Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

This is default featured post 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured post 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Alhamisi, 30 Mei 2013

Lipumba arekodiwa kwenye video 'akihamasisha UDINI' msikitini


Mwishoni mwa wiki zilipatikana taarifa za kushitua kumhusu Mwenyekiti wa Taifa cha Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba. Gazeti moja liliripoti kuwa limenasa mkanda wa video unaomwonyesha Prof. Lipumba si tu akikiri kuwa alimsaidia Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita bali pia ‘akihamasisha udini’ kwa kutaka Waislamu wajipange kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Awali nilitarajia mambo mawili, kwanza, Profesa Lipumba kupata ujasiri wa kufafanua kuhusu video hiyo, na pili, taarifa kutoka Ikulu aidha kukanusha au kufafanua kuhusu ‘msaada wa Prof Lipumba kwa Rais Kikwete.’ Hadi ninapoandika makala hii, hayo yote hayajatokea, na hivyo kilichozungumzwa na Lipumba kinaendelea kubaki halali.
Ni vema tutakumbuka kuwa hivi majuzi tu, Rais Kikwete alieleza bayana kuwa kuibuka kwa tatizo la udini kuna ‘mkono wa nchi za nje.’ Binafsi, nilitafsiri kauli hiyo ya Rais kama ‘kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.’ Ninapata taabu kuamini maelezo ya Rais wangu kuhusu uhusika wa mataifa ya nje kwenye tatizo la udini hususan kwa sababu hakutaja japo nchi moja inayochochea tatizo hilo huko nyumbani.
Na kwa upande mwingine, kutaja tu uhusika wa mataifa ya nje hakutoi maelezo ya kutosha kwani bado kuna swali la; je, ni sera ya taifa fulani dhidi yetu au ni vitendo vya watu binafsi walio nje ya nchi dhidi ya taifa letu.’
Ukisikiliza kwa makini maelezo ya Prof Lipumba, unaweza kuelewa vyema jinsi udini ulivyotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo Kikwete aliibuka mshindi. Lipumba amebainisha wazi kwenye video hiyo kuwa Waislamu walihamasishwa kumpigia kura Kikwete kwa matarajio kwamba angesaidia kutatua matatizo yao. Hata hivyo, kwa mujibu wa video hiyo, inaelekea kuwa matarajio hayo hayajatimia, na Lipumba amesikika akihamasisha Waislamu “Wajipange kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015...kwa vile wenzetu (ninaamini akimaanisha Wakristo) wameshaanza kujipanga.”
Katika namna isiyopendeza kabisa, Prof Lipumba amejaribu kuifanya ajenda ya utajiri wa rasilimali tulionao, ambao unahujumiwa na mafisadi, kuwa ina uhusiano na ‘wenzetu’ (yaani Wakristo).
Nilitarajia Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, angekuwa mtu wa kwanza kutoa wito kwa Lipumba kuachia ngazi mara moja, kama ambavyo amekuwa ‘mwiba mkali’ kwa CHADEMA kiasi cha kujengeka picha kuwa Msajili huyo ni mithili ya mtumishi wa CCM.
Pamoja na ‘kumhukumu’ Prof. Lipumba kwa kauli zake, binafsi ninaamini kuwa alizungumza hayo si kama Mwenyekiti wa CUF bali muumini tu wa kawaida wa dini ya Kiislamu. Tatizo ni kwamba ni vigumu kutofautisha matamshi ya Lipumba mwanasiasa na Lipumba muumini. Lakini kibaya zaidi, bila kujali matamshi hayo yalitolewa na Lipumba katika wadhifa gani, madhara yake yanabaki kuwa makubwa.
Hivi tukiweka kando mkanda huo mmoja wa video, Prof Lipumba ameshapita katika misikiti mingapi akimwaga sumu hiyo ya udini? Je, Lipumba anaweza kuwathibitishia Watanzania kuwa kuna chama kimoja (ambapo ni dhahiri alimaanisha CHADEMA) kinafanya harakati za kuingia Ikulu kwa kusaidia na mataifa yasiyoutakia mema Uislamu?
Wakati hoja za mwanasiasa huyo msomi kuhusu jinsi nchi yetu ilivyo tajiri wa rasilimali lakini inakwamishwa na ufisadi unaolelewa na CCM zina mashiko, ‘tiba’ anayopendekeza ya kutumia udini si tiba bali ni sumu kali kabisa.
Ningependa kuchambua kwa undani zaidi kuhusu suala hili lakini nafasi hainiruhusu. Hata hivyo, ninaomba kuhitimisha makala hii kwa kutoa wito wa haraka kuwa Profesa Lipumba anastahili kujiuzulu mara moja.
Kauli zake za kuchochea udini hazina nafasi hata kidogo katika siasa za Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa tatizo la udini limeshasababisha madhara kadhaa hadi sasa.
Kwa Lipumba kuendelea kubaki madarakani itarejesha picha ile ile ya mwaka 1995 kwamba CUF inatumia Uislamu kama silaha yake ya kisiasa, kwani haiwezekani chama kuwa chini ya Mwenyekiti anayehubiri udini pasipo chama hicho kuridhia udini kuwa ni moja ya sera zake.
Iwapo Lipumba atagoma kujiuzulu, basi ninaisihi CHADEMA (ambayo japo haikutajwa bayana kwenye video hiyo) ianzishe jitihada za kuhakikisha mwanasiasa huyo ‘anakwenda na maji.’
Kadhalika, ninataraji Msajili wa Vyama vya Siasa, Tendwa atatumia nguvu ile ile anayotumia dhidi ya CHADEMA kuchukua hatua stahili dhidi ya Prof Lipumba.
Vilevile, iwapo Lipumba hatojiuzulu, ninashauri waumini wa dini ya Kikristo kumshinikiza Lipumba ajiuzulu kwa sababu kamwe hatuwezi kuruhusu kuwepo kwa Uchaguzi Mkuu ambao mmoja wa wagombea urais (labda Lipumba atagombea tena mwaka 2015) ni mdini (angalau kwa mtizamo wake).
Nihitimishe makala hii kwa kutoa wito wa moja kwa moja kwa Profesa Lipumba kuwa licha ya kuthamini mchango wake kwa taifa na kimataifa, hususan katika nyanja za siasa na uchumi, alichokizungumza hakikubaliki hata kidogo. Na ni matarajio yangu kuwa atakuwa muungwana kwa sio tu kuomba radhi Watanzania pasi kujali itikadi zao za kisiasa na kidini, bali pia kujiuzulu uenyekiti wa CUF mara moja.
 Kwa wale wanaotaka kuangalia video angalia link hii http://www.chahali.com/2013/05/lipumba-arekodiwa-kwenye-video.html

