Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

Alhamisi, 30 Mei 2013

Lipumba arekodiwa kwenye video 'akihamasisha UDINI' msikitini

Mwishoni mwa wiki zilipatikana taarifa za kushitua kumhusu Mwenyekiti wa Taifa cha Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba. Gazeti moja liliripoti kuwa limenasa mkanda wa video unaomwonyesha Prof. Lipumba si tu akikiri kuwa alimsaidia Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita bali pia ‘akihamasisha udini’ kwa kutaka Waislamu wajipange kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao. Awali nilitarajia mambo mawili, kwanza, Profesa Lipumba kupata ujasiri wa kufafanua...

Ushoga walivunja Bunge

NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, jana alilazimika kuliahirisha Bunge mara mbili na kusitisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya wabunge wa CUF kumchachamalia mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA). Hatua hiyo ilikuja wakati Wenje akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani na kutaja vyama vya siasa vya nje rafiki vinavyoshirikiana na vyama vya CCM, CHADEMA na CUF, akisema msimamo wa kiliberali wanaoufuata CUF unashabikia...

Jumanne, 28 Mei 2013

KILICHOMUUA MANGWEA HIKI HAPA.. BOFYA HAPA KUSOMA HABARI ZAIDI

HABARI za kusikitisha zilizopatikana jioni ya leo ni kwamba msanii wa muziki wa bongo fleva, albert Mangwair maarufu kam,a ;ngwair' amefariki dunia akiwa nchini Afrika kusini. Imethibitika ni kweli Mangwea amefariki dunia leo. Mangwair ambaye anadaiwa alikuwa huko kwa ajili ya shughuli za kimuziki, alifia kwenye hoteli moja baada ya kutoiamka tangu alipolala usiku wa jana. Taarifa hizo zisizo rasmi zinaeleza kwamba, nyota huyo alizidisha kiwango cha dawa za kulevya ambacho ndio chanzo...

Sitta: Asema JK alinihujumu

WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amewatuhumu viongozi wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa walishiriki kwenye njama ovu za kumnyang’anya uspika kwa sababu waliogopa spidi na viwango vyake. Sitta alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (SAUT), Mwanza. Ingawa Sitta hakuwa tayari kutaja majina ya viongozi hao waliomhujumu, ni wazi kuwa tuhuma hizo zinamwelekea moja kwa moja Rais Jakaya...

Dk. Mwakyembe aundiwa zengwe bandarini

MAKUNDI mawili yenye nguvu kifedha na madaraka katika mamlaka za Serikali yanapanga njama ili kukwamisha jitihada za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe. Makundi hayo yametajwa kutoka Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kwa pamoja wanadaiwa kuunganisha nguvu ili kupunguza kasi ya kuwafukuza watumishi wa bandari inayolenga kuziba mianya ya rushwa. Baadhi ya watumishi TPA waliliambia MTANZANIA kuwa mkakati huo ulianza baada ya Dk. Mwakyembe...

Jumatatu, 27 Mei 2013

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka

Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini. Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa. Chanzo...

Chadema yaipunguza kasi CCM Tabora

*Viongozi CCM wazomewa katika mkutano wa hadhara*Ni baada ya kuanza kuwatukana viongozi wa Chadema Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora, juzi walijikuta katika wakati mgumu, baada ya kuzomewa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara. Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa, akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, walipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi ya mabasi...

Fumanizi la mume wa mtu na shoga

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka na shoga aitwaye Aunt Steve na kuibua mtiti mzito. Tukio hilo lililovuta umati lilijiri Mei 20, mwaka huu kwenye gesti moja (jina tunalo) iliyopo Mwananyamala, Dar ambapo mke wa Ezekiel alivamia na kutembeza mkong’oto wa hasira kwa mumewe. ILIKUWAJE? Mei 19, mwaka huu, saa 3:15 asubuhi, mwanamke mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya heshima yake mtaani alilipigia simu...

Jumamosi, 25 Mei 2013

Ubaguzi kwa Waislamu waongezeka

Shirika la Uingereza la mchanganyiko wa dini mbali-mbali linasema jamii zimeingiwa na uoga tangu kuchinjwa kwa mwanajeshi wa Uingereza na Waislamu wenye siasa kali katika barabara ya mjini London. Shirika hilo, Faith Matters, limesema mashambulio yameongezeka sana tangu kuuwawa kwa mwanajeshi huyo siku ya Jumatano. Linasema limearifiwa visa zaidi ya 162 vya ubaguzi dhidi ya Waislamu katika siku mbili...

