Jumatatu, 20 Mei 2013

WAYNE NA COLEEN ROONEY WAPATA MTOTO WA KIUME, WAMPA JINA LA KLAY!!

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United, “Mashetani wekundu” na mabingwa wa ligi kuu soka England, Wayne Rooney amepata mtoto wa pili usiku wa kuamkia leo.

Mke wake mpendawa Coleen amejifungua mtoto wa kiume na wamempatia jina la Klay.

Coleen alipatwa na uchungu jumamosi usiku wiki iliyopita na kumsababisha Rooney ashindwe kusafiri na timu yake kuifuata West Bromwich katika kipute cha kufunga pazia la ligi kuu England ambapo mechi hiyo ilimazika kwa sare ya kufungana mabao 5-5 na kumuaga rasmi kocha wa klabu hiyo Kibabu Sir Alex Ferguson.

Rooney alitangaza taarifa hiyo katika mtandao wake wa Twita akiwaambia wafuasi wake zaidi ya milioni 6 kuwa amefurahi kupata mtoto mzuri wa kiume Klay Anthony Rooney, huku mama yake na mtoto Klay wakiwa wazima.

Mtoto wa kwanza wa Rooney ana miaka mitatu mpaka sasa na anaitwa Kai, hivyo sasa amekuwa baba wa watoto wawili. Hongera sana Rooney.

Wakati huo kuna taarifa kuwa kocha mpya wa United, David Moyes anatarajia kukutana muda wowote na Rooney ili kuzungumzia hatima yake klabuni hapo msimu ujao.

Hivi karibuni Rooney na Ferguson hawakuwa katika maelewano mazuri mpaka nyota huyo aliomba kuihama klabu yake hiyo ambayo imempa jina kubwa zaidi duniani.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More