Ushoga walivunja Bunge


NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, jana alilazimika kuliahirisha Bunge mara mbili na kusitisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya wabunge wa CUF kumchachamalia mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA).
Hatua hiyo ilikuja wakati Wenje akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani na kutaja vyama vya siasa vya nje rafiki vinavyoshirikiana na vyama vya CCM, CHADEMA na CUF, akisema msimamo wa kiliberali wanaoufuata CUF unashabikia ushoga na usagaji.
Pamoja na Wenje kutokuwa ameufikia ukurasa wa nane uliokuwa na maneno hayo, hotuba yake ilikatizwa kwa mwongozo ulioombwa na mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim (CUF).
Salim alitumia kanuni ya 68 (1) sambamba na 64 (1) (a) (c) akisema maneno yaliyotumika yanaudhi, kizandiki, kihuni, kishenzi, kifedhuri kisha akamtaka Wenje ayafute na kuwaomba radhi.
“Anasema kuwa chama cha CUF, kutokana na itikadi yake ya mrengo wa kiliberali ambayo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga.
“Kwamba hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone, kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja,” alisema.
Salim aliitaka CHADEMA ifute maneno hayo na kisha kuomba radhi, vile vile Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge iwachukulie hatua, vinginevyo CUF walitishia kuchukua hatua.
Wakati Salim akiomba mwongonzo huo, wabunge wa CUF na CCM walikuwa wakichagiza kwa maneno ya chini kwa chini wakisema…wamezoea hao, wapigwe, waondoe maneno, washenzi…wakome kabisa.
Baada ya mbunge huyo kumaliza, Naibu Spika, Job Ndugai, alimuuliza Wenje kama ana lolote la kusema na ndipo akaomba wabunge wenzake wamsikilize na kujaribu kuelewa alikuwa akimaanisha nini.
“Kwa heshima kubwa naomba wabunge wanielewe, hapa tumeeleza vyama vya nje vyenye mahusiano na vyama vya hapa ndani, nilieleza CCM ilivyo na mahusiano na vyama vya kikomunisti, CHADEMA inahusiana na vyama vya kidemokrasia na CUF inahusiana na vyama vya kiliberali, hapa tunazungumzia itikadi,” alisema Wenje.
Hata hivyo, hotuba yake ilikatizwa na wabunge wa CUF waliokuwa wakiongozwa na Salim, wakisimama na kuanza kuporomosha maneno mazito wakisisitiza hotuba hiyo haisomwi, huku wengine wakichana vitabu vya hotuba hiyo.
Ndugai baada ya kuona hali hiyo, ambapo baadhi ya wabunge hao wakiwemo wa CCM walikuwa wakichochea wakitaka Wenje apigwe alitangaza kuliahirisha Bunge kwa muda hadi saa 11 jioni na kuomba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikutane.
Licha ya Bunge kuahirishwa, mzozo uliendelea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa wabunge wa CUF kutaka kumpiga Wenje.
Wakati vurugu hizo zikiendelea wabunge wengi wa CHADEMA hawakuwemo ukumbini maana walikuwa kwenye kikao na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwenye ofisi za kambi, jambo lililowafanya askari wa Bunge kusogea karibu na Wenje.
Bunge laahirishwa tena
Baada ya mapumziko ya mchana Bunge lilianza kwa Ndugai kumwita Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili, John Chiligati, kueleza uamuzi uliofikiwa.
Chiligati alisema kuwa walikutana na Salim kama mlalamikaji ambaye msimamo wake ulikuwa ni kumtaka Wenje aombe radhi na kuondoa maneno hayo, masharti ambayo Wenje alikubaliana na moja la kuondoa maneno.
“Lakini aliiahidi kamati kuwa anakwenda kuibadili hotuba yake kwa kuondoa maneno hayo lakini hakuna mabadiliko aliyofanya maana maneno aliyoweka kwa Kingereza ni yaleyale aliyotakiwa kuondoa,” alisema.
Hata hivyo, Wenje alipopewa muda aseme kama anakubaliana na ushauri huo, alitoa ufafanuzi huku akionyesha nyaraka za makubaliano ya vyama vya kiliberali yaliyofikiwa mwaka 1997 na CUF kikiwa mshiriki, kisha akakataa kuomba radhi kwa maelezo kuwa haoni kosa.
Kutokana na msimamo huo, Ndugai alimwamuru Wenje kuomba radhi na kuondoa maneno hayo ndipo aweze kuendelea na hotuba yake, lakini mbunge huyo aligoma katakata kuomba radhi na hivyo akatakiwa kuketi.
“Suala hili nalirudisha kwenye kamati ya maadili ili itushauri zaidi na kwa hali hiyo siwezi kuendelea, nasitisha Bunge hadi kesho saa tatu asubuhi na tutaendelea na Wizara inayofuata ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo,” alisema Ndugai.
Wabunge welionekana kubishana kwenye makundi nje ya ukumbi huku wengi wa CCM na CHADEMA wakimsifu Wenje na kumlaumu Ndugai kuwa alishindwa kulimudu Bunge.
Mapema asubuhi
Vugugu hizo zilihamia nje ya Bunge ambapo wabunge wa CUF walikuwa wakimfuata Wenje ili kumshambulia lakini wabunge wenzake wa CHADEMA na CCM walimsihi asifanye malumbano na hivyo kumsindikiza hadi ofisi za kambi hiyo wakiongozwa na Livingstone Lusinde.
Wabunge wa CUF walikuwa wakiporomosha maneno makali na matusi dhidi ya Wenje na viongozi wengine wa CHADEMA wakiapa kuwa liwalo na liwe lakini hotuba hiyo haitasomwa hadi maneno hayo yaondolewe.
Baadhi yao, Khatib Haji (Konde), Bungala (Kilwa Kusini), Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe), Rukia Kimwaga (Viti Maalum), Salim (Mtambile) na wengineo walikuwa wakiporomosha matusi mazito wakidai kuwa CHADEMA inawadhalilisha wakati chama chao kimekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ushoga.
Hata hivyo, mabishano hayo yaliibua pande mbili ambapo baadhi ya wabunge wengi wa CCM walikuwa wakiwaunga mkono CUF wakati wengine walikuwa wakipinga na kusema kuwa hawakufasiri vyema maneno ya Wenje.
“Wacha iwapate maana wakati tulipolalamikia hotuba za CHADEMA kuwa na maneno ya kuudhi dhidi ya CCM walikaa kimya, sasa kwa nini nao wasingekuwa wavumilivu hadi amalize hotuba yake. Kwanza ukurasa wenyewe alikuwa hajaufikia pengine angeruka,” alisema mbunge wa CCM.
Naye Ndugai, aliwarushia lawama waandishi wa habari akidai kuwa wanaibeba CHADEMA hata pale wabunge wake wanapofanya mambo ya hovyo.
“Hawa wanakwenda kuwa watawala, sasa kwa mwendo huu unadhani itakuwaje lakini nyie waandishi ndio mnawabeba. Hizi hotuba tunajua sio za kambi wanaandika wenyewe,”
Hata hivyo Ndugai alikwepa kufafanua ni kwa nini kiti cha Spika hakizipitii mapema kabla ya kusomwa bungeni.

Jumanne, 28 Mei 2013

KILICHOMUUA MANGWEA HIKI HAPA.. BOFYA HAPA KUSOMA HABARI ZAIDI


HABARI za kusikitisha zilizopatikana jioni ya leo ni kwamba msanii wa muziki wa bongo fleva, albert Mangwair maarufu kam,a ;ngwair' amefariki dunia akiwa nchini Afrika kusini.
Imethibitika ni kweli Mangwea amefariki dunia leo.
Mangwair ambaye anadaiwa alikuwa huko kwa ajili ya shughuli za kimuziki, alifia kwenye hoteli moja baada ya kutoiamka tangu alipolala usiku wa jana.
Taarifa hizo zisizo rasmi zinaeleza kwamba, nyota huyo alizidisha kiwango cha dawa za kulevya ambacho ndio chanzo cha kifo chake.
Kifo cha ngwair ambaye alikuwa ni muasisi wa kundi la Chamber squad la jijini Dar es salaam, kimeleta simanzi kubwa kwa wadau wa muziki huo.
Ngwai ambaye alikuwa na kipaji cha pekee cha kuimba kwa mtindo huru 'free styles' alipata kutamba na nyimbo kama GHETO LANGU, HOSTEL, MIKASI, SPEED 120, TUPO JUU N.K.
msiba wa msanii huyo upo nyumbani kwa mama yake huko Kihonda njia ya kuelekea Mazimbu mjini Morogoro huku familia nayo ikigubikwa na utata juu ya taarifa za kifo hicho.
RIP

