Jumatano, 22 Mei 2013

Mtwara Kimenuka: Fujo mtindo mmoja amani hakuna Bofya hapa ujionee mwenyewe

  • Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 
  • Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 
  • Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
  • Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
  • Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
  •  Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
  • Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
  • Matairi  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto   wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
  • Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi
  • Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
  • Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia ovyo ovyo.
  • watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia
  • Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .
  •  Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
  • Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.
  • Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.
  • Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
  • Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.
  • Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
  • Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
  • Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
  • Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.
  • Kesho inaendelea tena kwa siku ya pili.  
  • Serikali  isipoangalia inaweza ikasababisha "Uprising" maeneo mengine ya nchi.


HALI YA MTWARA MAENEO YA NKANALEDI MAGOMENI




0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More