Alhamisi, 18 Aprili 2013

JE UNAZIJUA SHEREHE ZA KUOGA UCHI KATIKA MTO GANGES UKO INDIA

Waumini wa dini ya Kihindu wakienda kuoga ili kujitakasa na dhambi walizotenda

 Mamilioni ya Wahindu wakiwa wamejipaka majivu tayari kuingia mtoni kuoga
 Mamilioni ya wahumini wa madhehebu ya kihindu wakiwa katika foleni ya kuingia kuoga ili kujitakasa na dhambi zao

kina mama nao huchanganyika na wanaume wakati huo wa kutakasa dhambi zao kwa maji

 Kutokana na wingi wa watu, treni kama unavyoona zinakuwa zimepakia hadi dereva hapati pa kuangalizia. Kila penye upenyo panakaa mtu isipokuwa tu kwenye magurudumu
 Hii ndio hali halisi ya usafili wakati wa sherehe za kwenda katika mto ganges ili kusafishwa hdambi

ALLAHABAD, India, Mamilioni ya watu wa dini ya Hindu hufanya ibada yakusafishwa dhambi zao kwa  kuoga katika makutano ya mito mitatu ya Ganges, Yamuna na Saraswati inapokutana. Kwa mujibu wa Imani ya Kihindu, binadamu anakuwa ametenda dhambi nyingi katika mzunguko wa mwaka na hivyo anahitaji kutakaswa na dhambi zake. Waumini wanaume wanajipaka majivu kuanzia utosini hadi unyayo na mara nyingi wanakuwa uchi wa mnyama ingawa sikuhizi wengine wanapendelea kuvaa pajama, wanaingia kwenye mto huo na kuoga nakuamini kuwa wameondolewa dhambi zao zote na nuksi nyingine zote.

Hii ni sherehe kubwa na inayodumu muda mrefu kuliko zote duniani kwani inadumu kwa kipindi cha siku 55.

Mratibu mkuu wa sherehe hizo Mani Prasad Mishra amesema karibu watu milioni 3 huwa wanauzulia katika ibada ya sherehe hizo za kuoshwa dhambi.
 Zaidi ya watu milioni 110 hutarajiwa kuoga kwenye eneo hilo liitwalo SANGAM. Hili ni eneo ambapo makutano ya mito ya GANGES, YAMUNA NASARASWATI . Sikukuu hii inategemea mwonekano wa nyota zinazolandana angani. Baada ya nyota hizo kukaa katika mkao fulani basi wahindu wanaenda kuoga ili kujitakasa na madhambi yao na kuepuka kufa na kuzaliwa upya katika hali ya adhabu.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More