Sitta: Asema JK alinihujumu


WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amewatuhumu viongozi wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa walishiriki kwenye njama ovu za kumnyang’anya uspika kwa sababu waliogopa spidi na viwango vyake.
Sitta alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Mwanza.
Ingawa Sitta hakuwa tayari kutaja majina ya viongozi hao waliomhujumu, ni wazi kuwa tuhuma hizo zinamwelekea moja kwa moja Rais Jakaya Kikwete, ambaye ndiye aliongoza vikao vya kupitisha jina la mgombea uspika.
Inafahamika pia kuwa Rais Kikwete ndiye aliyeleta wazo la kuwa na spika mwanamke, kigezo ambacho Sitta asingeweza kukitimiza.
Awali kabla ya kufanyika kwa vikao hivyo mwaka 2010 kulikuwa na tetesi kuwa Sitta hatakiwi kurejea kwenye kiti hicho kwa sababu alichangia kushamiri kwa upinzani na migogoro ndani ya CCM.
Baadhi ya wagombea wa CCM waliojitokeza kuchuana na Sitta katika kuwania nafasi hiyo ni Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, na Anna Makinda. Itakumbukwa kuwa wakati anagombea uspika, Sitta alikuwa ndiye Spika kwa miaka mitano iliyotangulia (2005-2010).
Alisema hujuma hiyo ililenga kumstaafisha kwa lazima kabla ya muda wake, kwa kisingizio cha wakubwa zake hao kutaka Bunge liongozwe na mwanamke, jambo ambalo alionekana kutoridhishwa nalo.
“Siku zote mimi ni mtu wa viwango na ukweli. Hata wakati nilipokuwa Spika wa Bunge, baadhi ya wakubwa zangu wa kazi hawakufurahishwa na uwazi, viwango na spidi yangu ya kuongoza Bunge.
“Kwa sababu ya baadhi ya wakubwa wangu kutofurahishwa na viwango vyangu, nilistaafishwa Uspika kabla ya muda wangu. Sababu na kisingizio chao, eti huu ni wakati wa Bunge kuongozwa na mwanamke!. Hii mmh,” alisema.
Wajuzi wa siasa ndani ya CCM wanasema kwamba hii ilikuwa mara ya pili kwa Rais Kikwete “kumhujumu” Sitta. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 kwa kumnyima uwaziri mkuu ambao Kikwete alikuwa amemuahidi wakati wa mchakato ndani ya kundi lake la wanamtandao.
Katika mtandao huo, Kikwete alikuwa na watu wawili aliokuwa amewaahidi uwaziri mkuu – Sitta na Edward Lowassa – kila mmoja kwa muda wake. Hata hivyo, habari za ndani zinaeleza kuwa mara baada ya kushinda, Rais Kikwete alibadili msimamo, kwa kigezo kuwa alikuwa anapata wakati mgumu kumpa uwaziri mkuu mtu ambaye (yeye Kikwete) angemmwamkia “shikamoo.”
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa njama za kumwondoa Spika aliyekuwapo, Pius Msekwa, na kumhamasisha Sitta agombee uspika. Kundi la wanamtandao lilimpiga vita Msekwa likimwita “agano la kale,” likahakikisha Sitta anapita.
Hata hivyo, Sitta alifanya kazi ya uspika kwa msuguano mkubwa kati yake na Waziri Mkuu wa wakati ule, Edward Lowassa, ambaye alijiuzulu mwaka 2008 kwa shinikizo la Tume ya Bunge kuhusu kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme, Richmond.
Kuhusu ufisadi, Sitta alisema amejipambanua kupambana nao pasi na woga kwakuwa anaamini hiyo ndiyo nia nzuri ya kuliokoa taifa.
Aliongeza kuwa wapo baadhi ya watu hapa nchini wanafanya biashara ya unyonyaji na wanasafirisha fedha nje ya nchi.
Alisema biashara hizo za kiunyonyaji ndizo zinazosababisha mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuendelea kucheleweshwa, na aliwataka wasomi na Watanzania wote kutokukubali nchi kushikwa na mafisadi, kwani watu hao ni hatari na hawana huruma na uchumi wa taifa.
“Mpaka leo hii namsifu sana Baba wa Taifa, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa uadilifu aliokuwa nao. Aliona mbali, alipiga vita ukabila na unyonyaji wa rasilimali za nchi. Hivyo, tusiruhusu tabaka la watu wanyonyaji kuongoza uchumi wa taifa hili,” alisema Sitta.
Alisema, yeye binafsi kamwe hakubaliani na vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na baadhi ya watu, hivyo wasomi na Watanzania wasiunge mkono watu walioihujumu nchi kupitia mikataba mingi mibovu ya kifisadi.
Aidha, Waziri Sitta alieleza kusikitishwa na usiri wa mambo unaofanywa na Serikali kuhusu maendeleo ya nchi, na alitaka usiri huo usiwepo, huku akihoji: “Utaendeshaje nchi kwa usiri? Kwa nini ufanye siri kuhusu mambo ya kimaendeleo kwa wananchi wako?”
Aliponda pia kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi wa nchi unaoonekana sasa kwa kukua kwa asilimia 6.9 kwa mwaka, badala ya kukua kwa asilimia 10 hadi 12 kwa mwaka, na aliwalaumu baadhi ya viongozi nchini kutazama suala la kuongeza ajira badala ya kupigania ukuaji wa uchumi wa taifa.
Kustaafu ubunge
Alisema hivi sasa anafikiria kustaafu ubunge, na tayari ameshawaambia wapiga kura wa Urambo Mashariki juu ya azima yake hiyo.
Alisema ni vema na viongozi wengine wakafikiria kustaafu siasa baada ya kuwatumikia wananchi kwa kipindi kirefu.
“Viongozi wenzangu msipende kung’ang’ania madaraka. Nawaombeni mjifunze kusema yatosha …staafuni kama ninavyotaka kufanya mimi,” alisema.
Jitihada za kupata wasaidizi wa Rais Kikwete kuzungumzia kauli ya Sitta hazikuzaa matunda, kwani simu zao katika kitengo cha mawasiliano Ikulu, zilikuwa zimezimwa hadi tunakwenda mitamboni.

Dk. Mwakyembe aundiwa zengwe bandarini


MAKUNDI mawili yenye nguvu kifedha na madaraka katika mamlaka za Serikali yanapanga njama ili kukwamisha jitihada za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Makundi hayo yametajwa kutoka Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kwa pamoja wanadaiwa kuunganisha nguvu ili kupunguza kasi ya kuwafukuza watumishi wa bandari inayolenga kuziba mianya ya rushwa.
Baadhi ya watumishi TPA waliliambia MTANZANIA kuwa mkakati huo ulianza baada ya Dk. Mwakyembe kufanya operesheni ya kuwatimua baadhi ya watumishi wa bandari.

Walisema Dk. Mwakyembe amekuwa akifanya maamuzi mazito, ikiwemo kufukuza watumishi wa bandari na kuwasimamisha wengine.

“Si kazi rahisi kupata kazi bandari ukizingatia hali yenyewe ilivyo ya kupata ajira, kwanza unapata kazi kwa kuhonga hata kama una sifa zinazostahili,” walisema.

Mmoja wa wafanyakazi wa TPA, alisema Dk. Mwakyembe aliwahi kuagiza kurudishwa haraka scanner ya kupimia mizigo iliyoondolewa Bandari ya Dar es Salaam na kupelekwa Bandari ya Tanga, lakini hadi sasa haijarudishwa.

Alisema scanner hiyo ilipelekwa kwa kificho zaidi ya miaka mitatu iliyopita na haijawahi kufanya kazi yoyote huko mkoani Tanga.

Msemaji wa TPA, Janet Ruzangi alikiri scanner hiyo kupelekwa Tanga chini ya usimamizi wa TRA.

Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya hakupatikana kuzungumzia suala hilo, baada ya wasaidizi wake kutaka aandikiwe maswali.

Hata hivyo, licha ya maswali hayo kuandikwa, ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna majibu yaliyo

Source: Gazeti la Mtanzania

Jumatatu, 27 Mei 2013

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka


Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

Chadema yaipunguza kasi CCM Tabora

*Viongozi CCM wazomewa katika mkutano wa hadhara
*Ni baada ya kuanza kuwatukana viongozi wa Chadema

Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage













VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora, juzi walijikuta katika wakati mgumu, baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa, akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, walipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi ya mabasi ya zamani mjini hapa.

Mkutano huo wa hadhara ulifanyika siku chache baada ya ule wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye aliwaeleza wananchi, kuwa wabunge wa CCM mkoani Tabora hawawakilishi vema wapigakura wao na kwamba kutokana na hali hiyo, wabunge wa Chadema wameamua kupigania haki zao.
Baada ya Zitto kuhutubia katika uwanja huo, viongozi wa CCM waliamua kujibu mapigo wakiongozwa na Rage ambapo juzi waliamua kuitisha mkutano huo.

Dalili za CCM kuzomewa katika mkutano huo, zilianza mapema kabla ya kuanza kwa mkutano kwani baadhi ya wananchi walisikika wakikejeli kwamba wanataka kusikia sera si majigambo, matusi wala blaa blaa nyingine.

“Tunataka barabara za lami kuanzia Tabora-Nzega, Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora, vinginevyo wapisheni peoples power,” walisikika baadhi ya wananchi wakisema.

Wakati hayo yakitokea, Katibu wa CCM, Mkoa wa Tabora, Idd Ame, alianza kuhutubia huku akikiponda Chadema jambo ambalo liliwakera wananchi na kuanza kumzomea.

“Ndugu zangu wananchi, hebu angalieni mnavyodanganywa, hivi hawa Chadema wanajigamba kujenga barabara wakati wao siyo watoaji wa fedha, Serikali ya CCM ndiyo yenye dhamana ya fedha wala siyo hao wanafiki na waongo wakubwa.

“Mtu anaacha jimbo lake huko Kigoma anakuja hapa Tabora kuwafundisha siasa chafu, huu ni ‘upumbavu’ hatuwezi kuuvumilia,” alisema Ame.

Baada ya kauli hiyo, mkutano ulivurugika na wananchi walianza kuzomea kwa maneno ya kejeli wakidai wanataka sera na siyo matusi, huku wengine wakisema CCM ni wepesi wa kujibu hoja za Chadema na siyo kuanzisha hoja zao wenyewe.

Aidha, katibu huyo aliendelea kuwaambia wananchi kuwa kama wataendelea na tabia ya kuwasikiliza Chadema, watasababisha mapigano bila kutarajia.

“Hapa tuko kamili, endeleeni kuzomea tu, tutaumizana kweli kweli, hapa msifikiri hatuwezi na tutawashitaki viongozi wa Chadema Tabora kwa kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu,” alisikika akisema Ame.

Wakati akisema maneno hayo, yaliyoonekana kutowafurahisha baadhi ya viongozi wa meza kuu ambapo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), John Mchele, aliamua kwenda kumnong’oneza katibu huyo ili aache malumbano na wananchi.

Huku mkutano huo ukikosa utulivu, fujo kubwa zilizuka baada ya vijana wa ulinzi wa CCM wanaojulikana kama ‘Green Guard’ kuamua kutuliza vurugu hizo.

Baada ya vurugu kutulia kidogo, Rage alipanda jukwaani kuhutubia na baadaye alitoa Sh milioni 68 kwa kata kumi za Manispaa ya Tabora, ambapo kila kata ilikabidhiwa hundi yake kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa vyoo, umaliziaji nyumba za walimu pamoja na madarasa.

