Jumanne, 7 Mei 2013

CHANZO CHA KIFO MFANYABIASHARA KARIAKOO CHAGUNDULIKA


Mwili wa Costa Shirima baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya tisa katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Mtaa wa Mchikichini, jijini Dar

CHANZO cha kifo cha mfanyabiashara maarufu Costa Shirima,47,  aliyejirusha kutoka ghorofa ya tisa hadi chini katika Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo jijini Dar  kimegundulika, Uwazi lina mkanda mzima.
Kifo cha mfanyabiashara huyo ambacho awali kilikuwa na utata, gazeti hili lilifuatilia mpaka  nyumbani kwake Kimara, Wilaya  ya Kinondoni ili kutaka kujua ni kitu gani kilicho mkera marehemu hadi kufikia uamuzi mgumu wa kufupisha maisha yake kwa kujirusha.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwa marehemu, mtoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charles Shirima ambaye alikuwa naye siku chache kabla ya mauti kumfika baba yake alikuwa na haya ya kusema.
“Hatukuamini kama  baba angeweza kuchukua maamuzi hayo magumu kulingana na ratiba yake ya shughuli zake za kibiashara ambapo hivi karibuni alipanga kusafiri kwenda  nchini China  saa kumi jioni  siku ambayo alijirisha kwa siku hiyo aliyojiua majira ya saa 12.45 mchana
“Tunaamini kwamba baba amekufa kutoka na maralia kali iliyopanda kichwani kwani wiki moja kbala ya mauti kumfika alikuwa na presha ya juu sana na na mararilia kali iliyosababisha kutapika na kuharisha kwa kiwango kikubwa kitendo kilichosababisha  tumchukua  na kumpeleka katika Hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam
“Baba alilazwa kwa muda wa siku mbili akaanza kupata unafuu,wakati huo  tulikuwa naye hospitalini akiwa akizungumzia  kuhusina na sdhughuli zake za kibiashara na alitaamani aende kuzishughulikia pamoja  kuwa alikuwa anaumwa, tulimshauri asubiri afya yake itengamae
“Daktari alimshauri  baba alisifanye shughulli yeyote bali akapumzike nyumbani hadi pale afya yake itakapotengamaa,hata hivyo  siku hiyo ya kifo chake ambayo ilibidi asafiri china  na teyari alikuwa na tiketi ya ndege, alimwambia mdogo wake aitwaye Albart Shirima kuwa anajisikia vibaya ambapo mdogo wake huyo alishauri asisafiri hata hivyo hakujisikia kuupokea ushari huo, aliamua kwenda Concord Hoteli alionekana kama mtu mwenye wasiwasi,alipofika huko aliwashangaza wahudumu kule Hotelini  kwa alikuwa ni mtu ambaye hakutulia
“ Kutokana na hali aliyokuwa nayo hotelini hapo wahudumu walimuliza anachokihangaiki ili waweze kumsaidia lakini alisema yeye alikwenda kuangalia ukumbi kwa ajili ya shughuli za harusi ambapo alielezwa ukumbi upo gorofa ya kumi.
“Baadaye  mmoja wa wahudumiu alimuona akiwa katika hali isiyokuwa ya kawaida akiwa anahangaika hangaika  huku akiww anafanya mawasiliano na siku yake ya kiganjani ambapo aliulizwa kuwa wamsaidie nini , yeye alijibu shida kubwa ni ukumbi
“Kwa mujibu wa wahudumu hao walieleza kuwa walimuacha akiwa anaongea na siku lakini baada ya muda si mrefu walikia kishindo mithili ya bomu, baadaye waligundua kuwa Shirima tayari ameisha dondoka  na kuangukia teksi iliyokuwa amepaki jirani na Hoteli hiyo.
“Sisi tunaamini kuwa baba amekufa kutokana na Maralia kali iliyompanda kichwani na si vinginenevyo na teyari kuna mengi yamesemwa , kwa sabau baba yetu huyo katika maisha  yake yote hatujawahi kusikia akitueleza kitu kinachomukwaza,ambacho  kingeweza kumfanya kufiki uwamuzi huo wa kujiua alisema” mtoto huyo
Baadhi ya wafanyabiahara waliopo karibu na hoteli hiyo katika maelezo yao walisema kuwa wamesikitishwa sana  na kifo cha mfanyabiashara huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kitokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa jeshi lake linaendelea na uchunguzi.
Source: Global publishers

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More