Ijumaa, 24 Mei 2013

Nini Siri ya mafanikio ya Bayern na Dortumund Kutinga Fainali UEFA? Bofya hapa uone siri ya mafanikio

Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borussia Dortmund
Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali.
Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.
Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Kocha wa Bayern Munich
Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.
Kocha wa Borussia Dortmund
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More