Pia, Rage alikabidhi pikipiki mbili kwa chama cha waendesha bodaboda na kuahidi kuendelea kutoa misaada mingine kadiri atakavyoweza.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CCM Tabora Mjini, Moshi Nkonkota, alilitupia lawama Jeshi la Polisi, kuwa hawataki kulinda mikutano ya CCM na kusababisha wafanyiwe vurugu.

Fumanizi la mume wa mtu na shoga


Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka na shoga aitwaye Aunt Steve na kuibua mtiti mzito.

Tukio hilo lililovuta umati lilijiri Mei 20, mwaka huu kwenye gesti moja (jina tunalo) iliyopo Mwananyamala, Dar ambapo mke wa Ezekiel alivamia na kutembeza mkong’oto wa hasira kwa mumewe.
ILIKUWAJE?
Mei 19, mwaka huu, saa 3:15 asubuhi, mwanamke mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya heshima yake mtaani alilipigia simu gazeti hili na kutoa malalamiko kwamba mumewe amekuwa na tabia ya kulala na wanaume wenzake ambao ni mashoga.
“Jamani, mimi naitwa… (akataja jina), naomba jina langu lisiandikwe gezetini. Malalamiko yangu ni kwamba, mume wangu amekuwa na tabia ya kulala na mashoga, hivi ninavyoongea ana ahadi ya kukutana na mmoja wao gesti kama si kesho basi keshokutwa, niliona meseji kwenye simu ya mume wangu.

“Nawaomba chondechonde, mnisaidie ili hii tabia ikome. Nipo tayari kusikia maelekezo yenu kwa sababu nimesoma kwenye gazeti lenu kwamba mnafichua maovu na huu nao ni uovu,” alisema kwa masikitiko mwanamke huyo.
MKE APEWA MAELEKEZO
Mratibu wa Oparesheni Fichua Maovu alimpa maelekezo mwanamke huyo akimtaka kufuatilia kwenye simu ya mumewe ili kubaini siku ya wawili hao kukutana gesti.
“Nawaahidi kwamba leo hiihii kabla giza halijaingia nitakuwa nimejua siku yao ya kukutana, naomba msiache kupokea simu yangu jamani.”
OFM: Sawa mama, pole sana.
Mwanamke: Asante sana.
SIMU YASUBIRIWA
Saa 11:00 jioni, mwanamke huyo alipiga simu tena kwa OFM na kupokelewa na yuleyule mratibu wake aliyempa maelekezo.
Mwanamke: Mchana wakati mume wangu amekwenda kuoga niliipekua simu yake, wanakutana kesho kwenye gesti ya …(anaitaja jina).
“Kwa hiyo mtanisaidiaje?”
OFM: Wewe kuwa beneti na mumeo, kesho akiondoka na wewe ondoka hata kwa kujificha, mfuatilie hadi kwenye hiyo gesti huku ukitupa mawasiliano.
Mwanamke: Hilo halina shida, nitakodi Bajaj halafu nitawaambia.
OFM: Oke, kuwa makini, mawasiliano ni muhimu. Tutawanasa kisha wakaishie polisi.
Mwanamke: Nitashukuru sana jamani. Loo! Kweli dunia imekwisha, mwanaume ana mke, hatosheki anatafuta wanaume wenzake, afadhali angekwenda kwa machangudoa.”
MKE ACHUKUA MASHOSTI, WATINGA GESTI
Siku ya tukio saa 8:00 mchana, mwanamke huyo akiwa ameongozana na mashoga zake, walifika kwenye gesti hiyo na kubana sehemu ambayo wangeweza kumwona anayeingia na kutoka kisha akawasiliana na mratibu wa OFM ambaye aliwatuma mapaparazi watatu wenye kamera za kupiga picha kwa umbali wa mita 100.
Kufumba na kufumbua, Aunt Steve aliwasili na kuzama ndani ya gesti hiyo kwa kutumia mlango wa nyuma ili asionekane kwa vile sheria ya serikali kuhusu gesti, wanaume hawaruhusiwi kuingia kwenye chumba kimoja.
Mapaparazi wetu wakiwa tayaritayari walitega katika pembe tatu za gesti hiyo ili kunasa tukio hilo hatua kwa hatua.
BABA KULWA NAYE HUYO
Kufumba na kufumbua, Baba Kulwa alitokea na kuingia ndani ya gesti hiyo kwa kutumia mlango mkubwa wa mbele huku akiwa hajui kama arobaini yake ilikuwa imebakiza dakika chache siku hiyo.
Alifika mapokezi na kupewa chumba No. 01, akaenda uani na kufanya jitihada kubwa za kumpitisha shoga huyo kwa mlango wa nyuma hadi ndani.
WAACHWA KWA DAKIKA KUMI ILI…
Baada ya wote kuzama chumbani, mke wa mwanaume huyo, mashosti zake na mapaparazi waliwaacha kwa dakika kumi ili wafikie hatua ya kuchojoa nguo hivyo kuweza kuwanasa wakiwa watupu.
MUDA WA MCHEZO WAFIKA
Baada ya dakika kumi, wafumaniaji wote walizama ndani na kugonga mlango wa chumba walichomo wawili hao huku shosti
mmoja wa mwanamke huyo akijitambulisha yeye ni mhudumu anawaongeza taulo. Baba Kulwa bila kufahamu janja hiyo alifungua mlango kidogo na kuchomoza kichwa lakini ghafl a akinadada hao akiwemo mkewe walimvamia na kusukuma mlango, wakazama ndani.
MBILINGE YA NGUVU
Wawili hao walikutwa hawana nguo, ndipo msala ulipomwangukia Baba Kulwa na Aunt Steve wake, mke akipewa nguvu na wapambe wake waliwatembezea kipigo huku wakiwakejeli kwa tukio hilo la aibu.
SHOGA ACHOROPOKA KAMA KAMBALE
Baada ya kuwaweka wote chini ya ulinzi, waliwatoa nje huku Baba Kulwa akiomba msamaha kwa mkewe lakini bila kukubaliwa.
“Msamaha wa nini? We si kidume cha kweli, twendeni nje tukawaanike mbele ya watu,” alisema mwanamke huyo.
Katika hali iliyoonekana ni kukosa umakini wa kuweka kizuizi vizuri, Aunt Steve alifanikiwa kuchoropoka kama samaki aina
ya kambale na kutokomea kusikojulikana huku wanawake hao wakimsindikiza na zomeazomea hadi wakafunga mtaa.
NYUMBANI KWA BABA KULWA
Taarifa za katikati ya wiki iliyopita kutoka nyumbani kwa Baba Kulwa zilidai kuwa baada ya kufi ka nyumbani, mwanamke huyo
alikusanya kila kilicho chake na kutimka zake huku mumewe akimbembeleza bila mafanikio.

Jumamosi, 25 Mei 2013

Ubaguzi kwa Waislamu waongezeka

Shirika la Uingereza la mchanganyiko wa dini mbali-mbali linasema jamii zimeingiwa na uoga tangu kuchinjwa kwa mwanajeshi wa Uingereza na Waislamu wenye siasa kali katika barabara ya mjini London.
Muislamu mjini London
Shirika hilo, Faith Matters, limesema mashambulio yameongezeka sana tangu kuuwawa kwa mwanajeshi huyo siku ya Jumatano.
Linasema limearifiwa visa zaidi ya 162 vya ubaguzi dhidi ya Waislamu katika siku mbili - kutoka misikiti kushambuliwa hadi matusi.
Viongozi wa Kiislamu wa Uingereza wamelaani vikali mauaji ya mwanajeshi huyo.

