Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Alhamisi, 25 Aprili 2013

KUELEKEA UCHAGUZI 2015 MBINU MPYA HADHARANI BAINA YA KAMBI HASIMU

 



















ATIKA hali inayooshesha kupamba moto kwa harakati za kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), makundi ndani ya chama hicho yameanza kuungana.
Mbali ya kuungana kwa makundi, pia wale wote wanaotajwa kuwania kuteuliwa, macho na nyoyo zao vimeelekezwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ambaye nguvu aliyonayo ndani ya vikao vya uteuzi inatarajiwa kutumika kumpata mgombea urais.
Ingawaje viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakipinga mjadala kuhusu mgombea urais au Rais ajaye ndani ya chama hicho kikongwe nchini, lakini mjadala huo unatajwa kufunika hata ile mijadala muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Uchunguzi wa Rai umebaini kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ameanza ‘kurudisha majeshi’, na anatajwa kumuunga mkono Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye anatajwa kuwa ‘safi’, mtu asiye na kikwazo mbele ya Rais Kikwete.

“Hali inavyoonekana sasa, Membe anaelekea kuungana na kambi ya Dk. Nchimbi, na si yeye pekee, wale wote ambao wanampinga Lowassa lakini wanajua hawana kura ndani ya CCM, wanaanza kumuunga mkono Nchimbi.

“Lengo kubwa hapa ni kutengeneza mgombea mmoja mwenye nguvu kubwa ili kumkabili Lowassa ambaye anatajwa kuwa na nguvu kubwa zaidi ndani ya chama katika ngazi zote.

“Katika hao, yumo Waziri Samuel Sitta, Dk. Harrison Mwakyembe na watu wao, lakini vile vile wanasahau uhusiano mzuri na kuheshimiana kati ya Lowassa na Dk. Nchimbi.

“Pia tetesi za kuwapo mpango wa kulikata jina la Lowassa katika ngazi ya Kamati Kuu lisirudishwe kwenye Mkutano Mkuu ambako anadaiwa kukubalika kuliko wagombea wengine, kunatajwa kuwa moja ya sababu za makundi kuungana,” alisema mchambuzi mmoja wa mambo ya siasa nchini.

Mgombea mwingine anayetajwa kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM 2015, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira, ambaye tofauti na wagombea wengine, yeye hana kundi wala makundi.

Kutokana na kutokuwa na makundi, wachunguzi wa mambo wanasema haitakuwa rahisi jina lake kukwama katika ngazi ya Kamati Kuu, hivyo uwezekano wa jina lake kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu kuchuana na wagombea wengine ni mkubwa.

“Huyu Mzee ana advantage moja kubwa, Kanda ya Ziwa inatajwa kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura tofauti na maeneo mengi, na ni katika kanda hiyo hiyo Lowassa anaungwa mkono sana.

“Kama CCM wataamua kulikata jina la Lowassa, kuna uwezekano mkubwa sana kwa wana-CCM waliokuwa wakimuunga mkono kuhamishia kura zao kwa Wasira, na kumchagua,” alisema mchambuzi huyo.

Wakati hali ikiwa hivyo, pia imethibitika vigogo wa chama hicho wakiwamo wale wa kundi la wanamtandao lililomwingiza Rais Kikwete madarakani mwaka 2005 hawaaminiani katika harakati za kugombea urais kupitia CCM.

Uchunguzi unaonyesha vigogo wa CCM kutoka kambi zote wamekuwa wakiendesha kampeni za chini kwa chini kwa ajili ya kujiimarisha na kisha kuweza kuteuliwa kugombea kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu 2015.

Taarifa zinaonyesha kwamba hata baadhi ya vigogo wanaosadikiwa kuwa kundi moja sasa hawaaminiani jambo ambalo linaashiria kuwa vita ya urais CCM inapamba moto siku hadi siku.

Wakati wa vikao vyake vya juu vilivyomalizika Novemba 24 mwaka jana mjini Dodoma, CCM kilipokea na kupitisha taarifa ya hali ya siasa ambayo kimsingi ilibainisha kuwa hali ya siasa ndani ya chama si shwari, kutokana baadhi ya viongozi kupigana vikumbo kuwania madaraka.

Katika taarifa hiyo, CCM kilisema chanzo kikubwa cha migawanyiko ndani ya chama hicho ni harakati za kugombea urais mwaka 2015.

Hata hivyo, wimbi hilo la urais limeendelea kutikisa kambi ya wanamtandao ambayo taarifa za ndani zinasema huenda suala la urais likaibua mtafaruku mkubwa siku zijazo, hivyo kutoa mwanya kwa kundi jingine kuibuka kidedea.

