Jumatatu, 8 Aprili 2013

Marekani yachelewesha kombora la masafa


California. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imechelewesha jaribio la kombora la masafa marefu lililotarajiwa kufanywa wiki hii katika jimbo la California, wakati kukiwa na ongezeko la mvutano wa nyuklia na Korea Kaskazini.
Ofisa mmoja wa Wizara alisema Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel alipanga upya siku ya kufanywa jaribio la kombora hilo kwa jina Minuteman 3 litakalofanywa katika kambi ya jeshi la angani ya Vandenberg mwezi ujao.
Alisema kutokana na wasiwasi kuwa uzinduzi huo huenda ukachukuliwa na wengine kumaanisha kuwa Marekani inalenga kuuchochea hata zaidi mzozo unaoendelea kwa sasa na Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini, iliyoghadhabishwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa na majaribio ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini, ilitoa msururu wa vitisho vya kuanzisha vita vya nyuklia katika wiki chache zilizopita.
Tangazo hilo la Pentagon limefuatia ripoti kuwa Korea Kaskazini imeificha mizinga miwili ya masafa marefu ndani ya handaki karibu na viwanda vyake vya pwani ya Mashariki.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imehamisha makombora baadhi kwenye mwambao wake wa Mashariki tayari kwa mashambulizi dhidi ya Marekani, huku nchi hiyo inayotishiwa kushambuliwa ikisema inachukua tahadhari kutokana na vitisho hivyo.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Yonhap cha Korea Kaskazini kilimnukuu ofisa mmoja wa Serikali nchini humo, makombora mawili tayari yameshasafirishwa kwa treni na kuwekwa katika magari tayari kwa kushambulia.
Kwa upande wake Wizara ya Ulinzi ambayo ilithibitisha kupelekwa kwa kombora la kwanza ilikataa kutoa maoni yake juu ya habari za hivi karibuni kwamba makombora mengine yamesafirishwa Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More