Jumanne, 21 Mei 2013

MSIWAUE WAPENZI WA JINSIA MOJA. RAIS MSEVENI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja
 
Katika matamshi yake ya kwanza hadharani, kuhusu muswada huo, Rais Museveni amekariri kuwa suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kupewa nafasi kukita mizizi.
Muswada wa awali uliowasilishwa katika bunge la Uganda, ulipendekeza adhabu ya kifo kwa wale watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini kipengele hicho kimefutwa katika muswada mpya.
Katiba ya Uganda kwa sasa inaharamisha mapenzi ya jinsia moja.

Serikali imekana kuhusika na mswada huo

Mwandishi wa Uingereza aliyekamatwa kwa kuandika mchezo kuhusu hatma ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda
Mwandishi wa BBC mjini Kampala, anasema serikali ya nchi hiyo imesema kuwa mswada huo uliwasilishwa na mbunge na wala sio muswada wa serikali.
Katika hotuba yake wakati wa kuapishwa kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Uganda Rais Museveni, alijiepusha kuupinga au kuunga mkono muswada huo.
Rais alisema, ''ikiwa kuna watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, hatutawaua au kuwanyanyasa lakini suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kuhimizwa katika jamii''
''Hatuwezi kukubali mapenzi ya jinsia moja kupewa msisitizo zaidi katika jamii kana kwamba ni jambo nzuri'' aliongeza rais Museveni.
Mawaziri wamewaonya wabunge kuwa ikiwa watapitisha muswada huo, basi kutakuwa na athari kubwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na jamii ya kimataifa.
Mataifa ya Magharibi yamelaani muswada huo na wametishia kusitisha misaada kwa Uganda ikiwa itapitishwa na bunge la nchi hiyo.
Spika wa bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amesema muswada huo utapitishwa kama zawadi ya Krismasi kwa mawakili wake

0 maoni:

Chapisha Maoni

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More