Akilitz Technologies

Ni wataalama walio bobea katika Teknologia ya habari na mawasiliano ya Kompyuta na mitandao ya inteneti

Jumanne, 30 Aprili 2013

Borussia Dortmund yapeta - Real Madrid 2-0 Borussia Dortmund

Borussia Dortmund imejikatia tiketi ya kuingia fainali ya Klabu bingwa Ulaya 2012-13 baada ya kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-3 dhidi ya Real Madrid. Real Madrid imeshinda 2-0  katika mechi ya nusu fainali  ya pili katika Bernabeu Jumanne. Lakini imeshindwa kusonga mbele kutokana na kipigo ilichopata cha magoli 4-1 Kutoka kwa Borussia Dortmund walipokuwa nyumbani wiki iliyopita. Upande wa timu hiyo ya Bundesliga ulinusurika kutolewa katika kinyang’anyiro hicho. Na kama Rael Madrid...

Jumatatu, 29 Aprili 2013

Majaji wamnusuru Jerry Muro na wenzake

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemnusuru aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili katika hatari ya kesi yao kusikilizwa umpya, badala yake itaendelea kusikilizwa kama rufaa. Awali kesi hiyo ilikuwa kwenye hatari ya kusikilizwa upya baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, kudaiwa kufanya makosa katika utoaji wa hukumu ya Muro na wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius  Mugassa. Hata hivyo leo...

GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

  Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha. Kwa sasa mamia ya wafuasi wa Chadema wanaandamana na mbunge huyo kuelekea makao makuu ya chama hic...

Iraq yaifungia Al-Jazeera, vituo vingine tisa

Seriakli ya Iraq imekifungia kituo cha televisheni cha kimataifa cha Aljazeera na vituo vingine tisa vya nchini humo siku ya Jumapili, baada ya kivituhumu kwa kuchochea vurugu za kidini. Hatua hii imemulika wasiwasi unaozidi wa serikali inayoongozwa na washia, juu ya hali ya usalama inayozidi kudorora, wakati wa machafuko ya waumini wa kisunni na makabiliano yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 180 katika muda wa chini ya wiki moja. Kusimamishwa kwa vituo hivyo ambako utekelezaji wake...

ALIYEZIKWA AKIWA HAI AFUKULIWA NA KUKUTWA AMEKUFA CHUNYA MBEYA

JENEZA LA ALIYEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUKULIWA MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUTOLEWA KABURINI   KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.    Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu  majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina...

Rais wa Algeria alazwa hospitalini Ufaransa

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amepelekwa mjini Paris Ufaransa kwa matibabu baada ya kupatwa na kiharusi. Bwana Bouteflika, mwenye miaka 76, alipata tatizo la mshipa wake wa damu kuziba kwa muda, hali ambayo inasemekana kuwa kiharusi. Jumapili, Madaktari walisema kuwa rais huyo anapata nafuu na kuwa athari aliyopata kutokana na kuziba kwa mshipa wa damu inaweza kutibika. Bwana Bouteflika anapokea matibabu katika hospitali ya kijeshi...

Nyumba nyingi kuporomoka nchini

Dar es Salaam. Imebainika kuwa nyumba nyingi zilizopo jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, zipo hatarini kubomoka kutokana na kujengwa kwa matofali yasiyokuwa na ubora. Pia, hatua hiyo inatokana na kutokuwapo kwa ukaguzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi yakiwamo matofali ya saruji yanayotumika katika ujenzi wa nyumba hizo. Uchunguzi uliyofanywa na Mwananchi hivi karibuni jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneo nchini, umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la biashara holela ya...

Yanga ijipange kwa mashindano ya Afrika

Timu ya soka ya Yanga ndiyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2012/2013. Yanga imetwaa ubingwa huo ikiwa bado imebakiza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Coastal Union na Simba. Huu ni ubingwa wa 24 kwa Yanga tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara rekodi ambayo hakuna timu yoyote ya Tanzania inayoifikia kwani Simba wanaowafuatia wametwaa ubingwa huo mara 18 tu. Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985,...

Mbowe amtwisha mzigo mzito Zitto

Tabora. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu ujao. Mbowe alisema chama chake kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki), Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015. Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo...