Rama mla vichwa vya watu aachiliwa huru, Je wamjua? - Bofya hapa usome zaidi

Dar es Salaam. Mshtakiwa Ramadhan Selemani Mussa, maarufu kama ‘Rama mla vichwa’, aliyekutwa na kichwa cha mtoto kikiwa bado kinavuja damu, pamoja na mama yake Hadija Ally, wameachiwa huru.
Rama na mama yake walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la kumuua kwa makusudi mtoto Salome Yohana (3), kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hata hivyo, jana Mahakama Kuu ilimwachia huru Rama baada ya kuridhika na ripoti ya jopo la madaktari waliomfanyia uchunguzi wa akili yake, iliyoeleza kuwa wakati wa tukio hilo hakuwa na akili timamu.
Wakati Rama akiachiwa kwa kutokana na ripoti hiyo ya madaktari, mama yake aliachiwa huru baada ya upande wa mashtaka (Jamhuri) katika kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2010, kudai kuwa hauna nia ya kuendelea kumshtaki.
Kuachiwa kwa washtakiwa hao kulisababisha vilio kwa mama wa mtoto aliyeuawa, Upendo Dustani na shangazi wa mtoto huyo, Furaha Mussa, aliyekuwa akiishi na mtoto huyo nyumbani kwake Tabata.
Septemba 29, 2011, Mahakama Kuu iliamuru Rama apelekwe katika hospitali ya magonjwa ya akili ili apimwe akili kama alikuwa na akili timamu au la, wakati wa tukio hilo.
Amri hiyo ya Mahakama iliyotolewa na Jaji Samuel Karua, ilitokana na maombi yaliyotolewa na Wakili Yusuph Shehe aliyekuwa akiwatetea
Wakili Shehe alisema ameamua kutoa ombi hilo ili kujiridhisha na utimamu wa akili za mshtakiwa kwanza kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo kulingana na kumbukumbu za maelezo ya ushahidi ulioko mahakamani.
Jana, kabla ya washtakiwa hao kuachiwa, Wakili wa Serikali, Secy Mkonongo aliyekuwa akisaidiana na Clara Charles, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao.
Hata hivyo Wakili Shehe alidai kuwa mara ya mwisho Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa wa kwanza, Rama, apelekwe katika hospitali ya magonjwa ya akili kwa ajili ya uchunguzi wa akili yake.
Wakili Shehe alisema ripoti hiyo tayari imeshawasilishwa mahakamani hapo kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Akili Isanga tangu Juni 20, 2012, ikiwa imesainiwa na Dk Mndeme Erasmus na kwamba inaeleza kwa mshtakiwa wakati akitenda kosa hilo hakuwa na akili timamu.
“Kutokana na ripoti hii, ninaiomba Mahakama yako ijielekeze katika vifungu cha 220 (4) na 219 (2) vya CPA kinachoelekeza Mahakama
Wakili wa Serikali Mkonongo alisema kuwa upande wa mashtaka hauna pingamizi.
Akitoa uamuzi, wake Jaji Rose Temba alisema kuwa Mahakama imetilia maanani ripoti hiyo kuwa ya uchunguzi wa akili za mshtakiwa wa kwanza kuwa wakati akitenda tukio hilo hakuwa na akili timamu.
Jaji Temba alisema kuwa kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa mahakamani hapo, inaamini kuwa mshtakiwa wa kwanza alitenda kosa la mauaji.
Hata hivyo alisema kuwa kulingana na ripoti hiyo ya daktari kuwa mshtakiwa hakuwa na akili timamu, chini ya kifungu cha 219 (2) CPA, Sura ya 20 kama kilivyorekebishwa mwaka 2002, Mahakama haiwezi kumtia hatiani.
“Naamuru aendelee kubakia chini ya uchunguzi wa Watalamu wa magonjwa ya akili na hospitali itakuwa ikitoa taarifa kwa Waziri wa Sheria na Katiba.”, alisema Jaji Temba.
Baada ya uamuzi huo dhidi ya Rama, Wakili wa Serikali, Mkonongo alisema katika kesi hiyo walibakiwa na mshtakiwa mmoja, mama yake Rama, lakini akasema kutokana na uamuzi upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshtaki.
Awali Wakili Mkonongo aliwasomea washtakiwa hao mashtaka na maelezo ya mashtaka yanayowakabili ambapo alidai kuwa April 25, 2008, saa 2:30 usiku, mtoto Salome alikuwa akicheza nje ya nyumba ya Shangazi yake Furaha Majani, akiwa na Rama na mwenzao Paschael.
Alisema baada ya baba wa mtoto huyo Yohana Mussa Majani alifika kwa dada yake huyo na kumkuta mkewe, akauliza kwa nini walikuwa wamemwacha mtoto yule nje hadi wakati ule? Wakili Mkonongo alidai kuwa Furaha alipotoka nje hakumkuta, lakini Paschael akawaambia kuwa alikuwa amepotea katika mazingira tata na kwamba aliwaambia wazazi wake wakamtafuta.

Ijumaa, 24 Mei 2013

Nini Siri ya mafanikio ya Bayern na Dortumund Kutinga Fainali UEFA? Bofya hapa uone siri ya mafanikio

Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borussia Dortmund
Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali.
Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.
Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Kocha wa Bayern Munich
Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.
Kocha wa Borussia Dortmund
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.

HABARI TOKA ZANZIBAR: Shehe wa Tumondo Zanzibar amwagiwa TINDIKALI

HABARI KWA UFUPI: Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.

Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
HABARI KUTOKA ZANZIBAR ZINASEMA;Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.

Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Alhamisi, 23 Mei 2013

KUMBE UINGEREZA NAKO UKEKETAJI UPO: Hebu soma hapa uone jinsi Wanavyoandamwa na Ukeketaji Uingereza

Ukeketaji au kukatwa kwa sehemu za siri za mwanamke , inadhaniwa kuwaathiri angalau wanawake 66,000 nchini Uingereza.
Mara nyingine kitendo hiki hufanyika kwa wasichana ambao hurejeshwa nyumbani kwa jamaa zao Afrika Mashariki, lakini pia inaaminika kuwa wanawake wanakeketwa nchini Uingereza pia.
Hata hivyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wanaotenda unyama huo lakini serikali inasisitiza kuwa iko tayari kuhakikisha kuwa ukeketaji unakwisha.
Hospitali kadhaa na kiliniki za kijamii mjini London, huwasaidia wanawake ambao wamekeketewa. Pia kuna kliniki moja Birmingham na nyingine inatarajiwa kufunguliwa Bristol.
Moja ya kliniki za serikali katika hospitali yaChelsea, huwatibu zaidi ya wanawake 100 kila mwaka ambao wamekeketwa na kuwashona kwa sababu ya imani za kitamaduni, akiwemo Filsan, mwenye umri wa miaka 35.
Filsan ni mama mwenye watoto watatu na anaishi nchini Uingereza . Alikabidhiwa nguo mpya akiwa tu na umri wa miaka saba , ikiwa ni dalili ya muda kuwadia wa yeye kukeketwa.
"wasichama wamekuwa wakikeketwa kisiri nchini humu, lakini huu ni unyanyasaji wa wanawake na watoto.''

'miguu kufungwa pamoja'

''Nilihisi uchungu mwingi, licha ya kudungwa sindano ya kumaliza uchungu. Wakati uchungu ulipokwisha, singeweza hata kwenda haja ndogo.''

"tulilazimika kulala sakafuni , kwa sababu hata hatungeweza kutembea. Miguu yetu ilikuwa imefungwa kwa kamba, kwa hivyo hatungeweza kuitenganisha , yaani uchungu ulikuwa mwingi sana.
"na sasa ikafika muda wangu kujifungua mwanangu wa kwanza. Nilichokuwa nakitafakari tu, je mtoto anaweza kupitia vipi katika sehemu ambayo imeharibiwa hivyo?
''Ilikuwa hali ngumu sana kwangu.Kutafakari yote niliyoyapitia, lakini kwa sasa nina afueni kwa sababu nilikuwa na daktari mzuri ambaye aliweza kuelewa kila kitu nilichokuwa napitia.''
  • Inasemekana kuwa zaidi ya wasichana 20,000, walio chini ya umri wa miaka 15 , huwa katika hatari ya kukeketwa kila mwaka nchini Uingereza.
  • Wanawake 66,000 nchini Uingereza wanaishi na athari na makovu ya ukeketeji nchini Uingereza.
Kumbu kumbu za Filsan humletea majonzi tele. Lakini jazi yake anayoifanya na shirika moja la kisomali, inampa matumaini kwa sababu anahisi kuwa watu wa jamii yake wameanza kupinga ukeketeaji.
Anasema kuwa watu wanafahamu na kuelewa kuwa sio kitendo kizuri na kuwa kinahitaji kukomeshwa.
Inasemekana kuwa zaidi ya wasichana 20,000, walio chini ya umri wa miaka 15 , huwa katika hatari ya kukeketwa kila mwaka nchini Uingereza.
Wanawake 66,000 nchini Uingereza wanaishi na athari na makovu ya ukeketeji.

Hakuna manufaa yoyote ya kiafya yanatokana na ukeketaji, bali wanawake huharibiwa sehemu zao za siri bure.

''Kazi nyingi inafanywa barani Afrika, lakini lazima tuwahamasishe watu ikiwemo jamii kila sehemu ambazo zinakumbatia utamaduni wa kuwakeketa wanawake,'' anasema Filsan
Tangazo maalum la kibiashara limepeperushwa kwenye stesheni moja ya kisomali na hivyo kuchochea idadi kubwa ya watu wanaopiga simu katika kniliki ya Queen Charlotte's.
Mkunga Juliet Albert, alielezea kwa nini baadhi ya familia hulazimu wasichana wao kukeketwa.
Anasema ''wanawake wengi, husema kuwa hawatakubali kufanyiwa kitendo hiki , lakini kwa sababu ya shinikizo za kimila na kitamaduni kuhusiana na ukeketeji, hawezi kukwepa.
Baadhi ya wanawake huwa na wasiwasi kuwa ikiwa wasichana wao hawatafanyiwa kitendo hicho, jamii itawatenga na kuwa hawawezi kuoleka tena.
Wao hupata matayizo mengi ya kiafya kutokana na kufanyiwa ukeketaji, kama magonjwa , uchungu wakati wa kujifungua au hata wakati wanapokuwa wanajamiiana na waume zao.
Na tunachokifanya ili kurekebisha tatizo hilo ni kushona na kuacha shimo ndogo wanayotumia kujifungulia mtoto na kujamiiana.''
Kliniki hii huwaelekeza wasichana na wanawake kwa wahudumu wa kijamii ikiwa wanahisi kuwa yeyote anakabiliwa na tisho la kukeketwa.

