Mkandarasi Raza Hassan Raza akiinama tayari kusujudu baada ya kufikishwa mahakamani.
Akiwa kaifikia ardhi kwa ajili ya kusujudu
Akiongea na wakili wake Mahakamani
MKANDARASI wa jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa iliyopita na
kuua watu kadhaa kwenye Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, Raza
Hussein Raza, na wenzake 10 leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini.
Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka
24 ya kuua bila kukusudia. Katika kesi hiyo mawakili wa upande wa
utetezi waliwapigania wateja wao kupata dhamana lakini upande wa
mashitaka ulipinga ombi hilo na kuzua mjadala mzito ulioshindwa
kupatikana suluhu.
Washitakiwa wamerudishwa rumande mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Posted in:
0 maoni:
Chapisha Maoni