Mnamo
tarehe 01/04/2013 muda wa saa 4:40 asubuhi huko Moshono Tanganyika Parkers
kwenye machimbo ya moramu, watu kumi na tano (15) wakiwa katika uchimbaji na
upakiaji wa moramu waliangukiwa na kifusi cha udongo wa moramu na
hatimaye kusababisha vifo vya watu kumi na tatu (13) na wawili kujeruhiwa.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba, muda wa saa 4:00 asubuhi watu hao walikuwa
wanapakia moramu katika magari mawili ambayo ni Scania lenye namba za
usajili T. 886 BDA na jingine ni aina ya Mitsubishi Fuso lenye
namba za usajili T. 109 AYB.
Ilipofika muda huo wa asubuhi, kifusi cha moramu kiliporomoka ghafla na
kuwafunika watu wote waliokuwa katika eneo hilo. Mpaka hivi sasa Jeshi la
Polisi Mkoani hapa limetambua miili ya marehemu pamoja na majeruhi.
Waliofariki katika ajali hiyo ni:- Julius s/o Peter Palangyo (56) mkazi
wa Nkoaranga Wilayani Arumeru, Fredy s/o Loserian (21) mkazi wa
Tanganyika Parkers Moshono,Christopher s/o Laurent (24) kondakta na ni
mkazi wa Kijenge, Gerald s/o Jacob maarufu kwa jina la kababu (24) mkazi
wa Moivaro, Gerald s/o Masai (33) mkazi wa Tanganyika Parkers, Japhet
s/o Amani Kivuyo (27) mkazi wa Moshono na Mwenda s/o Stephano (25)
mkazi wa Moivaro.
Wengine
ni Elias s/o Fanuel (28) mkazi wa Tanganyika Parkers, Barick s/o
Kipara (26) mkazi wa Moshono, Seurii s/o Raphael maarufu kwa jina la mbu
(24) mkazi wa Moshono, Alex s/o Marick (23) dereva na ni mkazi wa
Moshono, Hassan s/o Mussa (24) mkazi wa Moshono na wa mwisho ni Gerald
s/o Nerujangi (45) mkazi wa Moshono.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,
0 maoni:
Chapisha Maoni