Jumapili, 5 Mei 2013

KANISA KATOLIKI LALIPULIWA KWA BOMU ARUSHA WAKATI IBADA YA UZINDUZI WA KANISA HILO IKIWA INAENDELEA


 

Taarifa  zilizotufikia  hivi  punde  ni  kwamba  bomu  limelipuka  katika  kanisa  katoliki, parokia  mpya  ya Olasiti  iliyokuwa  inazinduliwa  leo  jijini  arusha.
Bomu  hilo  limelipuka  wakati  waumini  wa  kanisa  hilo  wa  wakijiandaa  na  misa  ya  uzinduzi  wa  parokia  hiyo.
Mpaka  sasa  haijajulikana  idadi  kamili  ya  watu  waliojeruhiwa  ama  kupoteza  maisha  lakini taarifa  za  awali  zinasema  kuwa  baadhi  ya  majeruhi  wamekimbizwa  hospitali

Chanzo  cha  mlipuko  huo  inasemekana   kuwa  kuna  gari  ndogo  ilifika  kanisani  hapo  na  kusimama....

Baadae  alishuka  mtu  aliyekuwa  amevalia  vazi  mithili  ya  kanzu  na  kurusha  kitu  kuelekea  kanisani  ambacho  ndicho  kilichosababisha  mlipuko  huo..
Mgeni rasmi   katika  uzinduzi   huo  alikuwa  ni   balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo  baada  ya kunusurika  katika  mlipuko huo

Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )

Kanisa lililolipuliwa na bomu Parokia ya Olasiti kama linavyoonekana

  Baadhi ya majeruhi waliokumbwa na zahma hilo la mlipuko wa Bomu walipokuwa katika ibada ya jumapili
                                         Askari wa kutuliza ghasi wakiwa eneo la tukio la kanisa


0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More