Rama mla vichwa vya watu aachiliwa huru, Je wamjua? - Bofya hapa usome zaidi

Dar es Salaam. Mshtakiwa Ramadhan Selemani Mussa, maarufu kama ‘Rama mla vichwa’, aliyekutwa na kichwa cha mtoto kikiwa bado kinavuja damu, pamoja na mama yake Hadija Ally, wameachiwa huru. Rama na mama yake walikuwa wakikabiliwa na shtaka moja la kumuua kwa makusudi mtoto Salome Yohana (3), kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Hata hivyo, jana Mahakama Kuu ilimwachia huru Rama baada ya kuridhika na ripoti ya jopo la madaktari waliomfanyia uchunguzi...

Ijumaa, 24 Mei 2013

Nini Siri ya mafanikio ya Bayern na Dortumund Kutinga Fainali UEFA? Bofya hapa uone siri ya mafanikio

Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borussia Dortmund Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo. Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri...

HABARI TOKA ZANZIBAR: Shehe wa Tumondo Zanzibar amwagiwa TINDIKALI

HABARI KWA UFUPI: Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia. Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua...

Alhamisi, 23 Mei 2013

KUMBE UINGEREZA NAKO UKEKETAJI UPO: Hebu soma hapa uone jinsi Wanavyoandamwa na Ukeketaji Uingereza

Ukeketaji au kukatwa kwa sehemu za siri za mwanamke , inadhaniwa kuwaathiri angalau wanawake 66,000 nchini Uingereza. Mara nyingine kitendo hiki hufanyika kwa wasichana ambao hurejeshwa nyumbani kwa jamaa zao Afrika Mashariki, lakini pia inaaminika kuwa wanawake wanakeketwa nchini Uingereza pia. Hata hivyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wanaotenda unyama huo lakini serikali inasisitiza kuwa iko tayari kuhakikisha kuwa ukeketaji unakwisha. ...

Mvutano kati ya Profesa Tibaijuka na NHC

Katika kesi hiyo, Li ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya China, alikuwa akilalamikia hatua ya kuondolewa kwenye nyumba Nambari 103 iliyopo katika vitalu namba 3, 5, 7 na 8, Barabara ya Haile Selassie, Oysterbay, Dar es Salaam. Kesi dhidi ya NHC ilifunguliwa mwaka 2006 wakati shirika hilo likiongozwa na Martin Madekwe na imedumu kwa miaka sita hadi Aprili mwaka jana ilipotolewa hukumu wakati shirika hilo likiwa chini ya Nehemia Mchechu aliyeteuliwa mwaka 2010. Katika hukumu yake ya Aprili...

Hali bado tete Mtwara

Mtwara. Wakati mtu mwingine akiripotiwa kufa, hali bado ni tete katika Mji wa Mtwara kutokana na mabomu ya machozi na risasi za moto kuendelea kurindima kwenye mitaa kadhaa wakati polisi wakipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam. Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi alithibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, linaloaminika kuwa linatokana na risasi. “Ni kweli kwa leo tumepokea maiti...

Wizi na uharibifu wa muda mrefu wa miundombinu ya umeme TANESCO - waziri wa Nisati na Madini Tanzania

Dodoma. Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limepata hasara ya Jumla ya Sh966.18 milioni kutokana na wizi na uharibifu wa miundombinu katika mikoa mbalimbali nchini, Bunge lililezwa jana. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka 2013/14. Waziri huyo alisema, kiasi hicho ambacho ni sawa na Dola za Marekani 603,862 kilipotea katika kipindi cha Julai 2012 hadi Aprili 2013 ambapo...

Jumatano, 22 Mei 2013

GESI IBAKI AU TUGAWANE NCHI - Kikwete akemea vikali vurugu Mtwara

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewaonya watu wanaosababisha uvunjifu wa amani nchini humo kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Onyo hilo linafuatia ghasia ambapo ofisi kadha, maduka na nyumba zimechomwa katika mkoa wa Mtwara ulioko kusini mashariki mwa Tanzania leo. Akihutubia kupitia televisheni ya taifa, TBC1, Rais Kikwete amesema wale waliokamatwa na polisi wakati wa ghasia hizo watashitakiwa. Ghasia hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa...