Waziri wa afya Anna Soubry anasifu hatua hii sana

Bi Soubry anasema kuwa wanawalinda watoto wote nchini humo licha ya wanavyotaka wazazi wao.
"licha ya kuwa hatujachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya wale wanaohusika na vitendo hivyo, haimaanishi kuwa ni sawa kwa vitendo hivyo kuendelea,'' alisema waziri Soubry

Mvutano kati ya Profesa Tibaijuka na NHC

Katika kesi hiyo, Li ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya China, alikuwa akilalamikia hatua ya kuondolewa kwenye nyumba Nambari 103 iliyopo katika vitalu namba 3, 5, 7 na 8, Barabara ya Haile Selassie, Oysterbay, Dar es Salaam.
Kesi dhidi ya NHC ilifunguliwa mwaka 2006 wakati shirika hilo likiongozwa na Martin Madekwe na imedumu kwa miaka sita hadi Aprili mwaka jana ilipotolewa hukumu wakati shirika hilo likiwa chini ya Nehemia Mchechu aliyeteuliwa mwaka 2010.

Katika hukumu yake ya Aprili 27, 2012, Jaji Atuganile Ngwala aliamuru NHC pamoja na washtakiwa wa pili na wa tatu katika shauri hilo; Lars Eric Hulstrom na Kampuni ya Udalali ya Manyoni, wamlipe Li karibu Sh478 milioni ikiwa ni fidia ya hasara na usumbufu uliosababishwa na kuhamishwa kwake kinyume cha sheria katika nyumba hiyo.
Mchanganuo huo unahusisha Sh70 milioni na Dola za Marekani 177,450 (Sawa na Sh283, 920,000 - Dola moja ni sawa na Sh1,600), gharama za kesi pamoja na riba ambazo pia zinapaswa kulipwa.
Pia Mahakama hiyo iliamuru Li arejeshwe katika makazi hayo, amri ambayo inamaanisha kuondolewa katika nyumba hiyo kwa mpangaji aliyeingizwa badala ya Li ambaye ni Hulstrom aliyekuwa mdaiwa wa pili katika kesi hiyo.
Baada ya kupokea nakala ya hukumu ya Jaji Ngwala, NHC waliazimia kukata rufaa kupinga uamuzi huo lakini habari kutoka ndani ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zinadai kwamba Waziri Tibaijuka alitoa maelekezo ya mdomo kwamba hakukuwa na haja kwa shirika hilo kukata rufaa.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinadai kwamba Waziri Tibaijuka aliitisha vikao kadhaa vilivyowahusisha watendaji wa wizara yake na wale wa NHC na moja ya ajenda ilikuwa ni kuwataka watendaji wa shirika hilo kuandaa taratibu za malipo na utekelezaji wa amri nyingine za Mahakama na si vinginevyo.
Mwandishi wetu alifanikiwa kuona muhtasari wa kikao cha Mei 21, 2012 jana ambazo zinamnukuu Profesa Tibaijuka akiwaelekeza NHC kutokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama na badala yake wamlipe Li kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo, NHC kabla ya kutekeleza maelekezo ya bosi wao huyo, iliomba ushauri wa kitaalamu kutoka Kampuni ya Uwakili; Chuwa Advocates & Co., ambayo ilishauri kwamba kulikuwa na haja ya kuukatia rufaa uamuzi huo wa Mahakama ushauri ambao mbali na kukubaliwa na menejimenti pia ulipata baraka za bodi ya shirika hilo.
NHC kupitia Chuwa Advocates & Co. ilikata rufaa katika Mahakama ya Rufani Tanzania Mei 29, 2012 ikipinga hukumu hiyo katika kesi ya madai namba 71 ya 2012 ambayo mpaka sasa inaendelea kusikilizwa na majaji watatu.
Uamuzi huo wa NHC unaelezwa kuwa umesababisha mkwaruzano baina ya Waziri Tibaijuka na Mchechu.Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Mchechu alikiri kwamba kesi baina ya NHC na Li inaendelea mahakamani lakini alikanusha kuwapo kwa mgogoro baina ya shirika analoliongoza na Waziri Tibaijuka.Kwa upande wake, Waziri Tibaijuka akizungumza mjini Dodoma alisema ni kweli kwamba kesi hiyo ipo mahakamani na kusema hawezi kuilazimisha NHC kutekeleza suala ambalo halijatolewa uamuzi wa kimahakama.
“Nadhani tuiachie Mahakama ifanye kazi yake na uamuzi utakapotoka basi tutaona jinsi utekelezaji wake utakavyokuwa,” alisema Profesa Tibaijuka.

Hali bado tete Mtwara

Mtwara. Wakati mtu mwingine akiripotiwa kufa, hali bado ni tete katika Mji wa Mtwara kutokana na mabomu ya machozi na risasi za moto kuendelea kurindima kwenye mitaa kadhaa wakati polisi wakipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi alithibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, linaloaminika kuwa linatokana na risasi.
“Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba akiwa amepigwa risasi tumboni,” alisema Dk Kodi. Inadaiwa kwamba mjamzito huyo ambaye jina lake halikufahamika, ameuawa akiwa nyumbani kwake. Kifo hicho ni cha pili baada ya Karim Shaibu (22), mkazi wa Chikongola kuuawa juzi.
Aidha, kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa mtu mwingine ambaye jinsia yake haikujulikana aliuawa kwa bomu la machozi na mwili wake kutawanyika barabarani.
Kuhusu majeruhi, Dk Kodi alisema wamefikia watu 18... “Majeruhi wa mwisho tuliyempokea ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chuno. Alikuwa amevunjwa miguu yote kwa risasi.”
Waomba hifadhi hospitalini
Umati wa watu wengi wao wakiwa kinamama na watoto umemiminika kwenye Hospitali ya Ligula kukimbia msako wa nyumba kwa nyumba unaofanywa na polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamelalamikia kitendo cha polisi kuingia katika makazi yao, kuwapiga na kuwapora mali zao.
“Magomeni A hatuna amani, askari wanaingia nyumbani kwetu, wanatupiga na kutunyang’anya simu, yaani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepotezana na watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi,” alisema Paulina Idd.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa alisema hali ni shwari na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Hadi sasa huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyofunguliwa, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya huku sauti za milio ya mabomu na bunduki ikitawala, wanajeshi waliovalia sare wametapakaa sehemu mbalimbali za mji wakiwa katika magari na pikipiki.
Nchimbi atua Mtwara, jeshi lamwaga vifaa
Dk Nchimbi aliwasili jana jioni kwa helikopta na kukutana na viongozi wa Mkoa wa Mtwara walioongozwa na Mkuu wa Mkoa, Kanali Joseph Simbakalia kujadili suala hilo.
Pia ndege kubwa ya jeshi nayo ilitua huko na wanajeshi walikuwa wakipakua vitu mbalimbali vilivyoaminika kuwa vifaa.
Jeshi hilo limeombwa kuongeza kukabiliana na vurugu hizo ambazo zimesambaa sehemu mbalimbali za Mtwara.
Imeandikwa na Haika Kimaro, Mary Sanyiwa na Elias Msuya.

Wizi na uharibifu wa muda mrefu wa miundombinu ya umeme TANESCO - waziri wa Nisati na Madini Tanzania

Dodoma. Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limepata hasara ya Jumla ya Sh966.18 milioni kutokana na wizi na uharibifu wa miundombinu katika mikoa mbalimbali nchini, Bunge lililezwa jana.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.
Waziri huyo alisema, kiasi hicho ambacho ni sawa na Dola za Marekani 603,862 kilipotea katika kipindi cha Julai 2012 hadi Aprili 2013 ambapo ni hasara kubwa zaidi kwa Tanesco.
Kwa taarifa, ni wazi kuwa Tanesco imekuwa ikipata hasara ya karibu Sh96.7 milioni kila mwezi kiasi ambacho ni kikubwa.
“Wizi na uharibifu wa muda mrefu wa miundombinu ya umeme kwa muda mrefu umekuwa ni tatizo sugu kutokana na wahusika kubuni njia mbalimbali za kufanya uharibifu huo na kuisababishia Tanesco na nchi kwa ujumla hasara kubwa,” alisema Muhongo.
Akizungumzia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara, alisema, “Tatizo la kukatika kwa umeme ni uchakavu wa miundombinu ya usambazaji na vifaa vyake pamoja na kuzidiwa uwezo kwa mifumo yake.”
Kingine alitaja kuwa ni wizi wa nyaya za shaba na mafuta ya transfoma zaidi kwenye mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Mkoa wa Tanga.
Alitaja mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo kuwa ni pamoja na kubadilisha nguzo zilizoharibika katika njia za msongo wa Kv 0.4 na Kv 11 na 33, kukata miti na kubadilisha vikombe vilivyovunjika na nyaya chakavu.
Waziri alitaja miradi mingi ya umeme ambayo wizara inajiandaa kuikamilisha katika maeneo mbalimbali nchini kuwa itagharimu fedha nyingi.
Miradi hiyo ni ile ya MCC, REA ambayo inaendelea kuzinduliwa katika maeneo tofauti na mingi imetekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha.
Kwa upande wao Kambi ya Upinzani waliitaka Wizara ya Nishati na Madini kueleza ukweli kuhusu mgao wa umeme ambao unaendelea kuwatesa Watanzania huku kukiwa na taarifa kuwa hakuna mgao.
Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo, Msemaji wa Upinzani katika Wizara ya Nishati na Madini,John Nchimbi aliituhumu Serikali kuwa imekuwa ikikanusha kuhusu mgao huo wakati hali ni tofauti na kauli ya Serikali.

