Jumamosi, 13 Aprili 2013

super star kim kumaliza mambo mahakamani

Kim Kardashian, akiwa amezungukwa na usalama mzito, alionekana mahakamani leo asubuhi huko Los Angeles akisikiliza shauri lake la talaka kwa mchezaji wa NBA Kris Humphries.

Humphries, hakuonekana mahakamani wakati kesi hiyo iliyokuwa ikiwakilishwa na wanasheria watatu.
AP anasema, Kim ambaye anatarajia mtoto majira haya na mpenzi Kanye West, aliingia mahakamani kupitia mlango wa nyuma. Nywele zake akuwa amefunga nyuma katika style ya ponytail huku akiwa amekunja mikono yake wakati akimsikiliza kwa makini Jaji Hank Goldberg wakati akiuelezea umati wa waandishi wa habari kuwa fursa ya kusikiliza ingefungwa.

Kama Kim na Kris hawatafikia makubaliano, Kesi imepangwa tarehe 6 mei. Wote wanatarajiwa kushuhudia katika kesi hiyo, kama ni mama wa Kim, Kris Jenner.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More