“Kuna hali ya kutoaminiana ndani ya CCM, kila kundi sasa liko mstari wa mbele kujijega ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutoa mgombea urais.

“Hata ndani ya kundi la mtandao ambalo ndilo lenye nguvu kwa sasa wakubwa hawaaminiani,” alisema mtoa habari mmoja kutoka kundi la mmoja wa kiongozi anayetajwa kutaka kuwania urais ndani ya CCM.
Chanzo: gazeti la rai

Jumatano, 24 Aprili 2013

MAMA ZITTO AVAMIWA NA WATU WALIOTAKA KUMUHUA

 







SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
(CHADEMA), Zitto Kabwe, amenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakiwa na silaha za moto.
Habari zilizolifikia MTANZANIA Jumatano kutoka kwa watu walio karibu na mama huyo zilieleza kuwa, vijana hao walifanikiwa kumfikia akiwa katika sebule ya nyumbani kwake na kumuelekezea bastola kichwani, huku wakimlazimisha awakabidhi baadhi ya vifaa vyake vya kufanyia kazi na simu yake ya kiganjani.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, tukio hilo lilitokea Ijumaa ya Aprili 19, majira ya saa moja na nusu asubuhi.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu tukio hilo, mama yake Zitto alisema ni kweli lilitokea na amekwisharipoti katika kituo cha Polisi cha Buguruni.

Mama Zitto alisema siku kadhaa kabla ya tukio hilo alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa mwanachama wa Chadema wa Tawi la Tabata Relini na kumuomba msaada wa mifuko miwili ya saruji kwa ajili ya kukarabati jengo la ofisi yao.

Alisema alikubali kuwasaidia vijana hao kwa kuwataka wafike nyumbani kwake mapema siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, kwa sababu alikuwa na ratiba ngumu na ndefu siku hiyo.

“Nilikubaliana nao hivyo, bila kuwa na fikra kwamba wanaweza kuwa watu wabaya, hivyo walipokuja nyumbani kwangu baada ya kuruhusiwa na mlinzi niliwakaribisha ndani na kuwaeleza kuwa nitawapatia Sh 20,000 na Sh10,000 waongeze wenyewe.

“Lakini niliposimama kuelekea chumbani kuwachukulia kiasi hicho cha fedha, mmoja wao alitoa bastola na kunielekezea kichwani huku akieleza kuwa hawana shida na pesa, bali wanataka laptop yangu, flash na simu yangu ya mkononi kwa sababu zina mambo muhimu,” alisema mama Zitto.

Alieleza zaidi kuwa alipowauliza ni kwa nini wanataka vitu vyake hivyo, walieleza kuwa anajua sababu na hata siri yake ya kutumia nafasi yake ya uongozi wa chama cha walemavu kuzunguka nchi nzima akimnadi mwanaye Zitto kwa wana Chadema kuwa anafaa kuwa mwenyekiti wa chama hicho na rais wa Tanzania inafahamika.

“Nilijua kuwa ninakufa, sikuona haja ya kubishana nao sana, nikamwita dereva wangu, Mtana, alete simu yangu niliyokuwa nikiichaji chumbani na flash ili niwapatie, wakati akielekea kuvichukua aliwaona walivyokuwa wameniwekea bastola, akakimbia moja kwa moja chumbani akajifungia na kuanza kupiga kelele, wakatoka haraka wakakimbia,” alisema.

Alipoulizwa iwapo hawakupata upinzani wowote kutoka kwa mlinzi aliyekuwa getini au majirani walishtushwa na kelele za dereva wake, alisema wakati wanatoka geti lilikuwa wazi na mlinzi alikuwa akiosha gari nje, hivyo ilikuwa rahisi kutoka na gari lao na kutokomea.

Alisema anaweza kuwatambua watu hao akiwaona na kwamba mmoja wao si mgeni machoni mwake, kwa sababu aliwahi kumuona mkoani Tanga katika moja shughuli za chama hicho.

Mama Zitto alieleza zaidi kuwa kabla ya tukio hilo, amekuwa akiulizwa na baadhi ya wafuasi wa chama na hata watu wengine mahali anakopata fedha za kuzunguka mikoani kumnadi mwanaye, Zitto kwa ajili ya kugombea urais na uenyekiti wa chama.

Alisema kwa sababu ya kuhofia maswali ambayo amekuwa akiulizwa mara kwa mara, alimfikishia taarifa Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Ahmed Sagula, lakini katika hatua ambayo hakuitegemea, naye alimhoji mahali anakopata fedha za kuzunguka mikoani kumnadi Zitto, kabla ya kumuahidi kushughulikia malalamiko yake.

Sagula mwenyewe hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake kutopatikana kila ilipopigwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, naye hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni, mahali ambako Mama Zitto ameripoti tukio hilo naye hakuweza kupatikana.