Jumatano, 22 Mei 2013

GESI IBAKI AU TUGAWANE NCHI - Kikwete akemea vikali vurugu Mtwara

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewaonya watu wanaosababisha uvunjifu wa amani nchini humo kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Onyo hilo linafuatia ghasia ambapo ofisi kadha, maduka na nyumba zimechomwa katika mkoa wa Mtwara ulioko kusini mashariki mwa Tanzania leo.
Akihutubia kupitia televisheni ya taifa, TBC1, Rais Kikwete amesema wale waliokamatwa na polisi wakati wa ghasia hizo watashitakiwa.
Ghasia hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni. Akizungumzia madai ya waandamanaji hao, Rais Kikwete amesisitiza kuwa raslimali za nchi ni mali ya taifa zima.
Amesema mkoa wa Mtwara haujatelekezwa na kusema kwamba kuna mipango ya kutumia gesi hiyo kujenga viwanda vya mbolea na kutumia gesi hiyo asilia kuzalisha nishati ya umeme kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma ili kuunganishwa katika gridi ya taifa.

Ofisi zachomwa

Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa mkoa wa Mtwara kamanda Linus Sinzumwa, vurugu hizo zimetokea asubuhi ya leo mara baada ya Wizara ya Madini na Nishati kusoma bajeti yake ya makadirio ya mapato na matumizi huko Bungeni mjini Dodoma na kusababisha uharibifu wa mali.
Ametaja uharibifu huo kuwa ni pamoja na kuchomwa kwa majengo ya serikali kama mahakama, nyumba za watendaji wa serikali, baadhi ya majengo ya chama tawala na nyumba za watu binafsi.

Polisi wawasaka waandamanaji Mtwara
Hata hivyo, kamanda huyo, amekanusha taarifa za kuuawa kwa mtu mmoja katika eneo hilo na kubomolewa kwa daraja linalounganisha mji wa Mtwara na maeneo mengine.
Kamanda Sinzumwa amesema watu wapatao tisini na mmoja wanashikiliwa na jeshi na polisi kuhusiana na matukio mbalimbali ya ghasia hizo.
Ghasia hizo, zinahusishwa na madai ya muda mrefu sasa ya wananchi wa mkoa huo kupinga ujenzi wa bomba la gesi iliyogunduliwa mkoani humo kusafirishwa hadi Dar es Salaam, kaskazini mwa Mkoa wa Mtwara, kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme.
Hii ni mara ya pili mkoani Mtwara kutokea kwa ghasia zinazohusisha maafa kwa binadamu na uharibifu wa mali kama ilivyotokea mapema mwaka huu.

Kweli dunia imevaa bukta inatroti sasa hebu ona tena tukio jingine - Shambulizi la kigaidi mjini London

Mtu mmoja ameuwawa katika shambulio la mapanga na washukiwa wawili wamepigwa risasi na polisi katika mtaa wa Woolwich, kusini mashariki ya London.
Waziri Mkuu David Cameron amesema kuna ishara nzito kua ni tukio la kigaidi na Uingereza haitaterereka wakati inakabiliwa na mashambulio kama hayo.
Picha za video zimejitokeza zikimuonyesha mtu akipunga panga la kuchinja nyama na kutoa matamshi ya kisiasa.
Akisema " Lazima tupigane nao kama wanavyopigana nasi. Jicho kwa jicho,jino kwa jino".
Taarifa zizisothibitishwa zaeleza mtu aliyeuwawa alikuwa mwanajeshi katika kambi ya kijeshi ya Woolwich.
Makao ya waziri mkuu yamesema Bwana Cameron ambae alipanga kulala mjini Paris baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa anarejea Uingereza.
Waziri wa mambo ya ndani Theresa May aliita mkutano wa kamati ya dharura ya usalama , Cobra.
Watu wote wawili waliopigwa risasi na polisi walipelekwa hospitali na mmoja anasemekana kua katika hali mbaya.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema watu hao wawili walimshambulia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 ambae alikua amevalia fulana iliyokua na maandishi ya wakfu wa kuwasaidia wanajeshi uitwao Help for Heroes.Msaada kwa mashujaa

Mtwara Kimenuka: Fujo mtindo mmoja amani hakuna Bofya hapa ujionee mwenyewe

  • Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 
  • Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 
  • Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
  • Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
  • Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
  •  Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
  • Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
  • Matairi  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto   wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
  • Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi
  • Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
  • Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora vinalia ovyo ovyo.
  • watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia
  • Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi wayapate .
  •  Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
  • Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo.
  • Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.
  • Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
  • Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.
  • Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
  • Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
  • Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
  • Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.
  • Kesho inaendelea tena kwa siku ya pili.  
  • Serikali  isipoangalia inaweza ikasababisha "Uprising" maeneo mengine ya nchi.


HALI YA MTWARA MAENEO YA NKANALEDI MAGOMENI




Tume yasema wakuu wawajibishwe Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake wametajwa katika ripoti inayowahusisha na ghasia za baada ya uchaguzi katika ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu ukiukwaji wa haki za bindamau nchini humo.
Ripoti hiyo hata hivyo haikutoa mapendekezo ya hatua inazotaka kuchukuliwa dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Mwenyekiti wa tume hiyo, aliambia BBC kuwa ni kwa sababu wawili hao wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya kimataifa ya ICC.
Rais Kenyatta na bwana Ruto wanakana tuhuma hizo.
Tume ya maridhiano na haki ilikabidhiwa jukumu la kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa tangu mwaka 1963 nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake.
Iliundwa baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/08 uliozua ghasia miaka mitano iliyopita kama njia ya kuleta maridhiano miongoni mwa wakenya.

Baada ya uchaguzi huo, watu 1,500 waliuawa na wengine zaidi ya 600,000 kulazimika kutoroka makwao.
Kenyatta na Ruto, waliokuwa mahasimu katika uchaguzi wa mwaka 2007, walishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi baada ua kuungana chini ya muungano wa Jubilee.
Licha ya kuwa hakuna mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo dhidi ya Rais na naibu wake, inapendekeza uchunguzi zaidi dhidi ya maafisa wakuu waliotajwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 na hata kufunguliwa mashtaka
Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na waziri mpya wa madini Najib Balala na maseneta wawili.
Hata hivyo yume hiyo ilimtaka rais Kenyatta kuwaomba radhi wakenya kwa makosa waliyotendewa chini ya seri9kali zilizopita katika kipindi cha miezi sita tangu kukabidhiwa ripoti hiyo hapo jana.
Rais mstaafu Daniel Moi pia alitajwa katika ripoti hiyo akihusishwa na mauaji ya waliokuwa wanasiasa mashuhuri wakati wa utawala wake

Maalim Seif: Nitaomba kuwania tena urais mwaka 2015

Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ataomba tena kugombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV, Maalim Seif alisema kuwa anachoomba tu Mwenyezi Mungu ampe afya njema.
“Ni uamuzi wa wananchi na wanachama wenyewe wa CUF lakini kama Mwenyezi Mungu akinipa afya na uzima bado nia ipo,” alisema Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Alisema hivi sasa chama hicho kimekuwa kikijiimarisha visiwani huko kwa kufanya mikutano Pemba na Unguja ili kuhakikisha kinaendelea kukubalika kwa wananchi.
Kauli hiyo ya Maalim Seif ambaye amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi, ilipokewa kwa hisia tofauti ambapo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ali alisema vyama vya siasa ni lazima viwe vinatayarisha viongozi wa baadaye ambao watafahamu kwamba uongozi ni dhamana wanayopewa na wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Maalim Seif kama mwanachama wa chama hicho anaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa dola.

