavyo kwa wingi (strengths). Jifunze kufanya tathmini ya maisha yako binafsi kila wakati, tathmini matendo yako ya kilasiku, maneno yako ya kilasiku, mitazamo yako (perceptions and attitudes) halafu angalia wapi kuna mapungufu na wapi kuna fursa zaidi). Baadhi ya mapungufu ambayo twaweza kuwa nayo katika maisha ni kama vile mapungufu ya kihisia (emotional gaps), mapungufu ya kiroho (spiritual gaps), mapungufu ya kiujuzi (skills gaps), mapungufu ya kifedha (financial gaps) na mengineyo mengi. Kumbuka, uzuri ni kwamba kila tunapoweza kuyatambua mapungufu haya tunaziona fursa za kuweza kuyashuhulikia.
2.    2.  Uwezo wa kuwa na msimamo (Take a stand)
Wengi wetu tumeshindwa kuyafikia malengo tuliyowahi kujiwekea kwasababu tu hatunamisimamo katika vile tunavyoviamini kwahiyo inakuwa rahisi kuyumbishwa na kupeperushwa na kila upepo unaokuja upande wetu. Ili kufikia mafanikio tunayoyatamani hatunabudi kuwa na misimamo fulani katika maisha. Naupenda msemo unaosema kama  huwezi kuwa na msimamo katika chochote basi utachukuliwa na chochote “He who stands for nothing will fall for anything”. Kama wewe ni kijana na huna msimamo katika chochote basi ni rahisi kujikuta unachukuliwa na vingine ikiwemo madawa ya kulevya, umalaya n.k. Kama wewe ni mfanyakazi na hauna msimamo katika baadhi ya mambo basi ni rahisi kujikuta unabebwa na mengi kama vile rushwa na ubadhilifu. Ni vema kufahamu kila wakati maishani kuwa kama hauna msimamo katika ufanisi basi utaangukia katika uzembe na kutowajibika, na kama hautakuwa na msimamo katika kuhakikisha unafanikiwa basi utaangukia katika umaskini.
Kusimamia kitu fulani  maanayake ni kuwa na nidhamu, kujua kanuni, na kukiheshimu kitu kile unachokisimamia. Kanuni na nidhamu hizi ndizo zinazotuongoza katika maisha yetu ya kilasiku katika kufikia kile tunachotamani. Amua mwenyewe ninini unasimamia na ni wapi unaiweka misimamo yako kwasababu vile tunavyoamua kuwa na misimamo navyo ndivyo vinavyosimama kama misingi katika maisha yetu.
  1. Uwezo wakupiga hatua (Take a step)
Yamkini unatamani sana kufanikiwa na kilasiku unaongelea sana mafanikio, ni vema kujua kwamba mafanikio yetu hayaji kwa kuyatamani sana au kuyaongelea sana bali katika uwezo binafsi wa kuamua kupiga hatua. Yawezekana uko katika chombo kizuri tu cha usafiri lakini utajikuta unapitwa na kila mtu, hata wale wenye vyombo vibovu vya usafiri nao watakupita kama utakuwa umekaa tu kwenye chombo chako pasipo kuruhusu mwendo. Chukua hatua kuelekea mustakabali wako, angalia mbele yako unaona nini? nini ambacho unakiona kwenye mustakabali wako? Nini ungetamani ukipate kwenye mustakabali wako? Anza kufanya kila kinachohusika ili kuiona hiyo ndoto yako ikiwa dhahiri. Anza kupiga hatua ya kwanza na hatua nyingine zitakuwa rahisi kufuatia. Kamwe usitishike na umbali unaouona kuelekea mustakabali wako, jinsi unavyopiga hatua ujasiri wako unafunguka na kukua, kumbuka kuwa kila hatua unayoipiga hatakama nindogo kiasi gani inakusogeza karibu na mustakabali wako. Usisahau tu kuwa ziko mbio unatakiwa kuzikimbia na uko ushindi unatakiwa kuushinda ilikufikia hapo unapotamani, kwahiyo piga hatua.
  1. Uwezo wa kujitengenezea sura ya maisha yako (Take a shape)
Katika maisha yetu ya kilasiku ni ama uamue kuitengeneza sura ya maisha yako au kuibomoa sura hiyo, wengine wetu maisha yetu hayajawahi kuwa na sura nzuri ya kuvutia, sisi wenyewe ndiyo wenyeuwezo wakuamua kuitengeneza sura hiyo kuwa vile tunataka iwe, ukiamua kukaa tu pasipo kufanya chochote basi umekusudia kwa dhamira halisi kuiharibu sura ya maisha yako mwenyewe. Ulimwengu waleo unabadilika kwa kasi sana, ili kuweza kubakia wenye maana na wenye umuhimu basi hatuna budi kuwezana na mabadiliko hayo. Kama hatutoweza kuyaweza mabadiliko ya karne hii basi mabadiliko hayo yatatuweza sisi (If you don’t manage change change will mismanage you). Fahamu dhahiri kwamba karne ya 21 haijaleta tu fursa bali na   changamoto tele.
Lazima tuweze na tuwe na ujuzi wa kufanya tabia zetu za kilasiku kuendana na mabadiliko haya, lazima kuwa kasi kama vile kasi ya mabadiliko ilivyo, lazima kuwa wenye uwezo wa kuendana na mazingira kwasababu ukijaribu kukakamaa na kutokubali mabadiliko (being rigid) katika enzi hizi basi lazima utavunjika. Chamsingi wote tujitahidi kufanya hata yale ambayo maranyingine hayaturidhishi sana, yale ambayo tunaona yanatugarimu zaidi na kutuminya zaidi, kumbuka mafanikio sio wakati wote yanakuja tukiwa tunayasubiria kwa kicheko bali maranyingine kwa kuumia (we must be willing to step out of our comfort zones)
  1. Uwezo wa kukikalia kiti na kuyaongoza maisha yako mwenyewe (Take a seat)
Ziko nyakati ambazo wengi wetu hatuwezi kufika tunapotamani kufika kwasababu dereva anayeendesha chombo chako sio wewe, wakati huohuo unafikiria kuelekea pale unapotamani wewe. Ningumu sana. Katika maisha kama kweli unaifahamu ndoto yako na unaiona kesho yako na unaitamani sana kuifikia basi amua kukaa kwenye kiti cha dereva wewe mwenyewe na kuendesha chombo kuelekea huko. Wengi wetu sio kwamba tumewakabidhi wengine udereva wa safari yetu kwa kujua bali kwa kutokujua, mara unaona muelekeo wa safari sio ule ulioutarajia, yamkini sasa dereva uliyemkabidhi kiti anakupeleka kwenye ndoto yake siyo yakwako tena. Sasa amuakuingia kwenye kiti cha dereva wewe mwenyewe, hayo ni maisha yako na siyo ya mwingine. Kamwe usiache furaha na mafanikio yako katika mikono ya wengine.  Kubali na kuwa tayari kubeba majukumu. Kama inatokea unafanya makosa basi usijitetee na kukwepa, kwasababu kujitetea na kukwepa yawezakuwa njia tu ya kuchomoka na siyo njia ya kuendelea mbele. Usiwalaumu wengine kwa madhaifu na kushindwa kwako, kwasababu kwa kufanya hivyo unaipoteza nguvu ya kukua.
Chukua tano!!!!
Acknowledgement: Dr John Tibane’s teachings.
Prepared by Chris Mauki
Social and counseling psychologist
PhD candidate, University of Pretoria
South Africa

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More