BUNGE LA UFARANSA LAPITISHA SHERIA YA NDOA ZA JINSIA MOJA

Ni wale tu wanaopenda demokrasia ndio wako hapa, Rais wa bunge la Ufaransa alisikika akisema kwa satui ya ukali wakati wa kupiga kura, ambapo vurugu zilianza kutimka kutokana na kugawanyika wka mawazo ya wabunge hao, huku kinara wao akiwa amevalia nguo za rangi ya pink, rangi ambayo imeasiliwa na wanaopinga vitendo vya ushoga nchini humo.

Kura 331 za kukubali kati ya zile 225 za kupinga kupitisha kwa sheria hiyo ndizo zilizopelekea taifa la Ufaransa kuwa taifa la 14 duniani kuidhinisha vitendo hivyo, licha ya upinzani mkubwa ambao hutokea mara kwa mara nchini humo, ikiwemo leo bungeni.

Waziri wa haki nchini Ufaransa, Bi. Christiane Taubira akihutubia wabunge  wakati wa  maswali kwa serikali, kwenye baraza kuu jijini Paris.

Kutokana na kuchukizwa kwa baadhi ya wananchi kufuatia mpango wa serikali wa kuidhinisha muswada huo, hali ya usalama kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na tabia hizo wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa wanaharakati na wananchi wanaopinga, huku kinara mmojawapo wa kuunga mkono vitendo hivyo akipokea barua jumatatu iliyo na unga wa silaha (gun powder), ikiwa ni ishara ya kumtahadharisha aachane na mambo yake vinginevyo atadhuriwa.

Katika hatua nyingine, mshabiki mkubwa wa ndoa za jinsia moja nchini humo amekuwa waziri wa haki, Bi Taubira, ambaye amesema kuwa anaamini ndoa za kwanza kwanza zitakuwa mnamo mwezi juni, hali ambayo italeta hamasa na kubadilisha upeo wa baadhi ya watu wanaipinga vitendo hivyo.
"Naamini wale wanaopinga watajawa na furaha pale ambapo ndoa hizo zinafungwa, ndugu, jamaa na familia wakishuhudia." Bi Taubira anasema.

Wakati rais François Hollande alipoahidi kushughulikia kuruhusu ndoa za jinsia moja, haikuwa na utata kwa sana, lakini jambo hilo limekuwa likimgusa karibu kila mtu, na kupelekea umaarufu wa rais Hollande kushuka sana.

wabunge wa chama cha msimao mkali cha UMP, kupitia mbunge wake, Laurent Wauquire, ameiambia serikali kuwa licha ya wao kuforce kupitisha jambo hilo kuwa sheria, lakini hiyo haitowazuia watu kuingia mtaani na kuandamana kulipinga jambo hilo, wakitaka lirudishwe kwenye hatua ya muswada ili baadae liondolewe kabisa.

Hali yamtaani karibu na bunge ilikuwa tofauti, watu kadhaa wakishuhudiwa kuwa na chupa za wine na champagne, wakijipongeza kwa kunywa, akili zao zikichangamka kwa kujua kwamba sasa wanaweza kuoana jinsia moja na pia kuasili mtoto kama ambavyo haki hiyo ipo kwa wanandoa wowote wale.

Kwa upande mwingine, wapinzani wa ndoa za jinsia moja nao pia walionekana mtaani wakipinga hatua hiyo huku wakionesha alama ya vidole viwili kwenye maeneo mengi akama ambavyo GK imeshuhudia kwenye vyombo kadhaa vya habari.

Mwezi Aprili unashuhudia nchi ya pili ikipitisha muswada huu, huku New Zealand likiwa taifa la kwanza Asia Pacific kuruhusu ndoa za jinsia moja, ikiungana na mataifa mengine ya Ulaya kama vile Uholanzi, Ubeljiji, Spain, Norway, Denmark, Ureno, Iceland na Sweden, ambayo kwa muda sasa imekuwa kimbilio la Waafrika wanaounga mkono ndoa za namna hiyo, huku wakitimkia hukokufunga ndoa zao. Na iwapo Rais wa Ufaransa atatia saini kwenye muswada huo, basi Wafaransa watakuwa wamepewashiwa taa ya kijani kwa ajili ya vitendo hiyvo

Jumanne, 23 Aprili 2013

Bayern yaitandika 4-0 Barcelona


Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia bao la kwanza

 Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Barcelona 4-0 katika mchezo wa kwanzawa nusu fainali nchini Ujerumani.

