Alhamisi, 2 Mei 2013

MTOTO MWENYE VIUNGO VYA AJABU AZALIWA MPANDA MKOANI KATAVI

Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke aitwaye Johari Raphael ( 35) mkazi wa mtaa wa Makanyagio Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi amejifungua mtoto wa kiume mwenye viungo vya ajabu utofauti na banadamu wa kawaida.

Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpanda Naibu Mkongwa aliwaambia waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuwa mwanamke huyo alijifungua mtoto wa ajabu ambae alikuwa na kichwa kikubwa kama cha mtu mwenye umri mkubwa huku mikono na miguu yake ikiwa mifupi mfano wa pingili za miwa.

Dkt Mkongwa alieleza kuwa mwanamke huyo alijifungua mtoto mwenye uzito wa kilo nne na nusu(4.5) hata hivyo alifariki dunia muda mfupi baada ya mama yake kujifungua kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida katika hospitali hiyo.

Madaktari waliamua kumfanyia upasuaji baada ya kupata maelezo kutoka kwa mama huyo alipoeleza kuwa huo ulikuwa ni uzao wake wa tano na kati ya zao hizo amekuwamara hizo akijifungua kwa shida hali iliyo pelekea kujifungua watoto wawili wakiwa wameisha kufa.

Dkt Mkongwa akifafanua zaidi alieleza kuwa baada ya kupata historia ya mama huyo waliamua kumfanyi a uchunguzi na walipobaini kuwa mama huyo hawezi kijifungua kwa njia ya kawaida kutokana na ukubwa wa kichwa alicho kuwa nacho mtoto ambacho mwanamke yoyo hawezi kujifunga kwa njia ya kawaida

Alisema kutokana na hari hiyo madakitari wa waliamua kumfanyia upasuaji na ndipo mtoto huyo wa kiume alipotolewa na alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa

Kwa upande wake muuguzi mkuu wa hospital hiyo ya wilaya ya Mpanda Elexzanda Kasagula alisema kuwa mwanamke huyo alifikishwa katika hospital hiyo hapo juzi na kulazwa katika wodi ya wazazi baada ya kuonekana muda wake wa kujifungua umefika

Alieleza hali ya Johari ambae amelazwa katika wodi ya wazazi inaendelea vizuri na wanasubiriwa ndugu zake ili wakabidhiwe mwili wamarehemu kichanga hicho kwa ajiri ya mazishi

Kasagula alisema hili ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa kuzaliwa watoto wa ajabu kwani miezi mitatu iliyo pita alizaliwa mtoto huku utumbo ukiwa nje juu tumbo

CHANZO: Full shangwe

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More