Lema kizimbani Arusha leo

Dar/mikoani. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema anafikishwa mahakamani leo kwa madai ya kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha, huku ikielezwa kwamba jiji hilo litakuwa katika ulinzi mkali. Ulinzi umeimarishwa maradufu katika mitaa yote jijini Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi anakoshikiliwa mbunge huyo tangu usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita. Lema anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo akidaiwa kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya wanafunzi kuchachamaa kutokana...

Jumapili, 28 Aprili 2013

DIAMOND PLATNUMZ AWATUPIA UJUMBE WAREMBO WA UINGEREZA

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’. Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke. Bila...

Arsenal yaibana Man United

Ligi kuu soka nchini Uingereza imeendelea kwa michezo mitatu iliyopigwa kwenye viwanja vitatu tofauti jijini London jumapili hii. Manchester United ambao ni mabingwa wa ligi hiyo msimu huu, Hii leo walikuwa wageni wa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates Kaskazini mwa london, Theo Walcot alianza kuifungia Arsenal bao la mapema kabisa dakika ya pili ya mchezo huo ambao BBC ulimwengu wa soka ilikuwa ikuutangaza moja kwa moja. United walio chini ya Sir Alex Ferguson walionekana kutokuwa kwenye...

Mambo matatu aliyohojiwa Lema Polisi

Arusha: Kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine. Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa kwake kungehatarisha amani. Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha kwa askari hao usiku huo...

Wafu wanavyofukuliwa, kisha kuzikwa wapya

 Siku zote tunaamini kuwa mtu anapofariki hupumzika kwa amani, lakini siku hizi wafu hao hawapumziki tena kwa amani, bali huamshwa, kisha, wafu wengine kushika nafasi zao. Ni kama vile muda wa marehemu hao kukaa kaburini umekwisha hivyo, nafasi zao zinatakiwa kutumiwa na wengine kutokana na uhaba wa maeneo ya kuzikia. Maeneo mengi ya kuzikia katika Jiji la Dar es Salaam, hasa yale maarufu kama Kinondoni, Sinza, Temeke na Kisutu yanapendwa zaidi na watu na sasa yamefurika. Kujaa...

CHADEMA KUMSHITAKI RC MKOA WA ARUSHA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Arusha (Chadema) kinafanya utaratibu wa kumfungulia mashitaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, dhidi ya kauli zake za uchochezi kwa chama hicho na vitisho kwa Mbunge Godbless Lema ambaye kwa sasa anashikiliwa na Polisi.Akizungumza na vyombo vya habari jana, Katibu wa chama hicho, Amani Golugwa, alisema tayari wameanza kufuata taratibu za kumfikisha kwenye vyombo vya sheria na karibu wanakamilisha kupitia wanasheria wao wa chama.Golugwa...

Jumamosi, 27 Aprili 2013

CHAMA CHA CUF CHAHUSISHWA NA FUJO ZA LIWALE

  MBUNGE wa Liwale, Faith Mitambo (CCM), amekishutumu Chama Cha Wananchi (CUF) kwamba ndicho kilichoasisi vurugu zilizotokea jimboni kwake. Mbunge huyo pia alilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti machafuko hayo na badala yake kuwaacha wafuasi wa chama hicho kufanya uharibifu wa mali za watu. Kwa mujibu wa mbunge huyo, katika vurugu hizo amepoteza nyumba zake mbili zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 100, huku wengine wakichomewa magari na maduka.Akizungumza...

POLISI WARUKA UKUTA KUMKAMATA MBUNGE LEMA

Maofisa wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne. Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo. Walifika nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini...

Ijumaa, 26 Aprili 2013

Lema: RC kanitumia ujumbe wa vitisho

Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.” Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa...

Alhamisi, 25 Aprili 2013

HATUA TANO MUHIMU KUELEKEA MAFANIKIO (High five to success)

  Maranyingi katika maisha yetu ya kilasiku tumesikia sana maneno kama “nipe tano” “chukua tano” maneno haya yamekuwa maarufu sana na katika mazingira tofauti maneno haya yamekuwa yakiashiria ushindi, au hali ya mafanikio au furaha baada ya hali fulani. Vivyo hivyo katika maisha yetu ya kutafuta kufanikiwa katika yaleyote tunayoyafanya kilasiku viko vitu au ziko hatua ambazo huwa zinatulazimu kuzijua au kuzipitia kama kweli tunamaanisha na tunayadhamiria hayo mafanikio tunayoyatafuta....

Page 1 of 5812345Next

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More