Mabao mawili ya Thomas Müller, na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliizamisha Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa,akiwemo Messi ambaye alikosa michezo kadhaa kabla ya kuanzishwa hii leo.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kufungwa mabao 4-0 tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kyiv ya Urusi mwaka 1997 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

Habari  zaidi zinakujia hivi punde

Tundu Lissu asema Fujo zitaisha spika akiacha upendeledo



Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema fujo zitaisha bungeni ikiwa Spika wa Bunge, Naibu na Wenyeviti watafuata na kusimamia kanuni za Bunge bila kupendelea upande wowote.

Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Alisema fujo hazitaisha kama watu hawatafuata kanuni na Spika kusimamia na kuzingatia mamlaka yake bila ya upendeleo wowote.

“Tatizo kubwa Spika anafanya kazi bila kufuata kanuni za Bunge. Kuna mambo mengine anayatolea maamuzi bila kufuata kanuni za Bunge. Mfano suala letu la adhabu tuliyopewa wabunge watano wa Chadema ya kutohudhuria vikao vitano. Hakuna katika kanuni za Bunge. Spika alipaswa kupeleka majina yetu katika Kamati ya Maadili ili ichunguze na kupendekeza adhabu kisha ipeleke taarifa bungeni na Bunge ndilo litoe adhabu," alisema.

Alisema kama utaratibu ndani ya Bunge unakiukwa, Chadema wataendelea kupinga hata kama watafukuzwa kila mara kwani wasipofanya hivyo athari yake itakuwa kubwa hapo baadaye.

“Hata kama watu wote watasema niache kuongea, nasema siwezi kuacha mimi ni mbunge na sehemu yangu kubwa ya kazi ni bungeni. Hivyo nikifika huko lazima nitazungumza, kama sitazungumza ndani ya Bunge, nitazungumza nje na nikirudi tena ndani nitalizungumza,” alisema.

Lissu aliongeza kuwa hulka ya Bunge ni kelele na  hii si hapa nchini tu, bali hata nchi nyingine, ila tatizo la Watanzania ni uchanga wa mfumo wa vyama vingi na ndiyo maana wanaona mambo hayo kama ni mageni.

CHANZO: ALASIRI

Uchunguzi kesi ya Lwakatare wakamilika


Dar es Salaam: Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mulungu, amesema upelelezi kuhusu tuhuma za vitendo vya ugaidi zinazomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatale na mwenzake Joseph Ludovick umekamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mulungu alisema kwa sasa jalada linaandaliwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.

Lwakatare na mwenzake, Ludovick, wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, katika Mahakama ya Kisutu.

Watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kufanya mipango ya kumteka na kutaka kumdhuru kwa sumu, Dennis Msacky.

Kuhusu kesi ya kumwagiwa tindikali Kada wa CCM, Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Igunga Septemba 2011, alisema tayari watuhumiwa wawili wamekwishafikishwa mahakamani.

Mulungu alisema kuhusu kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka na matukio mengine yaliyotokea Zanzibar, upelelezi bado unaendelea na kwamba upo katika hatua mbalimbali. Aliwataka watu kuwa na subira

FA Uingereza yamfungulia mashtaka Suarez


Suarez akimng`ata Ivanovic uwanjani

Chama cha soka nchini Uingereza, FA kimenuia kumpa adhabu kali mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwa kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mchezo wa jumapili baina ya Liverpool na Chelsea,mchezo uliomalizika kwa sare ya 2-2.
FA imesema mwamuzi wa mchezo huo hakukiona kitendo hicho uwanjani lakini marejeo ya picha za mchezo huo zilionyesha Suarez alimng'ata Ivanovic,kitendo ambacho kinachukuliwa kama vurugu mchezoni na adhabu yake ni kufungiwa mechi tatu lakini adhabu hiyo haitoshi kwa tukio alilolifanya Suarez.
Suarez amepewa muda wa mpaka saa 12 jioni jumanne ya April 23, awe amekubali au kukataa kosa hilo kabla ya tume ya kudhibiti maadili haijakutana hapo siku ya jumatano kutoa hukumu stahili kwa kosa hilo.
Mwenyewe Suarez aliisha kiri kufanya kosa hilo na kumuomba Ivanovic msamaha kwa njia ya simu na kuwaomba mashabiki wa soka wamsamehe kwa kosa hilo.
Klabu yake ya Liverpool imempa adhabu ya kumpiga faini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay.
Mwaka 2010, Suarez wakati akiichezea Ajax ya Uholanzi alimng'ata begani kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal na kufungiwa mechi saba na chama cha soka nchini Uholanzi kwa kosa hilo.
Itakumbukwa Suarez tayari amekwishawahi kufungiwa kutocheza mechi nane za mashindano nchini Uingereza na faini ya paundi elfu 40 kwa kosa la kumtolea lugha ya kibaguzi beki wa Manchester United Patrice Evra mwaka 2011.

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More