Bandari D’Salaam yapoteza Sh3 trilioni kwa mwaka

Dar es Salaam. Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikilikosesha taifa Dola 1.8 bilioni za Marekani (Sh2.8 trilioni) kwa mwaka, kutokana na kukosa ubora wa biashara.
Kutokana na hali hiyo, wataalamu wameeleza kuwa bandari hiyo inahitaji kufanyiwa maboresho muhimu ya hali ya juu, ili fedha hizo zisaidie nchi kuacha kutegemea misaada ya maendeleo.
Kwa mujibu wa ripoti iliyopo kwenye kitabu cha Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania, licha ya Bandari ya Dar es Salaam kuwa sehemu nzuri, imekosa uwezo hivyo usimamiaji sera bora za kuiboresha zinatekelezwa taratibu. Ripoti hiyo inaeleza kuwa, mwaka 2012 pekee bandari hiyo ilikosesha taifa kiasi hicho cha fedha, huku ikizikosesha nchi jirani Sh1.3 trilioni.
“Fedha hizo ni sawa na asilimia saba ya pato la taifa, kitu ambacho kinawaathiri wanunuzi, wafanyabiashara na wakala mbalimbali wa Serikali,” inaeleza.
Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB), Jacques Morisset ameihimiza Tanzania kuifanya bandari hiyo kuwa moja ya vipaumbele vyake vya juu kwa ajili ya kukua kwa uchumi.
“Watumiaji Bandari ya Dar es Salaam wanalipa fedha nyingi kwa wasimamizi wa bandari na wakala mbalimbali, kwa ajili ya huduma zao kuliko Mombasa,” alisema Morisset.
Akizungumzia ripoti hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha bandari hiyo, lakini kazi ya ziada inahitajika kuifanya iweze kushindana na nyingine. “Tunahitaji nchi jirani ziendelee kuitumia bandari yetu, bado tuna kazi kubwa ya kufanya ndiyo maana niko hapa, tunahitaji kuimarisha Kitengo cha Operesheni na maeneo mengine,” alisema Dk Mwakyembe.

Jumanne, 21 Mei 2013

Mapigano yaendelea kwa siku ya pili Goma


Mamia wanatoroka maeneo ya vita Goma 
kukimbilia usalama wao
Makabiliano kati ya jeshi na waasi wa kundi la M23 Mashariki mwa Congo yameendelea kwa siku ya pili.
Pande hizo mbili, zilifyatuliana risasi mjini Goma huku kila upande ukituhumu mwingine kwa kuanzisha uchokozi na kuchochea mapigano.
Mapigano yalianza Jumatatu na kumaliza makubaliano ya miezi sita ya kusitisha vita kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa kundi la M-23 , ambao waliwahi kuteka mji wa Goma mwaka jana ingawa kwa muda mfupi.

Mtaalamu wa maswala ya kijeshi amesema kuwa waasi wa M23 wanatumia makombora na magari ya kivita ambayo waliyapokonya wananajeshi Novemba mwaka jana.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anayetarajiwa kuzuru Goma wiki hii alisema ataharakisha mpango wa kupelekwa kwa wanajeshi wa Umoja wa mataifa katika eneo hilo kujaribu kusitisha uasi .
Kikosi cha UN kitakachokwenda DRC kupambana na waasi, kitajumuisha wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.
Taarifa zinasema kuwa watu 19 wameuawa na wengine 27 kujeruhiwa katika mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali mjini Goma DRC.
Mapambano yalikuwa makali kwa siku ya pili huku katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akitarajiwa kuwasili mjini humo hapo kesho, kama sehemu ya ziara yake ya eneo hilo.
Chanzo: bbc.com

Rais Obama ajiandaa kwa ziara Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama atazuru Afrika 
kwa mara ya tatu
Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White house.
Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii.
Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake ya pili Kusini mwa jagwa la Sahara akiwa rais wa Marekani.
Alizuru Ghana mwaka 2009 .
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na mwenzake George W Bush, wote walizuru Afrika wakati wa muhula wao wa pili wa utawala.
Clinton alizuru nchi sita wakati Bush akizuru nchi tano.
''Rais atatilia mkazo uhusiano kati ya Marekani na baadhi ya nchi za kiafrika ambazo zinakuwa ikiwemo maswala kama ukuwaji wa uchumi, uekezaji na biashara pamoja na kukuza taasisi za kidemokrasia na kuendelea kukuza viongozi wa kizazi kijacho Afrika,'' ilinukuu taarifa kutoka ikulu ya White House.
Ziara ya Obama pia itatilia mkazo kukuza uhusiano kati ya Marekani na watu wa bara la Afrika ili kuendeleza ushirikiano wa kikanda, amani na ukuwaji.
Wadadisi wanasema kuwa ziara kama hizi hufanywa sana na marais wa Marekani hasa baada ya kuondokewa na kazi ngumu ya kampeini za uchaguzi na shinikizo za ndani ya nchi.
Wakati huohuo, tisho linaloongezeka kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali, limefanya kanda hiyo kumulikwa zaidi na Marekani. Bi Michel Obama ataambatana na mumewe katika ziara hiyo.

Lissu abadili mbinu uzinduzi kampeni

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anna Kilango akizozana na mnadhumu wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu nje ya ukumbi wa Bunge jana baada ya Spika kuahirisha Bunge akiagiza hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kufanyiwa marekebisho.
Ikungi. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi wa nafasi ya udiwani Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja, Wilaya ya Ikungi, Tundu Lissu, juzi alishindwa kuuza sera za Chadema, na badala yake alitumia muda mwingi kuhimiza ‘sera ya kuwakataza’ wananchi kuchangia maendeleo yao .
Tundu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia chama hicho, alipanda jukwaani huku akiwa amebeba makabrasha ya michanganuo ya Bajeti ya Serikali ya kuanzia mwaka wa fedha wa 2010/11 hadi 2013/14.
“Mimi leo sitaki kabisa kuzungumzia habari za Amosi Mghenyi ambaye ametusaliti kwa kuhama Chadema na kurejea CCM. Amosi kisiasa ni mfu, kwa hiyo siwezi kupoteza muda wangu kuzungumiza mambo ya mfu”,alisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha iseke.
Alisema ufunguzi wake utajikita zaidi katika kuwaelimisha wananchi wa Kata ya Iseke kwamba Serikali inazo fedha nyingi na za kutosha kugharamia maendeleo ya wananchi.
Akijenga hoja yake hiyo, alisema kwa mfano katika mwaka wa fedha wa mwaka 2010/11, Mkoa wa Singida, ulipewa zaidi ya Sh903 milioni za undeshaji wa shule, lakini zilizotumika ni Sh464 milioni na kubaki Sh438.2.
Alisema fedha hizo zaidi ya Sh438.2 milioni zilizobaki, hazijaainishwa zilipelekwa wapi. “Kwa vyo vyote zitakuwa zimeishia kwenye matumbo ya mgambo na watendaji wa Serikali ya CCM”.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma, aliwataka wakazi wa Kata ya Iseke, kumchagua Emmnuel Jackson Jingu awe diwani wao.
ili waondokane na manyanyaso ya michango kama walivyojikomboa wakazi wa Jimbo la Singida Mashariki.
Wagombea wengine wa nafasi ya udiwani Kata ya Iseke, ni Amosi Munghenyi wa CCM na Abdallah Kinyenje maarufu kwa jina la Petro wa CUF.

MSIWAUE WAPENZI WA JINSIA MOJA. RAIS MSEVENI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja
 
Katika matamshi yake ya kwanza hadharani, kuhusu muswada huo, Rais Museveni amekariri kuwa suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kupewa nafasi kukita mizizi.
Muswada wa awali uliowasilishwa katika bunge la Uganda, ulipendekeza adhabu ya kifo kwa wale watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini kipengele hicho kimefutwa katika muswada mpya.
Katiba ya Uganda kwa sasa inaharamisha mapenzi ya jinsia moja.

Serikali imekana kuhusika na mswada huo

Mwandishi wa Uingereza aliyekamatwa kwa kuandika mchezo kuhusu hatma ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda
Mwandishi wa BBC mjini Kampala, anasema serikali ya nchi hiyo imesema kuwa mswada huo uliwasilishwa na mbunge na wala sio muswada wa serikali.
Katika hotuba yake wakati wa kuapishwa kwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Uganda Rais Museveni, alijiepusha kuupinga au kuunga mkono muswada huo.
Rais alisema, ''ikiwa kuna watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, hatutawaua au kuwanyanyasa lakini suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kuhimizwa katika jamii''
''Hatuwezi kukubali mapenzi ya jinsia moja kupewa msisitizo zaidi katika jamii kana kwamba ni jambo nzuri'' aliongeza rais Museveni.
Mawaziri wamewaonya wabunge kuwa ikiwa watapitisha muswada huo, basi kutakuwa na athari kubwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na jamii ya kimataifa.
Mataifa ya Magharibi yamelaani muswada huo na wametishia kusitisha misaada kwa Uganda ikiwa itapitishwa na bunge la nchi hiyo.
Spika wa bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amesema muswada huo utapitishwa kama zawadi ya Krismasi kwa mawakili wake

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More