Kweli dunia imevaa bukta inatroti sasa hebu ona tena tukio jingine - Shambulizi la kigaidi mjini London

Mtu mmoja ameuwawa katika shambulio la mapanga na washukiwa wawili wamepigwa risasi na polisi katika mtaa wa Woolwich, kusini mashariki ya London. Waziri Mkuu David Cameron amesema kuna ishara nzito kua ni tukio la kigaidi na Uingereza haitaterereka wakati inakabiliwa na mashambulio kama hayo. Picha za video zimejitokeza zikimuonyesha mtu akipunga panga la kuchinja nyama na kutoa matamshi ya kisiasa. Akisema " Lazima tupigane nao kama wanavyopigana...

Mtwara Kimenuka: Fujo mtindo mmoja amani hakuna Bofya hapa ujionee mwenyewe

Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA  Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa)  Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.  Nyumba ya...

Tume yasema wakuu wawajibishwe Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake wametajwa katika ripoti inayowahusisha na ghasia za baada ya uchaguzi katika ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu ukiukwaji wa haki za bindamau nchini humo. Ripoti hiyo hata hivyo haikutoa mapendekezo ya hatua inazotaka kuchukuliwa dhidi ya Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto. Mwenyekiti wa tume hiyo, aliambia BBC kuwa ni kwa sababu wawili hao wanakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama...

Maalim Seif: Nitaomba kuwania tena urais mwaka 2015

Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ataomba tena kugombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV, Maalim Seif alisema kuwa anachoomba tu Mwenyezi Mungu ampe afya njema. “Ni uamuzi wa wananchi na wanachama wenyewe wa CUF lakini kama Mwenyezi Mungu akinipa afya na uzima bado nia ipo,” alisema Seif ambaye pia ni Makamu...

Bandari D’Salaam yapoteza Sh3 trilioni kwa mwaka

Dar es Salaam. Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikilikosesha taifa Dola 1.8 bilioni za Marekani (Sh2.8 trilioni) kwa mwaka, kutokana na kukosa ubora wa biashara. Kutokana na hali hiyo, wataalamu wameeleza kuwa bandari hiyo inahitaji kufanyiwa maboresho muhimu ya hali ya juu, ili fedha hizo zisaidie nchi kuacha kutegemea misaada ya maendeleo. Kwa mujibu wa ripoti iliyopo kwenye kitabu cha Opening the Gates: How the port of Dar es Salaam can transform Tanzania, licha ya Bandari ya Dar es...

Jumanne, 21 Mei 2013

Mapigano yaendelea kwa siku ya pili Goma

Mamia wanatoroka maeneo ya vita Goma  kukimbilia usalama wao Makabiliano kati ya jeshi na waasi wa kundi la M23 Mashariki mwa Congo yameendelea kwa siku ya pili. Pande hizo mbili, zilifyatuliana risasi mjini Goma huku kila upande ukituhumu mwingine kwa kuanzisha uchokozi na kuchochea mapigano. ...

Rais Obama ajiandaa kwa ziara Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama atazuru Afrika  kwa mara ya tatu Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuzuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya White house. Rais Obama atakutana na watunga sheria na wafanyabiashara pamoja na viongozi wa asasi za kijamii. Ziara ya Obama itaanza tarehe 26 Juni hadi 3 Julai na itakuwa ziara yake ya pili...

Lissu abadili mbinu uzinduzi kampeni

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anna Kilango akizozana na mnadhumu wa kambi ya upinzani, Tundu Lissu nje ya ukumbi wa Bunge jana baada ya Spika kuahirisha Bunge akiagiza hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kufanyiwa marekebisho. Ikungi. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya uzinduzi wa nafasi ya udiwani Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja, Wilaya ya Ikungi, Tundu Lissu, juzi alishindwa kuuza sera za Chadema, na badala yake...

MSIWAUE WAPENZI WA JINSIA MOJA. RAIS MSEVENI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja   Katika matamshi yake ya kwanza hadharani, kuhusu muswada huo, Rais Museveni amekariri kuwa suala la mapenzi ya jinsia moja halipaswi kupewa nafasi kukita mizizi. Muswada wa awali uliowasilishwa katika bunge la Uganda, ulipendekeza adhabu ya...

Page 1 of 5812345Next

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More